Utafiti: Ushuzi unaotokana na Kujamba, una uwezo wa kutibu Saratani

FikraPevu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2010
Posts
304
Reaction score
236
UTOAJI wa ushuzi, katika mazingira yoyote yale, umekuwa na matokeo tofauti katika jamii yetu ya Kitanzania. Watu wanaotoa ushuzi au kujamba mbele za watu, huonekana mbele ya watu hao kama watu wasio kuwa na adabu, hivyo kudhalauliwa wakati mwingine.

Hata hivyo, taarifa za kitafiti za kisayansi, zinaweka wazi kwamba kutoa ushuzi au kujamba, ni afya. Kwa mujibu wa wataalam hao, kila mnyama kwa maana ya viumbe wote walio katika kundi la wanyama kisayansi, binadamu akiwemo, wakati fulani hujihisi tumbo kujaa gesi nyingi (kuvimbiwa), hivyo njia pekee ya ufumbuzi wake katika kuondokana na shida hiyo, ni kupunguza gesi hiyo kwa njia ya kujamba.

Kwa mujibu wa taarifa hizo za kitafiti, katika idadi yote ya viumbe hai vinavyojamba, mchwa anaongoza kuliko wanyama wengine wote. Aidha, mchwa huyo huyo anadaiwa kuchangia kupanda kwa joto la dunia (global warming) kwa kiwango kikubwa kwa kuwa huzalisha gesi ya methane kwa wingi kupitia njia hiyo ya kujamba. Kwa kawaida, gesi ya methane na hydrogen inaweza kusababisha moto.

Tafiti mbalimbali ambazo FikraPevu inazo, zimebainisha kwamba.

Habari zaidi, soma=>Utafiti: Ushuzi unaotokana na Kujamba, una Uwezo wa Kutibu Ugonjwa wa Saratani
 
Hata kapiga chafya ni dalili ya kuwa na afya. Ndiomana uislam umefundisha mtu akipiga chafya amshukuru MwenyeziMungu.
 
Basi Kama Kweli Huu UTAFITI Unafanya Kazi Nadhani Sitakuja Kuumwa Ng'o Saratani Yenu Kwani Hakika Najitahidi Mno Kutoa Pafyumu Adimu.
 
Sisi tunaokula kunde huku kusini mwa Tanzania, hiyo saratani tutaisikia humu kwenye mitandao.

Mkuu Mbavu Zangu Zikipata Mushkeri Na Kuvunjika Kwa Hiki Ulichokiandika Hapa Utanipeleka Hospitali. Nimecheka Mpaka Basi. Akhsante!
 
Mmmh mm skaagi chumba moja nakibonge mpenda kulakula hata siku aniumize pua naona huo utafiti km kweli huko kwenye mabasi sjui itakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…