Utafiti: Wana JF na Avatar zao

Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
5,814
Reaction score
8,118
Nimekuwa nikifanya utafiti kwa miaka miwili sasa juu ya tabia za wana JF kwa kutumia aina za avatar wanazotumia. Mpaka sasa nimekutana na members zaidi ya 30 humu.

Kiukweli avatar wanazopendelea kuweka zinafana sana na maisha yao halisi au vile walivyo nk. Au kwa lugha nyingine zinatoa preliminary background ya jinsi walivyo. Ukiona member kaweka avatar ya mrembo mkali, asee ni mrembo kweli si mchezo. Ukiona member kaweka picha la jamaa lina hasira, basi ujue yuko hivyo. Ukiona jamaa kaweka picha ya ya kiroho-mbaya ujue anakaribiana na sifa hiyo. Ukiona kaweka avatar ya kituko fulani hivi, naye ni kituko. Kadhalika na wenye avatar za ki hekima hekima, ni kweli kabisa wapo hivyo. Walioweka picha za wanyama, relatively wana maamuzi na matendo kama ya wanyama. Na wale wasioweka picha means they don't care, na kweli wenyewe wako laissez-faire tu.

Huu utafiti unatoa mwangaza mpya wa aina ya wana JF unaopanga ima kukutana nao au unapochat nao kuwajua japo kwa uchache tabia na mwonekano wao (imaginary). Awamu ya pili ya utafiti huu inaendelea...

NB: sitaanika members niliokutana nao wala "derived instruments & indicators" for privacy.
 
Kama ambavyo mimi ni mtoto, sio?

Uko sahihi kabisa, soon ntamaliza darasa la saba B shule ya msingi Mtakuja.

Asante Anko Magu kutuletea laputopu sisi wanaKayumba. Mnaosoma St. Mtakatifu academy Mungu anawaona, tutakutana kwenye bodi ya mikopo.
 
Kama ambavyo mimi ni mtoto, sio?

Uko sahihi kabisa, soon ntamaliza darasa la saba B shule ya msingi Mtakuja.

Asante Anko Magu kutuletea laputopu sisi wanaKayumba. Mnaosoma St. Mtakatifu academy Mungu anawaona, tutakutana kwenye bodi ya mikopo.
Heri ya mwaka mpya.
Wasalimie wajukuu wako wote
 
Sio kweli, mtu anaweza kuweka picha isiyo na uhalisia wala uhusiano wowote na yeye.

Labda #bigbootylover# na [HASHTAG]#Rohombaya#[/HASHTAG]
 
Nakubaliana na utafiti wako kwa 75%
Na nyongeza ID anayotumia mtu inaendana kwa kiasi kikubwa na maisha yake halisi au vile alivyo.
Nadhani hili suala la ID na Avatar lipo kisaikolojia zaidi.
 
Kama ambavyo mimi ni mtoto, sio?

Uko sahihi kabisa, soon ntamaliza darasa la saba B shule ya msingi Mtakuja.

Asante Anko Magu kutuletea laputopu sisi wanaKayumba. Mnaosoma St. Mtakatifu academy Mungu anawaona, tutakutana kwenye bodi ya mikopo.
Babu Asprin umenichekesha sana lakini pia ulipotaja Mtakuja akili yangu ikaenda mbio kwa ile familia ya kufikirika ya Mr. and Mrs. Daud. Kwa hakika ile familia ilinihamasisha sana kusoma ikiwa pamoja na kuipenda lugha ya malkia. Japo sikuijua.

Babu Asprin, mi ni wa wakati wa 'original' "ninaye ndege mzuri mrembo wa kupendeza" (naskia siku hizi kuna remix kama kweli) "wengine mnawakanyaga", " heri mimi sijasema" tetemeko la ardhi, mkisi mmoja kavuka ziwa nyasa, heka heka mtoni. Enzi ambayo wanafunzi tulikuwa tukipenda elimu japo elimu haikutupenda (shule zilikuwa chache hivyo kufaulu sjui kuchaguliwa ilikuwa kimbembe). Tofauti na sasa hivi, elimu inawapenda wanafunzi lakini wenyewe hawaopendi elimu. Si zamani sana lakini kiasi kuitwa babu now.

Huu utafiti pamoja na mapungufu yake kadhaa, lakini naweza kusimama na kuutetea na hata kuthibitishwa na members.
 
We bhana wewe... mimi sizitaki mbichi hizi. Hebu tumbo niache nimbakizie Manenge...

Sisi wa Kayumba praimare tuliowasoma zaidi kina Juma na Roza, ndio maana unaona tulivyo mahiri kuongea kinyerere kuliko kikristu.
 
Sasa kwa mfano hii yangu inanielezeaje mimi?

Kwamba mimi ni katoto kahendsamu na katanashati au...?

Hizi tafiti za JF bana...huwa zinachekesha sana wakati mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…