Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Polisi wataweza kuingia nyumbani ama afisini mwako kuweka vifaa vya kunasa mawasiliano yako
Mahakama itakubali ushahidi unaopatikana kwa njia hiyo
Polisi huenda wakapata idhini ya kusikiliza mawasiliano yako kwenye simu ya mkononi iwapo watakushuku kwa kujihusiaha na biashara ya dawa za kulevya endapo sheria inayopendekezwa itapitishwa .
Mswada huo unaopendekezwa na mbunge wa Kiambaa Paul Koinange utawaruhusu polisi kuingia nyumbani ama afisini mwako na kuweka vifaa vya kuweza kusikiliza mawasiliano yako ya simu .
Na kwa minajili ya kutafuta ushahidi korti inaweza kumruhusu afisa wa polisi mwenye chao juu ya Chief inspekta kuifanya oparesheni kama hiyo .
Polisi hata hivyo watajitajika kupata idhini ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kabla ya kwenda kortini .
“ Korti itatoa agizo linalohitaji kampuni ya mawasiliano kunasa mawasiliano ynayaofanywa au yanayokaribia kutekelezwa’ sehemu ya mswada huo inasema
Koinange ndiye mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu usalama . Korti pia itawaruhusu polisi kuchukua simu yako ya mkononi na vifaa vingine vinavyotumiwa kufanikisha biashara ya dawa za kulevya .
Mahakama hata hivyo zitaridhishwa kwanza kwamba mawasiliano yanayonaswa yanaweza kusababisha kutekelezwa kwa uhalifu chini ya sheria hiyo ya kupambana na mihadarati .
RadioJambo