Baadhi ya wana CCM wamekipaka matope sana chama chetu sababu ya ubinafsi wao. Kilichotokea kwa baadhi ya majimbo husuani Sengerema ni aibu. Mabepari na watoa rushwa hasa jimbo la Sengerema waliwahonga wapiga kura kila kata.
Masharti yalitolewa kwa makatibu kata na viongozi wengine wanapokwenda kupiga kura kwa pamoja sharti waangalie kila mtu kampigia nani kura. Hapakuwa na utaratibu wa siri kuwa mmoja mmoja anaingia kwenye chumba cha kupigia kura na kupiga kura kwa siri. Hii iliwafanya waliopokea rushwa kulazimika kuwaonyesha viongozi wao kura zao wamezipiga kwa nani kama ushahidi.
Inasemekana mwaka flani, bepari mmoja katika jimbo hilo, alitoa sana rushwa lakn hakushinda. Baada ya matokeo akawa anawafuata wote aliowapa pesa na kuwatishia na silaha warudishe pesa zake. Mwaka huu ndo ikabidi strategy ibadilike ya kuzichunga kura. Inasemekana bepari huyo alimfuata hadi Mkurugenzi wa uchaguzi kuomba mwongozo siku moja kabla ya kura kupigwa eti kwa nini CCM imezuia wagombea kusafirisha wapiga kura?
Kwa upeo wake mdogo huyo mgombea alisikika mara kadhaa hadharani akilalamika kwa Mkurugenzi kuwa kwa nini wanamzuia asisafirishe wapiga kura wake. Kwa upeo wake aliamini wapiga kura huko kwenye kata walikuwa mali yake. Alipoeleweshwa, alikataa na kumpigia K.MKUU na kumtumia
text kulalamika na K.MKUU naye akaforward message tena kwa Mkurugenzi wa wilaya kutaka maelezo ya huyo bepari. Ushauri wangu ni kwa vyombo ya usalama na maadili kufyeka wote waliopatikana kwa harufu ya rushwa.
Ninaamini ni wachache tu na siyo majimbo yote. Tusipodhibiti tamaa ya rushwa na madaraka, mwaka huu tutapata wagombea wa hovyo kabisa. Ikiwezekana hata mishahara ya wabunge ipunguzwe ili ku-discourage rushwa kubwa sana kwenye kura za maoni. Wachaguliwe wagombea safi waliotosheka na wasio na tamaa na wakubali mishahara na posho zao kupunguzwa ili zikatumike kujenga hospitali, mashule na miundombinu ya maji.
MUNGU IBARIKI TANZANIA