Utafiti usio rasmi: Wanaosinzia kwenye daladala wanavuta hewa chafu

Utafiti usio rasmi: Wanaosinzia kwenye daladala wanavuta hewa chafu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baraza la Taifa la Uhifadhi Mazingira (NEMC), limezitaka taasisi za utafiti nchini kufanya utafiti kufuatia kuwepo kwa tafiti zisizo rasmi zinazoeleza kwamba, ukataji miti hovyo unafanya hewa ya ukaa kuongezeka na kusababisha watu wanapopanda kwenye daladala kuanza kusinzia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi la upandaji miti Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Hamadi Kisiwa amesema watu hao sio kwamba wanasinzia wana usingizi lakini ni ile hewa wanayovuta imekuwa na Carbon dioxide nyingi tofauti na watu wanapopanda magari yaliyofungwa vioo.

Kuhusu umuhimu wa kupanda miti kwenye jamii Meneja huyo amehimiza kuwepo kwa utaratibu wa mara kwa mara wa kupanda miti hasa shuleni ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa utunzaji wa mazingira.

Chanzo: EATV
 
Kwa hiyo sisi tunaoendesha bila kufunga vioo kuna siku tutajikuta mtaroni kwa kuvuta hewa ya ukaa?
 
Back
Top Bottom