Utafiti: Asilimia 82 ya vijana wa Afrika wanaona ushawishi wa China kwa nchi za Afrika ni jambo chanya

Utafiti: Asilimia 82 ya vijana wa Afrika wanaona ushawishi wa China kwa nchi za Afrika ni jambo chanya

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
China Afrika 1.jpg


China imebadilisha uchumi wake katika miongo miwili hadi mitatu iliyopita na kujenga uhusiano wa kibiashara na Afrika.

Takriban miongo mitatu iliyopita, sehemu ya biashara ya China na Afrika ilikuwa asilimia 3 pekee. Hata hivyo, kufikia mwaka 2012, takwimu hizi ziliongezeka kwa kasi hadi asilimia 13.

Ingawa ukuaji huu unachochewa zaidi na maslahi ya China katika rasilimali za Afrika, idadi kubwa ya vijana wa Kiafrika wanaona ushawishi wa nchi hiyo barani Afrika kuwa wa manufaa.

Utafiti wa Vijana wa Afrika (African Youth Survey) uliofanywa na Taasisi ya Ichikowitz Family umeweka bayana kuwa mtazamo chanya dhidi ya China katika mataifa ya Afrika unaendelea kuongezeka miongoni mwa vijana wa bara hili. Ripoti hiyo imeonesha ongezeko la maoni chanya kutoka asilimia 78 mwaka 2022 hadi asilimia 82 mwaka 2024.

Utafiti huo uliofanyika katika nchi kadhaa za Afrika unaonesha kuwa mtazamo wa vijana kuhusu ushawishi wa China ni chanya sana nchini Rwanda na Chad, ambazo zote zilirekodi asilimia 96, zikifuatiwa na Kenya kwa asilimia 95 na Nigeria kwa asilimia 93.

Hata hivyo, kuna mashaka zaidi nchini Gabon (asilimia 60), Ethiopia (asilimia 63), na Namibia (asilimia 70), ambapo vijana wachache wanaona uwepo wa China kuwa wa manufaa.

Jack Ma, mwanzilishi mwenza wa Alibaba Group, na Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, walitambuliwa kama viongozi watakaokuwa na ushawishi mkubwa kwa Afrika katika miaka ijayo.
 
Back
Top Bottom