Utafiti wa jeli ya kupambana na HIV

Utafiti wa jeli ya kupambana na HIV

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363




121129162616__64436021_c0121954-hiv_particles_artwork-spl.jpg
Kirusi cha HIV


"Kuna densi kati ya virusi na kinga ya mwili'' anasema Daktari Angela obasi kutoka taasisi ya utafiti wa matibabu nchini Uingereza.
"Wakati tunapopata uelewa zaidi kuhusu virusi hivi ndipo tunaelewa densi hii"




Ufafanuzi huu wa virusi hivi, unaweka wazi hali halisi ya tabia ya virusi vya HIV, kama densi ngumu ambayo haieleweki, ni ngumu sana kutabiri nana hivyo ngumu kukabiliana nayo.
"Kila wakati unapokuja na mbinu ya kukabliana na virusi, virusi hivi navyo vinabuni njia yake ya kupamba na Makati ule, " anaelezea mtafiti mkuu katika taasisi hiyo na ambaye amekuwa akitafiti kuhusu HIV tangu mwaka 1996.
Utafiti wa hivi karibuni kuhusu mbinu za kukabiliana na HIV, ni mafuta au jeli, ambayo inaziba sehemu muhimu ya kinga mwilini na kuzuia virusi kuingia katika seli za mwili.
Haya mafuta, yaliyozinduliwa na kikundi cha watafiti wa kimataifa kina umiuhimu mkubwa katika kuziba kuta za kinga ya mwili ambazo virusi vya HIV hupenya ili kuvamia celi za kinga ya mwilini.


""Wanawake wengi wanashindwa kujilinda dhidi ya virusi vya HIV''"




"Kwa kutumia jeli hii, seli za kinga ya mwili, za ,CD4 ambazo ni muhimu kwa waathiriwa wa virusi vya HIV,hulindwa dhidi ya kushambuliwa " anaelezea daktari Obasi.
Mtafiti mkuu katika kutengezwa kwa jeli hii, ametaja matokeo ya utafiti wao kama yanayotoa matumaini makubwa.
Hata hivyo jeli hii imeweza kutumiwa tu kwa wanyama kuona ikiwa inafanya kazi itachukua muda wa miaka mitano kabla ya kutumiwa kwa binadamu.

Utafiti mwingine ambao ulifanywa awali na ambao ulitumia jeli kama huu au Microbicides, umekuwa na changamoto nyingi sana katika vita dhidi ya virusi vya HIV.
Uchunguzi huu ulioleta matumaini makubwa, ya jeli za Microbicide, ulifanyika mapema miaka ya tisini, wakati jeli ijulikanayo kama (nonoxynol-9), ambayo inatumika katika mipira mingi ya condom, iliyojulikana kuua virusi vya HIV.
Lakini baada ya utafiti zaidi kufanywa, iligunduliwa kuwa , jeli hiyo ilikuwa na athari zaidi katika kuchochea maambukizi kuliko kukinga dhidi ya virisi vya HIV.
121211122528_hiv_virus_304x171_bbc_nocredit.jpg
Virusi vya HIV ni havisikii dawa


Kulingana na kampuni inayofanya utafiti huu wa Microbicide , Microbicide Trials Network, kuna bidhaa aina tisa zilizofanyiwa majaribio. Kulingana na daktari Obasi, baadhi ya jeli hizo zinaonyesha matumaini.

Katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, ambako janga hili limekita mizizi na ambako hali ni mbaya mno, zaidi ya asilimia 60 ya maambukizi mapya ni ya wanawake.

Daktari Obasi anasema kuwa " katika sehemu nyingi duniani, hasa katika nchi ambazo, zina visa vya maambukizi ya HIV, kuna

changamoto ya usawa wa kijinsia, hali inayoifanya vigumu kwa wanawake kudhibiti vyanzo vya maambukizi."

Kwa hivyo, nyenzo za maambukizi ambazo zinadhibitiwa na wanawake, zinaweza kuwapa nguvu kulinda miili yao dhidi ya maambukizi.

Wanawake katika nchi nyingi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, wanakumwba na unyanyapaa wakisisitiza kutotumia Condom kwa sababu inahusishwa na ukahaba.

Kumekuwa na ripoti nyingi za polisi kuwapokonya mipira yao ya condom wanawake makahaba katika baadhi ya nchi zikiwemo Kenya,

Namibia, Afrika Kusini na Zimbabwe ili kuzitumia kama ushahidi dhidi yao.

Mwaka 2011, jarida la New York Times, liliripoti,kuwa polisi nchini Marekani walikuwa wanatishia kuwakamata makahaba ikiwa
watapatikana wanabeba zaidi ya condom mbili.

Kutafuta tiba


Tiba ya ukimwi bado , na ikiwa itapatikana basi itakuwa tu katika chanjo.
Elimu kuhusu ngono na utumiaji wa mipira ya Condom ingali bado ni muhimu katika kukinga maambukizi.
120730075903_bbc_no_credit_namibia_hiv_304x171_bbc_nocredit.jpg
Wanawake wanakuwa na wakati mgumu kuweza kujilinda dhidi ya HIV


Moja ya kile kilichowachangamsha watafiti katika safari yao ya kutafuta tiba ilikuwa uchunguzi uliofanyiwa watu

16,000 nchini Thailand, na kupatikana kupunguza viwango vya maambukizi kwa thuluthi moja.

Mtafiti mkuu na mwanasayansi ambaye pia ni mshauri wa shirika la UNAIDS alisema jaribio hilo lilikuwa la kufana sana.

"Nadhani maoni yangu ni kuwa bado tuko mbali katika kupata chanjo, bado tunasubiri kupata mafanikio makubwa'' aliambia BBC

"kwa sasa watu watahitaji kuchanganya mbinu nyingi tu za utafiti ili kupata chanjo kamili siku moja''

"na hiyo haimaanishi kuwa tuwache kujilinda kama inavyosisitizwa kwa kutumia Condom na kufanya ngono salama.''

Kwa sasa hakuna tiba, lakini watafitio kama daktari Obasi wana matyumani kuwa tiba itakapatikana katika maisha yao ya utafiti. Lakini

kwa sasa jeli hii ambayo mtu anajipaka mwenyewe kabla ya kitendo cha ngono, ndio silaha ya leo dhidi ya maambukizi ya HIV.

chanzo. http://www.bbc.co.uk/swahili/kwa_kina/2012/12/121211_hiv_fight.shtml
 
Sasa jeli ndo silaha, na anasema we still have like 5years of experimenting with animals ili kufikia hitimisho kama inafanya akazi ama vipi. Which is which?
Kweli gonjwa limekaa pabaya. Sub saharan africa tunakwisha!
 
Ni bahati mbaya sana kuwa Ukimwi ni ugonjwa unaotokana na Virus,
kwani magonjwa yatokanayo na virus (mf. Polio, Surua, Serum Hepatitis,
Mafua ya nguruwe n.k) huwa hayana tiba maalum, mara nyingi wataalam
hutibu dalili zake. Tunachotakiwa kukazania ni chanjo na si tiba...
 
Yes 5 yrs. And after 5 yrs we will see if we need to add more 5 yrs or not. Remember this is just for EXPERIMENTATION.
Lakini kwanini Sub saharan africa? kwanini sisi?

Sasa jeli ndo silaha, na anasema we still have like 5years of experimenting with animals ili kufikia hitimisho kama inafanya akazi ama vipi. Which is which?
Kweli gonjwa limekaa pabaya. Sub saharan africa tunakwisha!
 
Lakini sisi hatuabudu ngono kama Ulaya. Au kwa sababu sisi tunapenda kufichamafichama katika mahusiano mtambuka yetu kiasi kwamba inawezekana tunaabudu sana kuliko Ulaya?. Lakini kwamba sisi tunaabudu sana ngono kuliko Ulaya inahitaji utafiti zaidi. Au kwa sababu sisi tunazaliana sana? maana Ulaya mtoto ni 1 au 2, Sisi hadi 5 siyo tatizo sana bila hata kujali vipato vyetu.

Maswali ni mengi. Lakini pia majibu ni ya kutafuta sana.

MziziMkavu tuache kuiabudu ngono na haya matatizo yatakwisha
 
Na Ugonjwa wowote unaotokana na Virusi huwa mara nyingi SIYO KILA MTU ATARUHUSIWA KUJIFANYIA TU UTAFITI NA KUJA NA MAJIBU YAKE, kunakuwa na control kubwa, watu wachache wataruhusiwa kutafiti kwa kulipwa mishahara mizuri hasa, ila kama wataanza (controlled watafiti) kuhojihoji nadharia za aliyegunduwa aina ya kirusi hicho, mengi yatatokea lakini mwisho aliyegunduwa aina ya kirusi hicho itabidi aendelee kulindwa.

Magonjwa mengi, narudia mengi ukienda hospitali daktari atajitahidi sana kuzisinziisha/kuzituliza DALILI za ugonjwa na siyo kuukomesha (yaani kukupa kinga) ugonjwa usikurudie tena siku zijazo.

We need to pray.

Ni bahati mbaya sana kuwa Ukimwi ni ugonjwa unaotokana na Virus,
kwani magonjwa yatokanayo na virus (mf. Polio, Surua, Serum Hepatitis,
Mafua ya nguruwe n.k) huwa hayana tiba maalum, mara nyingi wataalam
hutibu dalili zake. Tunachotakiwa kukazania ni chanjo na si tiba...
 
Back
Top Bottom