Utafiti: Watu weusi wanachukiwa zaidi Marekani wanaongoza kuuawa na polisi, hizi sababu tatu

Utafiti: Watu weusi wanachukiwa zaidi Marekani wanaongoza kuuawa na polisi, hizi sababu tatu

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Nimefanya utafiti wa takwimu za rangi na matabaka ya kijamii na ambavyo wanaathirika na mfumo wa utoaji haki na kuzuia uhalifu nchini Marekani
importedImage402513_header.jpeg

1. Wamarekani Weusi wako hatarini zaidi kuuawa na polisi
Takwimu ambazo zipo wazi kwa matukio ambayo polisi wameua raia kwa risasi zinaonesha kuwa kwa Wamarekani Weusi kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kupigwa risasi na kuuawa ukilinganisha na idadi yao kwa ujumla nchini humo.

Fatal shootings chart

Kwa mujibu wa kanzidata ya gazeti la Washington Post jus ya matukio ya polisi kupiga watu risasi, japo Wamarekani wenye asili ya Africa ni chini ya asilimia 14 ya raia wote wa Marekani, lakini wao ni wahanga kwa asilimia 24 ya matukio 6,000 ya polisi kuuwa watu kwa risasi toka mwaka 2015.

Idadi ya vifo vinavyotokana na kupigwa risasi na polisi nchini Marekani imeendelea kusalia kuwa takriban watu 1,000 kwa mwaka toka 2015.

Takwimu pia zinaonesha kuwa uwiano wa polisi kuwashambulia kwa risasi watu weusi ambao hawajajihami kwa silaha ni mkubwa mara tatu zaidi ya wazungu.

2. Uwezekano wa kusimamishwa barararani ni mkubwa zaidi
Tafiti zinaonesha kuwa watu weusi wapo kwenye uwezekano mkubwa zaidi wa kusimamishwa na askari wa barabarani nchini humo.
Protestor holding a placard with picture of George Floyd

Utafiti wa hivi karibuni zaidi ni wa mwaka 2020 uliofanywa na Chuo Kikuu cha Stanford na kupitia matukio milioni 100 ya watu kusimamishwa barabarani kote nchini Marekani. Matokeo yake yakawa ni madereva weusi wapo kwenye uwezekano wa kusimamishwa kwa zaidi ya asilimia 20 ukilinganisha na wazungu.

Na hata baada ya kusimamishwa, utafiti huo umebainisha kuwa madereva weusi walipekuliwa mara mbili zaidi ya madereva wazungu, japo madereva weusi kitakwimu uwezekano wa kuwa wamejihami kwa silaha haramu ni mdogo zaidi.

3. Wamarekani weusi wanakamatwa zaidi kwa matumizi ya mihadarati

Wamarekani wenye asili ya Afrika wanakamatwa zaidi kwa matumizi ya mihadarati kuliko wazungu japo tafiti zinaonesha kuwa matumizi ya mihadarati inawiana kwa jamii hizo mbili.

Mwaka 2018, takriban watu 750 kati ya kila wamarekani weusi 100,000 walikamatwa kea matumizi ya mihadarati, ukilinganisha na yatu 300 kati ya wazungu 100,000.

Black man under arrest with hands on head

Tafiti za nyuma za matumizi ya mihadarati nchini humo zinabainisha kuwa wazungu hutumia mihadarati kwa kiwango sawa na weusi, japo watu weusi hukamatwa zaidi.

Mathalan utafiti uliofanywa na taasisi ya American Civil Liberties Union uligundua kuwa wamarekani weusi wanaweza kukamatwa kwa kuwa na bangi mara 3.7 zaidi ya wazungu japo matumizi ya bangi baina ya jamii hizo mbili yanawiana.

Credit: Bongo five
 
Mimi tangu niskie yule malkia wa uingereza naye kabaguliwa hapo ilinikata stimu kabisa

Nikashindwa kuwaelewa wazungu wanataka nini, maana mwanzo nimekua nikijua ubaguzi wa rangi unaofanywa na wazungu ni ule wa kuwanyanyapaa wale walio weusi.

Lakini yule mrembo ni mweupe tena ana ng'aa kabisa awali nilijua ni mzungu pia mpaka pale niliposikia naye katengwa mpaka akataka kujiua

Hofu ipo kwa sisi ambao tukiwa huku kwetu africa tunaitwa weusi na waafrika wenzetu je kwa mzungu atatuonaje?
 
Yule kisa kua na mzazi mmoja mweusi tu nae anatengwa.......huku wamatumbi wenzetu wanatuita weusi wakati na wao hawana hata chembe ya hao weupe
 
Mimi tangu niskie yule malkia wa uingereza naye kabaguliwa hapo ilinikata stimu kabisa

Nikashindwa kuwaelewa wazungu wanataka nini, maana mwanzo nimekua nikijua ubaguzi wa rangi unaofanywa na wazungu ni ule wa kuwanyanyapaa wale walio weusi.

Lakini yule mrembo ni mweupe tena ana ng'aa kabisa awali nilijua ni mzungu pia mpaka pale niliposikia naye katengwa mpaka akataka kujiua

Hofu ipo kwa sisi ambao tukiwa huku kwetu africa tunaitwa weusi na waafrika wenzetu je kwa mzungu atatuonaje?
Dhambi ya ubaguzi ina watafuna hasa na itawatafuna mpaka wakome tena na hii COVID ndo kabisaa sababu hata chanjo zimewakataa, na majira baridi ndo hayooo yanaisha !! na vimelea vya covid vinapenda joto! subiri watazikimbia mahiti hao na hawatasahau
 
Mimi tangu niskie yule malkia wa uingereza naye kabaguliwa hapo ilinikata stimu kabisa

Nikashindwa kuwaelewa wazungu wanataka nini, maana mwanzo nimekua nikijua ubaguzi wa rangi unaofanywa na wazungu ni ule wa kuwanyanyapaa wale walio weusi.

Lakini yule mrembo ni mweupe tena ana ng'aa kabisa awali nilijua ni mzungu pia mpaka pale niliposikia naye katengwa mpaka akataka kujiua

Hofu ipo kwa sisi ambao tukiwa huku kwetu africa tunaitwa weusi na waafrika wenzetu je kwa mzungu atatuonaje?

Waingereza ndiyo washenzi zaidi, maana wana msemo wao "mbwa akizaliwa (pappy) kwenye banda la farasi hawi farasi". Kwa hiyo kale katoto hakawezi kuwa farasi.
 
Back
Top Bottom