Utafiti uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali TWAWEZA umeonyesha kwamba asilimia 53 ya wananchi waliohusishwa kwenye tafiti hiyo wameridhishwa na maboresha ya huduma za afya zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita.
Ukweli juu ya tafiti hiyo unathibitishwa kupitia ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya 305 ambavyo vipo karibu na wananchi hali inayowapelekea kupata huduma bora za afya kwa haraka pasipo kutembea umbali mrefu kama hapo awali.
Pia, serikali imetoa ajira kwa watumishi wa afya 1650 na kuongeza maslahi yao ikiwa ni moja ya mkakati wa kuwezesha ongezeko la ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi.
Katika kuhakikisha huduma za afya zinapatikana, serikali imepunguza gharama za dawa na vifaa tiba ili kusaidia wananchi waweze kupata huduma bora na sio bora huduma.