JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Vichungi vya sigara (vitako) ni kati ya vitu vyenye uchafuzi na sumu vinavyopatikana katika vyanzo vya maji, pia inachukua hadi miaka mitano kuoza vikitupwa ardhini, hiyo kuruhusu nikotini na kemikali kuingia kwenye mifumo ya ikolojia inayozunguka ambayo inaathiri maisha ya binadamu.
Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uinaonesha vichungi vinapowekwa kwenye maji vinaweza kutoa kemikali ambazo huweza kusababisha vifo vya viumbe wa majini wakiwemo samaki.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameshauri wataalam wa Tanzania nao wafanye utafiti ili kubaini kwa nini vichungi vinachelewa kuoza kuliko koili za chuma, plastiki na betrii...