Antonia lujabuka
New Member
- Aug 20, 2022
- 2
- 0
UTAFITI WA KISAYANSI KWA VITENDO
Mama: Selvina nenda kalale kesho shule
Selvina: mama bado kidogo ndio inaishia
Mama: kalale haraka kabla sijafika apo kupiga
Selvina alizima TV na kwenda kulala. Ni binti wa miaka kumi na tatu alipenda Sana kuangalia video za sayansi ya anga. Kila siku alikuwa akifuatilia vipindi mbalimbali vinavyoonesha sayansi ya anga. Selvina alipohitimu darasa la Saba alifanikiwa kwenda kidato Cha kwanza.
Selvina alifanikiwa pia kuingia kidato Cha kwanza kwa matokeo mazuri Sana. Alisoma kwa bidii Sana na akifanya Mtihani wa Taifa kidato Cha pili na pia alifaulu kwa matokeo yaliyo ya juu na mazuri. Alikuwa ni binti mwenyewe bidii na malengo mazuri katika masomo yake, pia alipenda kusomea sayansi.
Pia alishauri wanafunzi wenzake kuwa wasomee masomo ya sayansi kuwa yanafaida kubwa Sana katika maisha yetu ya Sasa.
Selvina alikuwa na jitihada Sana katika kusoma kwake na pindi alipokuwa kiongozi alihamasisha wanafunzi wenzake wa like kuwa wajitahidi kusoma kwa sababu wakati huo watoto wa like kusoma walikuwa wachache Sana hivyo wajitahidi Sana kusoma kwa ajili ya kusaidia wazazi na jamii nzima, pia kwa sababu alipenda masomo ya sayansi alihamasisha wasome masomo hayo kuwa Kuna kazi nyingi, Kama vile ualimu, udaktari, urubani, uhandisi, udaktari wa mifugo, ata pia bwana kilimo.
Selvina alifanikiwa kumaliza kidato Cha nne kwa matokeo mazuri na alikuwa ( Tanzania One). Ilikuwa ni shangwe Sana kwa mzazi kumwona bintie akielekea katika mstari ulio sahihi. Pia akifanya vizuri katika elimu yake ya juu kidato Cha sita na kuwa wa kwanza kitaifa.
Mama: Selvina
Selvina: abee mama
Mama: hivi umemaliza kidato Cha tano Sasa unataka ukasome Yale unayoyaangaliaga kwenye TV au?
Selvina: Ndio mama nataka nikasomee sayansi ya anga.
Mama: mwanangu mbona vitu vipo vingi kijijini tunahitaji wakulima, pia wauguzi wapo wachache wewe unataka ukatumikie anga ili iweje, unataka kwenda kufa, watu wanaanguka na ndege wanakufa Kila siku, Mimi Kama mama ako sitaki uende kusomea hayo maujinga yako.
Selvina: (Kwa huzuni na machozi kumlenga) lakini mama.
Mama: sitaki Cha lakini( kwa hasira na jazba) kwanza hiyo Ela hakuna ya kupoteza.
Selvina aliumia Sana akifanya jitihada zote za kusoma kwa bidii ili malengo yake yaweze kutumia Ila mwishoni ni maumivu. Hakuishia apo alianza kufatilia suala la kutafuta wasimamuzi wanaoweza kumsaidia katika kumsomesha na hatimae alifanikiwa aje alipe fadhila. Alimtambua kuwa mpaka apo alipofikia wazazi wake wasingeweza nsaidia kwa chochote hivyo alijiongeza kwa namna hiyo.
Selvina alikuwa ni binti mwenyw bahati na alikuwa anapenda kusoma Sana hivyo pia kutokana na mtiritiko wake mzuri kimasomo alifanikiwa kumpata msimamizi ambaye alimpa Selvina nafasi ya kusoma achague anachotaka kusomea. Hakuwa mbali Sana na zile ndoto zake za toka utotoni alipenda aje asomee sayansi ya anga. Ilikuwa ni shangwe kwa Selvina japo kilikuwa Kuna ugumu wa kumweleza mama. Ila alichokifanya alizidi kufatia suala zima la kuomba na uchaguzi wa vyuo ambavyo vipo nje Kama vile MAI na MSTU GA vilikuwa ni vyuo vya ufundi.
Selvina alifanikiwa kuchaguliwa katika chuo kikuu Cha ufundi Cha Jimbo la Moscow Cha usafiri wa anga iko kwenye Kronstadtsky Boulevard kwa nambari 20 ( MSTU GA). Alijitahidi akapata Kila kitu kachohusiana na suala Zima la usafiri na alipofanikiwa kupata ndio alienda kumweleza mama pia kwa kuniaga. Mama hakua na namna nyingine kwa sababu zote zilikuwa jitihada za mwanae.
Selvina alifanikiwa kwenda kusoma kwa kipindi Cha miaka sita bila ya kurudi nyumbani. Alipendezwa kuwa Yale aliyokuwa akitazama kwenye TV ndio alikuwa akiyaona kwa macho na kufanya kwa vitendo. Alijiskia furaha Sana kwa sababu alijua namna ya kutumia vifaa vya anga vya eletroniki. Pia alishiriki (Olympiads) mikutano ya kimasomo ya kisayansi ya wanafunzi kufanyika Mara kwa Mara kwa nvhi mbalimbali. Alijua pia kutumia ndege za kisasa juu katika uwanja wa anga.
Selvina alihitimu taasisi ya elimu ya anga na hivyo alikuwa na nafasi ya kupata kazi katika utaalamu wake katika mashirika ya ndege, viwanda katika utengenezaji wa ndege, helikopta na teknolojia ya anga na vitovu vya anga.
Hivyo alichagua kuwa awe katika mashirika ya ndege alifanikiwa kupata kazi kirahisi kutokana na elimu aliyonayo.
Selvina alikuwa ni binti wa kwanza mwenye umri mdogo kuwa rubani katika nchi ya Tanzania. Alikuwa na sofa ya kipekee inayoweza kusaidia pia watoto wa kike kufanya nao wawe wenye kupambana na kufanya utafiti wa kisayansi kwa vitendo.
Hata mama Selvina alishawishika Sana na bintie hakuamini walikuja kusaidiwa nyumbani na kuishi maisha yaliyo mazuri na hivyo alipata nafasi ya kuzunguka na ndege nchi yoyote aliyotaka kwenda mama Selvina.
Hivyo utayari wa kufanya kufanya Jambo lipo mikononi mwako pia sayansi na teknolojia ndio dunia ya Sasa kwa sababu hakuna ambalo litafanyika bila kutumia sayansi au teknolojia hivyo pia no vyema kujifunza.
Na pia ajira nyingi kwa Sasa zipo katika sayansi na teknolojia Kama vile mafundisho kwa kutumia kompyuta, utabibu, ukulima kwa dawa mbalimbali,sayansi ya anga na teknolojia ya simu.

Upvote
0