Utafutaji wa picha za mwanzo za Baba wa Taifa kwa ajili ya kuhifadhiwa katika nyumba ya kumbukizi yake Magomeni

Utafutaji wa picha za mwanzo za Baba wa Taifa kwa ajili ya kuhifadhiwa katika nyumba ya kumbukizi yake Magomeni

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUMBUKIZI YA NYUMBA YA MWALIMU NYERERE NA PICHA ZA MWANZO WA NYAKATI ZAKE

1569984970380.png

Tukichagua picha za Mwalimu Nyerere

Watafiti wa Kumbukizi ya Nyumba ya Mwalimu Nyerere leo L' Asr walinitembelea tena kwa nia ya kupata picha adimu za Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kuzionyesha katika nyumba aliyoishi Magomeni ambayo sasa ni sehemu ya kumbukumbu yake.

Tumekaa sote na tumesaidiana kuchagua picha moja baada ya jingine zaidi tukiongozwa na ''caption,'' za picha hizi.

Nyingi ya picha hizi nimeshazionyesha katika mitandao ya jamii lakini kwa maofisa hawa baadhi ni picha ngeni kwao.

Madhumuni yao ni kuweza kukusanya kila picha ya Mwalimu Nyerere na za washirika wake ili kukamilisha historia yake mwenyewe Baba wa Taifa katika picha ili kuonyesha uasilia wa hali ilivyokuwa katika miaka ya 1950 nyakati Baba wa Taifa alipofika Dar es Salaam na kupokewa na wenyeji wa mji na kuanza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Picha ni nyingi na sina hakika kama tumeweza kuzipata zote lakini nimefarajika wataalamu hawa waliponiambia kuwa hii ni kazi endelevu na tutakuwa tunaifanya siku zote na wakati wote.

Naweka baadhi ya picha ambazo mimi hii leo nimewakung'utia watafiti hawa ili zikapambe nyumba ya Mwalimu zikiwa kama kumbukumbu yake na wale aliokuwanao katika kuikomboa Tanganyika kutoka makucha na minyororo ya ukoloni.

Baadhi ya picha ambazo zimepatikana kwa ajili ya kumbukizi ya Baba wa Taifa ni hizo hapo chini na hizi hapo chini na kila picha inaeleza maisha ya Mwalimu Nyerere na chama cha TANU.

Baadhi ya historia za wazalendo hawa katika kupigania uhuru wa Tanganyika zinaweza kusomwa hapo chini katika hizo link:

  1. https://mohamedsaidsalum.blogspot.com/2013/12/bibi-titi-mohamed-1926-2000-shujaa-wa.html
1. Sheikh Hassan bin Ameir 2. Salum Mpunga (Lindi) 3. Yusuf Chembera (Lindi) 4.Yusuf Olotu (Moshi) 5 Iddi Tosiri 6. Sharifa bint Mzee (Lindi) 7.Mwalimu Kihere (Tanga) 8. Abdul Sykes, Nyerere, Dossa Aziz na Lawi Sijaona 9.Abdallah Rashid Sembe (Tanga) 10. Makatta Mwinyi Mtwana na Sadiq Patwa (Tanga) 11. Bi. Titi Mohamed na wazee wa Dar es Salaam 12. Shariff Abdallah Attas 13. Bi. Mruguru bint Mussa (Mama Abdul) 14. Sheikh Hussein na Hassan Juma 15. Robert Makange 16. Paul Bomani (Mwanza) 16. Ali Migeyo (Bukoba) 17. Maulidi Kivuruga (Tabora) 18. Chief Kidaha Makwaia (Shinyanga) 19. Mwami Theresa Ntare (Kasulu) 20. Amir Jamal na Nyerere 21. Haidar Mwinyimvua...
 
Jamaaa ana hila tu huyu hana picha hata moja ya baba Wa Taifa Mwa.Nyerere anawapigia kampen jamaa zake ,acha hila we babu
 
Jamaaa ana hila tu huyu hana picha hata moja ya baba Wa Taifa Mwa.Nyerere anawapigia kampen jamaa zake ,acha hila we babu
Gitarijosenga,
Kwa makusudi nimeweka picha za wazalendo ambao wengi hawajui michango yao.

Picha as Mwalimu ninazo nyingi sana.

Naona unaumia sana kusoma historia hii ambayo hakupata kuijua.

Wala haupo peke yako.
Wengi sana wamechomwa na historia hii.
 
Back
Top Bottom