DolphinT
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 2,014
- 2,979
Elimu ni mkusanyiko au muunganiko wa stadi, maarifa na ujuzi anakua nao mtu baada ya kuupata kwa njia mbali mbali, rasmi na zisizo rasmi. Katika elimu yetu ya Tanzania ambayo ina mfumo wa elimu ya awali mpaka chuo kikuu imegawanyika katika miaka mbali mbali ambayo mwanafunzi anatakiwa kusoma ili kupata stadi zinazohusika baada ya kuhitimu. Huu ni mfumo rasmi tuliyojiwekea kwa mujibu wa mtaala wetu wa elimu kama taifa.
Kwa takribani miaka mingi tumeshuhudia mabadiliko kadhaa yakijitokeza katika mfumo wetu wa elimu ukienda sanjari na matamko mbambali ya viongiozi wetu wa serikali ambao kwa namna moja ama nyingine wana nia njema ya kuboresha utoaji wa elimu kwa vijana wa kitanzania ili kuendana na kasi ya maendeleo ya nchi pamoja na mabadiliko ya mambo mbalimbali kisiasa, kijamii na kiuchumi katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
Ni jambo la kusikitsisha sana kuona vijana wengi wakihitimu elimu katika vyuo vikuu na vile vya kati wakilundikana mitaani na malalamiko ya ukosefu wa ajira pamoja na stadi za maisha ikiwemo kujiajiri na ujasiriamali. Haya ni matokeo ya kukosekana kwa utafiti ama utekelezaji wa utafiti katika mfumo wa elimu hasa katika suala la kuzingatia mahitaji ya rasilimali watu na fursa za ajira zilizopo katika sekta binafsi na sekta ya umma
Tafiti zinapaswa kufanywa na wakala au idara za serikali pamoja na sekta binafsi hasa katika muelekeo wa mahitaji ya rasilimali watu katika soko la ajira katika kipindi fulani. Na tafiti hizi zinapaswa kuwekwa wazi kwa watanzania hasa wanaohitaji elimu katika ngazi mbalimbali ili kujua ni fani zipi zitahitaji ajira na kwa kiasi gani kwa maana ya wahitimu
Tafiti katika elimu zinazofanywa na taasisi husika hasa za elimu ya juu, watu binafsi, serikali na mashirika zinapotumika kikamilifu zitaisadia serikali na sekta binafsi katika kupanga mahitaji ya kimiundo mbinu hasa panapokuwa na takwimu sahihi za mahitaji ya vyumba vya madarasa, nyumba za waalimu pamoja na mahitaji ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu na mafunzo pamoja na mwelekeo wa mahitaji ya rasilimali watu katika soko la ajira. Hii kwa kiasi kikubwa itaondoa ujenzi wa muda mfupi na wa kushtukiza hasa tunapogundua kwamba idadi ya wanafunzi ni kubwa kuliko idadi ya wanafunzi.
Tafiti hizi zitatoa muongozo kwa serikali na taasisi zake katika kupanga mahitaji ya wanafunzi watakaodahiliwa katika ngazi zote za elimu kwa maana ya mahitaji ya walimu, mahitaji ya kifedha pamoja na vifaa vya kujifunza na kufundishia katika ngazi zote za elimu na mafunzo.
Sanjari na hili tafiti hizi zitatoa mwelekeo wa kisera katika elimu na mipango ya kiuchumi kwa muda uliopangwa na hivyo kuwezesha kuwa na mfumo imara wa utoaji wa elimu utakaobana wanasiasa ambao matamko yao yanasababisha kuyumba kwa suala zima la utoaji wa elimu bora.
Katika eneo la ubora wa elimu inayotolewa tafiti zinahitaji kufanyika ili kukidhi mahitaji ya elimu ya sasa na mazingira ya Tanzania; Ni vyema serikali ikweka bayana nini vishiria vya elimu bora tuitakayo kwa kuhusisha wadau mbalimbali wa elimu na wa maendeleo. Ni vyema tafiti zikafanyika na kutumika kikamilifu ili kuvipata viashiria hivyo na kuweka mpango stahiki kuhakikisha kuwa viashiria hivyo vinafikiwa. Eneo hili linahitaji utafiti wa kina kwa kushirikisha wadau wengi na pia uwepo utashi wa kisiasa katika kutekeleza maazimio yatakayofikiwa.
Ubora wa elimu hauwezi kutenganishwa na ubora wa walimu na wakufunzi wenye dhamana ya kutoa elimu husika, hali kadhalika maafisa elimu na mamlaka mbalimbali zilizopewa dhamana ya kusimamia utoaji wa elimu hiyo lazima ziwajibike ipasavyo. Tafiti lazima zifanyike na kutukika kikamilifu ili kujua kama walimu na wakufunzi tulio nao wana stadi za kutosha pamoja na uwezo wa kuwasaidia wanafunzi kupata maarifa na stadi zilizokusudiwa? Hii itasaidia katika kupanga namna ya kuwanoa walimu na kuwaongozea ujuzi kwa kuwapatia mafunzo kazini ili kuhakikisha ufanisi kwa kazi wanayofanya. Hali kadhalika itasaidia kujua mahitaji pamoja na changamoto wanazokutana nazo katika utoaji elimu na kuzipatia ufumbuzi. Bila kuwa na tafiti na kuzitumia kikamilifu ni dhahiri kwamba uwekezaji katika elimu utachukua muda mrefu kufikia malengo yake.
Ni dhahiri kwamba watanzania tutahitaji kujua thamani ya uwekezaji unafanywa na serikali katika elimu kwa sasa, kwa njia ya mikopo hasa kwa elimu ya juu pamoja na ruzuku inayotolewa kwa ajili ya shule za msingi na sekondari za umma maarufu kama elimu bila malipo. Tafiti lazima zifanyike ili thamani ya fedha inayowekezwa isiwe kuzalisha daraja sifuri, bali matokeo chanya kwa ajili ya mustakabali mzuri wa taifa letu. Wahitimu katika gazi husika ya elimu lazima wawe na stadi stahiKI zitakazowawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha kiuchumi na kijamii, na hivyo kujiletea maendeleoa binafsi, jamii husika na taifa kwa ujumla.
Tafiti makini zinapotumika kikamilifu huwasaidia watunga sera na taasisi za ukuzaji mitaala kuandaa mitaala itakayoendana na mahitaji ya taifa, na hivyo kuja na mwelekeo kabambe ambao utasaidia taifa hasa katika uwekezaji katika elimu. Sambamba na hilo watazania na hasa wazazi watapata wakati mzuri wa kuwasaisia na kuwaelekeza watoto wao kipi cha kusoma na kwa wakati gani katika hatua ipi; ili baada ya kuhitimu masomo yao kusiwe na mlundikano wa watafuta ajira bali watengeneza ajira kwa ajili ya kukuza uchumi binafsi na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Nitoe rai kwa serikali kuhakikisha kuwa tafiti zinafanyika katika elimu na kutumiwa kikamilifu na watunga sera pamoja na watekelezaji wa mipango ili kuongeza tija katika suala zima la utoaji elimu kwa watanzania. Hali kadhalika serikali kuhakikisha kuwa inapitia mitaala upya na kufanya marekebisho stahiki ili kuendana na mabadailiko ya dunia sasa. Sera ya taifa katika elimu iwekwe wazi na kuwepo na mfumo rasmi wa elimu usiobadilika badilika mara kwa mara katika ngazi zote za elimu.