Utafiti: Mada za Corona viz a vis mada nyingine kwenye forums mbalimbali

Utafiti: Mada za Corona viz a vis mada nyingine kwenye forums mbalimbali

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwa muda sasa tangia ugonjwa wa Corona umeingia miye kama mdau katika maisha ya kawaida nimekuwa nikifuatilia mwelekeo wa ugonjwa na wa mada katika forums mbali mbali.

Kote mada trending zimeendelea (kama si zote) kuwa ni za kuhusiana na Corona.

Nadhani ni kwa sababu kama hizo ndiyo maana hata mkuu katika hotuba yake tokea kule Chatto alilazimika kulisemea hili la habari za Corona vilivyo.

Hali ni hivyo hivyo pia humu JF.

Hata hivyo tofauti na kwingine (humu JF), kwenye majukwaa yote ya siasa, mchanganyiko, historia nk, kumejaa vi utitiri vya mada mbalimbali. Mkuu ooh CHADEMA, CCM, takukuru, SGR, nk. Hapa chini ni kama ilivyo hali ya trending mada hapa JF kwa sasa:

IMG_20200516_085252_391.jpg

Mada zote ziko kwenye Corona na hii ndiyo habari kubwa.

Kwa logic ndogo tu, kama trending zote ziko katika Corona, ni wazi kuwa nyingi ya hizi zisizohusiana na habari kubwa kwenye trending ni mada uchwara zenye msukumo zaidi wa kujaribu kuhamisha milingoti ya magoli katikati ya mchezo.

Hatudanganyiki.

Uhai wetu kwanza.

Corona haikubaliki!
 
umesema kweli.

Ingawaje kuna maisha nje ya korona, hivyo hatuwezi kuwa tunazungumzia korona tu.

Lakini ni kweli propaganda zozote zinazo anzishwa kwa lengo la kuwatoa watu katika attention ya korona, HAZIKUBALIKI.

Kwa sababu korona ipo.
 
umesema kweli.

Ingawaje kuna maisha nje ya korona, hivyo hatuwezi kuwa tunazungumzia korona tu.

Lakini ni kweli propaganda zozote zinazo anzishwa kwa lengo la kuwatoa watu katika attention ya korona, HAZIKUBALIKI.

Kwa sababu korona ipo.

Ni kweli hatuwezi kuwa tunaongea Corona tu Ila ni wazi pana watu wanakereka mno kuona kuna Corona inaongelewa.Haijulikani ni kwa maslahi gani.
 
Ni kweli hatuwezi kuwa tunaongea Corona tu Ila ni wazi pana watu wanakereka mno kuona kuna Corona inaongelewa.Haikulikani ni kwa maslahi gani.
Kwa vyovyote itakavyo kuwa maslahi hayo hayata kuwa kwa wananchi maana wao ndio wanaoathirika na janga hili.
 
Back
Top Bottom