Utafutaji maisha ndio chanzo kupoteza mahusiano, marafiki, ndugu na wapenzi

Utafutaji maisha ndio chanzo kupoteza mahusiano, marafiki, ndugu na wapenzi

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Harakati za kutafuta huku na huku zinatufanya kupoteza watu wengi kwenye maisha yetu usitegeme usafiri mbali kutafuta maisha alafu mpenzi wako utadumu naye.

Maisha ya utafutaji ni kipingamizi tosha cha kupishana muelekeo, mtazamo na n.k.

Hivi konde boy anaweza kumrudia demu wake wa Mtwara au Dar hapo kabla hajawa msanii
 
Mkigandana sana mwisho wa siku ukawa huna kitu hao hao uliojisemea ngoja niwepo hapa kwa ajili yao still watakuona huna maana na kwenda kwa wengine ambao nao walitoka kwao wakawaacha waliowahitaji.

Muhimu sana kwenye haya maisha penda kutengeneza watu wapya na usiwe mwepesi wa kudharau watu,mwenye elimu asiyekuwa na elimu mwenye mali asiyekuwa na mali hao wote upo wakati utawahitaji so tuishi na watu kwa nidhamu.
 
Ndivyo maisha yalivyo hivyo, muda unapozidi kwenda lazima utapoteana na watu unaowafahamu mfano Kila level ya elimu utakayopita utakuwa na marafiki lakini Kila utakavyopanda juu ndivyo ukaribu unazidi kupungua mwisho watu wako wa karibu watakuwa ni familia yako tu, hii maana yake ni Nini Sasa?, maana yake ni kwamba una wajibika Kwa Kila hatua ya maisha yako, usitegemee mtu kwenye kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom