Kuna taarifa kuwa Synovate wapo njiani kutoa matokeo ya maoni ya watanzania kuhusiana na uchaguzi 2010.
Wasiwasi wangu ni kuwa bado watatumia sampuli ya watu 1,000 - 2,000 ambapo huenda wasipate uhalisia wa mambo ingawa report yao itaweza kutumiwa na baadhi ya wagombea kisiasa. Kwakuwa sijajua nini kitaongelewa basi fuatilia comments chini...
Tutarajie nini?
Mimi nafananisha kampeni ya CCM kuwa sawa na mashua iliyoundwa kwa mti wa mpodo, ambao hauwezi kustahimili vishindo vya maji ya chumvi kwenye bahari kubwa ya Tanganyika, huku nahodha wake, JK, akijitahidi kuchota maji ndani yake ili isizame kwani mashua ina matundu mengi yanayoingiza maji ndani (soma: hoja zisizo na msingi na ahadi kede kede zisizotekelezeka na za uongo...). Kadri jinsi nahodha JK anavyojitahidi kuchota maji, kumbe ndivyo anavyozidi kuadhirika, kwani sasa matundu yanaongezeka na kuwa makubwa, mashua inazidi kuzama baharidi.
Kwa upande mwingine - hapa ngoja nizungumze kwa Kiitaliano kidogo.... Inoltre, nell'alta parte ... mashua inayoongozwa na nahodha wa CHADEMA, Dk. Wilibrod Slaa, imeundwa kwa miti ya mitiki, ambayo ndiyo haswa inayofaa kwa safari za baharini, kwenye maziwa na mito. Slaa hana tatizo la kuchota maji toka ndani ya mashua yake ya kampeni; haina matundu yoyote. Kila kitu ni shwari. Anaendelea, polepole na salama. Hana shida. Ingawa CCM wanajaribu kurusha makombora kuiharibu mashua, mitiki inastahimili vishindo, hakuna madhara. Ila makombora wanayorusha kumbe yana milipuko inayobaki nyuma, kwa hiyo wanazidi kuharibu mashua yao ya MPODO!
Utafiti wa Synovate na Redet ni mojawapo ya makombora ambayo ni mapya, yaliyoandaliwa na CCM, kujenga hoja (isiyo na msingi) kumvika JK joho lililotengenzwa kwa kioo, ambalo pindi atakapolivaa litapasuka LOTE! Matumizi ya pesa yasiyo na tija, kufanya utafiti usio na kichwa wala miguu, kupoteza muda na malengo! HAWAWEZI! Muda watapoteza, malengo yako pale pale. Wote tunajua, hawa ni wapiga debe wa mfalme JK, ambao hawana ubavu wa kusema, Mfalme yuko uchi, hajavaa nguo. Wataendelea kusema, Jamani mfalme amependeza na nguo yake yenye vito vingi vya almasi, rubi na dhahabu! Wapi! Mwambieni ukweli mfalme wenu; hajavaa nguo! Mnamdanganya, mnampotosha, kwa kutaka sifa kwake! Siku akiwagundua mtakiona cha mtema kuni!
-> Mwana wa Haki
UFISADI utatupwa nje tu! Wala tusibabaishwe na Synovate!