Utajiri na Mafanikio

Jpinduzi

Senior Member
Joined
Feb 26, 2011
Posts
136
Reaction score
68
Ikiwa unapambana na hali mbaya ya kiuchumi na kifedha, jua kwamba, hayo si mapenzi ya Mungu; bali Mungu anataka uwe na mafanikio katika mambo yote. Unapotaka kupambana na hali yoyote inayozuia mafanikio yako ya kifedha na kiuchumi, pamoja na kufanya kazi kwa bidii na maarifa, lakini pia ingia katika maombi huku ukisimamia neno la Mungu katika mistari ifuatayo.

3Yohana 1:2
Mpenzi ninaomba ufanikiwa katika mambo yako yote na kuwa na afya yako, kama roho yako ifanikiwavyo

2Timotheo 2:7
Na Mungu atakupa akili katika mambo yote.

Kumbukumbu 28:1-13
Bwana ataibarikia kazi yote ya mikono yako …

Zaburi 1:1-3
Heri mtu yule asiyeenenda katika shauri la wasio haki … bai sheria ya Bwana ndiyo inayompendeza, atafananishwa na mti uliopandwa kando ya kijito cha maji … na kila jambo alifanyalo, litafanikiwa

Yoshua 1:7-8
Uwe hodari na moyo wa ushujaa , uangalie kutenda sawa sawa na sheria yote … ndipo utakapofanikiwa sana kila uendako … na ndipo utakapostawi sana

2Wakorintho 8:9
Yesu Kristo, alikuwa masikini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajri. Ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

2Wakorintho 9:11
Mkitajirishwa katika vitu vyote, mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu


Wafilipi 4:19
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Kumbukumbu 15:4
Na kati yenu, hawatakuwepo masikini kwenu, kwakuwa Bwana atakubariki kweli, katika nchi akupayo Bwana Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako

Isaya 45:1-3
Asema Bwana wa Majeshi, Nitakwenda mbele yako na kupasawazisha mahali palipoinuka, na kuvunja vunja milango ya chuma na mapingo ya shaba, nami nitakutolea hazina za gizani, zilizofichwa ziku nyingi

Malaki 3:10 – 12
Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi

Warumi 10:12
Yeye ni Bwana wa wote, wenye utajiri kwa wote wamwitao
 
mkuu umenitundikia drip ya kutosha na subili uniruhu kutoka wodini maana nahisi nimepona
 
Sawa mkuu!Nakusubiri utoke wodin ili uwajibike!
 
Asante sana kwa dozi zako,karibu katika kuandikia katika blog yetu,ni pm mkuu ulete material tuweke kwenye blog
gonga hapa
GSHAYO
 
umefungua kanisa la kuombea watu mafanikio! hongera. liko wapi? nawe unajiita nani vile? mzee wa mafanikio????? umechagua biashara nzuri sana, inalipa.
 
umefungua kanisa la kuombea watu mafanikio! hongera. liko wapi? nawe unajiita nani vile? mzee wa mafanikio????? umechagua biashara nzuri sana, inalipa.

Sijafungua kanisa wala sio mchungaji,ila inawezekana mtu/watu wanahangaika pasipokujua nini wafanye,kama tunavyoelewa kuwa maisha ya mwanadamu yanamtegemea Mungu kufanikisha kila jambo. Kwanza ni vizuri ukafahamu kwamba, ikiwa Mungu ana mawazo ya amani juu yako(Yeremia 29:11), basi, Shetani pia ana mawazo ya uharibifu juu yako. Na hii ina maana kila siku mwanadamu atakutana na vita ya nini atekeleze katika ufahamu wake, naam hii ndiyo vita ya mawazo. Mungu atapigana kuhakikisha mawazo yake juu yako yanafanikiwa na Shetani naye atapigana kuhakikisha mawazo yake kupitia wewe yanafanikiwa.Mistari niliyoiweka ni kumpa mwongozo msomaji nini afanye anapokabiliwa na vita ya mawazo(nini afanye) inayompa utajiri na mafanikio.
 
Sasa huoni kama ungefungua kanisa ndio ungewasaidia watu vizuri na kwa ukaribu zaidi???? fungua bwana, hakuna atakayekushangaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…