britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,295
- 33,994
Nashangaa tunajiulize kwanini hasa Tanzania rushwa haikomi
Utafit mdogo niliofanya ni huu
1. POLISI TANZANIA
Hapa wanaongoza kwa kutengeneza mazingira ya Rushwa. Ukiwa na kesi inayohusisha madai au Jinai lazima wale pande zote mbili,
Pia kuna hawa askari wa Usalama Barabarani, nao kila ukipita imefika hatua mpaka wanakulazimisha kutoa hela, wengine wanasema "TOA rushwa uondoke, au Usipotengeneza mazingira utakamatwa kila siku, Zoeleka kwa Askari" saa nyingine gari lako halina kosa lolote,
2. Hospitali za Serikali,
Hapa Rushwa inatembea sana, wanaohudumu ndani Kutokana na mlolongo uliopo nimeshuhudia Rushwa kwa aina zifuatazo
A. Wanaoenda kuwaangalia wagonjwa, wanabaniwa mpaka atoe chochote, mbaya zaidi ukienda kumpelekea chochote muda wa kuangalia wagonjwa umepita, nimeona na kushuhudia pengine wakitoa sh 10,000 saa nyingine 5,000.
B. Wanaokuwa masijala wakikupokea hujafuata utaratibu 10,000 inakutoka
C. Ukitoka nyumbani bila kupita popote kupata referral napo unatozwa 20,000.
3. TRA hawa bado wanakula Rushwa sana, kwenye Bidhaa na ukadiriaji,
4. Wakala Leseni za Biashara manispaa,
Hawa wanahongwa kurejesha tarehe za leseni nyuma, 300,000 yaani back dating kwa watu wanaotaka Mikopo lakini wanakata leseni mpya,
5. Askari wa Maliasili na Misitu
Ukikamatwa maeneo ya Karagwe ni matatizo