kijanamtanashati
JF-Expert Member
- Aug 22, 2014
- 516
- 905
Sio mpenzi sana wa mitandao ya kijamii lakini leo nimeamuwa kupita uko instagram kujionea nini kinaendelea kati ya SEDUCE ME ya kiba na ZILIPENDWA ya wcb, cha kustaajabu mpaka sasa tangu nyimbo hizo mbili zitoke ZILIPENDWA imekuwa shared mara 15,626(hizi ni kwa zile post za public tu na kwa mtandao wa instagram tu) lakini hali iko tofauti kwa SEDUCE ME kwani hata ukujaribu kusearch kwa post za public hazionyeshi unaambiwa "Sorry,this page isn't available" Sasa kwanini kiba wameamua kublock hii hastag ya seduce me? ni kuogopa kuumbuka kwa janja janja yake au vipi? kwa maana kama nyimbo imekubalika hata share yake itakuwa kubwa tu, hii inawezekana SEDUCE ME ina share ndogo, ili kuzima soo ameamua kublock hashtag hiyo. Kama amefanya hivi basi kuna uwezekano kabisa hata zile views zilikuwa za magumashi na ndio maana mpaka sasa zimekwama haziendi kabisa. Tuweke ushabiki pembeni je, wewe unadhani kwanini ali kiba ameblock hashtag ya seduce me on instagram?