Utafiti Wa Synovate: CCM Hoi Zanzibar


Same old story. CCM haijawahi kushinda uchaguzi visiwani. Lakini inaendelea kuongoza. It will be same story this time around, CUF watashinda, watapigwa mikwaju na CCM itatawala. Uchaguzi Zanzibar hauwezekani ni porojo tu na geresha.
 
wacha kujichanganya ndugu yangu. Inawezekana CUF ikapata satuwa ya kuongoza nchi- kama wenyewe wananchi wataamua hivyo, na wataoongoza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa mujibu wa katiba. Lakini Seif kamwe hawezi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar. Huo ndio ukweli. Sasa na tuende katika kisanduku cha kura tukamue huko.
 
kuhusu matokeo ya bara watachekeleaa ila visiwani lazimaa wayapingee sanaaaaa....

sasa sijui kwa nini wasikatae ripoti nzimaa ya utafiti huooo...
 
Kwani tukisema katiba zetu zinamapungufu hamjuwi tunalenga nini, katiba zote mbili zimekaa kichama chama tu, hazina sura ya kitaifa ku-fit matakwa ya nyakati za sasa na zijazo, katiba ya Zanzibar imtungwa utafikiri ku serve chama cha Mapinduzi peke yake na kama vile wana guarantee kuwa watatawaka maisha. Pakacha, hivyo ndo katiba inavyosema kuwa " rais" ni "rais wa zanzibar na Mw'kiti wa baraza la Mapinduzi", tuseme CUF wasipewe serikali hata wakishinda vipi, itakuwaje miaka 50 ijayo(sisi tutakuwa hatupo pengine) na katiba ipo kama hivyo, chama kisichokuwa CUF wala CCM kinashika dola(lets say Alternative Force), watatawala kwa katiba ipi kama si hiyo, rais wa Serikali ya Alternative Force ataitwa vipi kinyume na katiba hiyo, na Cabinet yake itaitwaje kama si BLM?
Hivyo ndo katiba inavyosema si ushabiki hapa Pakacha!!
 
Junius ukitaka kuyasarifu hayo mambo ya watu inabidi ufanye analysis kamili. Baraza la Mapinduzi (kwa kweli ni Baraza la Mawaziri). Baraza la Mapinduzi unalosema wewe limevunjika pale wakati ule lilipoundwa Batraza la wawakilishi. Baraza la \mapinduzi ni jina tu limeluwa "retained" for historical purpose na nia ya kuheshimu yale M apinduzi ya 1964. Junius nafikiri ungepata bahati ya kuzungumza na wazee kama Mzee Aboud Jumbe akakufahamisha vitu kama hivyo. sasa Baraza la Mapinduzi hilo lilobaki na jina kuna wajumbe pale kama kina Bi Asha, Samia, Mansour, Machano - hata hayo Mapinduzi wanayajua hao? Historia ibakishe kuwa historia-usijichanganye.
 
"Rose by any other name...."
 
"Rose by any other name...."
Haya makubwa! Mbona semantics za Pakacha kuhusu BLM hazieleweki.

He knows nothing and he thinks he knows everything.That points clearly to a political career.Bernard Shaw,Irish Playwright and Dramatist
 
Wale walipewa taarifa tu kuwa kuna Mapindunzi...Uchungu wa mwana aujuae mzazi
 
Junius, habari ndio hiyo 😀 Then kichwa cha bandiko lako kimekaa ndivyo sivyo... CCM inaweza kuwa hoi PBA tu!

Nafikiri hujafanya utafiti kwanini SMZ inaweka pingamizi wasiandikishwe kule Pemba. Pengine huelewi kuwa Pemba kuna mwamko mkubwa wa kisiasa na kuna idadi kubwa kule ya vijana wasio na shughuli nyengine bali kujiingiza katika siasa kuliko Unguja ambako vijana hawana mwamko wa kisiasa na badala yake wanashughuli nyengine zaidi ya siasa.
Sasa ukifanya hesabu juu ya kiwango kidogo cha ushindi unaopatikana na CCM unaweza kuona hatari ya kuachia kila anaestahiki kupiga kura kule Pemba kupewa nafasi ya kuandikishwa kwenye Daftari
 

Kushindwa kwa CUF kutaendelea kwa vile kunapangwa na Serikali ya Muungano. Basi.
Haitowezekana kwa CUF kusifia Mapinduzi kwani hiyo ni sera ya CCM kule visiwani, kwani hawana cha kukionyesha zaidi ya propaganda ya Mapinduzi na usultani. CUF inapata sapoti kubwa Unguja kwa sera ya CCM ya Mapinduzi daima na siku ambayo CCM itaacha sera hiyo basi ndio kifo cha CUF kwani hapo kitakuwa chama cha Wapemba peke yao.
Aidha umaarufu wa Mapinduzi unaanza kufifia kwa vile yale mambo yote yaliyoletwa na Mapinduzi yanapuuzwa na CCM na badala yake kuleta hali ngumu zaidi hata kabla ya Mapinduzi. Imefika wakati sasa Wazanzibari wengi wanakumbuka mambo mazuri yaliyokuwepo kabla ya Mapinduizui. Angalau wakati ule ungepata matibabu bure, elimu bure, maji bure na viongozi hawakuwa hakiwanyanganya wananchi ardhi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…