Hiii thread muhimuDHAMANA ZA MUDA MREFU (TREASURY BOND)
Sehemu ya kwanza tulijadili kuhusu dhamana za muda mfupi (treasury bills) na tukaona ni jinsi gani zinaweza kumuingizia mtu kipato.
Leo tutajadili kuhusu dhamana za muda mrefu (treasury bonds) kwa mazingira ya nchi ya hapa Tanzania na namna gani zinavochangia katika kutengeneza kipato.
Dhamana za muda mrefu (Treasury bonds) ni nini?Treasury bond ni hati ya madeni. Nikiwa na maana ya kwamba hati hiyo inaonesha mkopaji (borrower) ambaye ndiye ametoa dhamana hiyo na mkopeshaji (lender) ambaye anakuwa ndiye aliyenunua bond na huyu ndiye tunamuita mwekezaji.
Wakati serikali au mashirika makubwa yanapohitaji kupata pesa kwa ajili ya kujiendesha, wanakopa pesa kutoka kwa wawekezaji na wakishazipokea pesa hizo ndipo wanatoa hati ya dhamana ya madeni (bond) kwa wawekezaji kuonesha kwamba pesa walizozipokea ni madeni.
Hati hizo za madeni zinaonesha mda usiobadilika (fixed period of time) ambao deni hilo litalipwa na huwa zina ukomo wa zaidi ya mwaka mmoja. Kwa Tanzania kuna Treasury bond za miaka 2, 5, 7, 10 na 15.
Hati hizo za madeni (bonds) zinazotolewa na wakopaji zinakuwa na
- Ahadi ya kiwango cha malipo ya riba kwa kipindi fulani. Koponi ya hati yako yaweza kusema "kutakuwa na riba ya 10% ambayo italipwa kila mwaka mpaka ukomo wa deni utapofika") malipo ya riba yaweza kuwa mara moja, mbili, tatu na nne kwa mwaka kutegemeana na koponi ya hati inavosema.
- Ahadi ya kurudishiwa kianzio ulichowekeza wakati deni linapofika ukomo. Hii inamaana kama ulitoa milioni 100 kwa mfano kununua bond, ikishafika ukomo utarudishiwa ile milioni 100 yako ambayo uliitoa.
Faida za kuwekeza katika bondsUwekezaji katika treasury bonds una faida zifuatazo
- Umiliki wake unahamishika, ikiwa na maana unaweza kurithisha familia yako ama pia kuziuza pale inapotekea ukawa na ukitaji wa pesa.
- Zaweza kutumika kama dhamana za kuombea mikopo katika taasisi za fedha zinazotoa mikopo.
- Gawio la riba katika bond ni kubwa na lenye kuaminika zaidi kuliko riba zinazopatikana kwenye taasisi za fedha kama mabenki.
- Hazina hatari yoyote kubwa (risk free) kwa mwekezaji na ni uwekezaji wa uhakika kwa sababu zinatolewa na serikali. Ieleweke kwamba kwa Tanzania treasury bond zinatolewa na serikali ya Tanzania kupitia kwa banki kuu ya Tanzania lakini kwa nchi nyingine zilizoendelea sana kama America mashirika makubwa pia yanatoa bonds kwa wawekezaji.
Soko la treasury bonds kwa TanzaniaHapa hakuna tofauti na soko nililoeleza katika dhamana za muda mfupi (treasury bills).
- Soko la awali (primary market) hapa ni pale banki kuu ya Tanzania inapotoa kwa mara ya kwanza treasury bond kwa wawekezaji kwa niaba ya serikali.
- Soko la pili (secondary market) hii inahusisha kuuza na kununua treasury bills na hii inafanyika Dar es salaam stock exchange DSE. Hapa ndipo pale mtu anapotaka kuuza treasury bond anayoimiliki anaweza kwenda kuuza.
Kianzio cha kuwa mwekezaji wa moja kwa moja kwenye treasury bonds kwa Tanzania ni sh. 5,000,000. Ina maana kwamba ukiwa na mtaji wa kuanzia milioni tano basi unaruhusiwa moja kwa moja kushiriki kwenye mnada wa treasury bonds (treasury bonds auction).
Kwa wawekezaji wa mtaji chini ya milioni tano basi wao watashiriki kwenye mnada kupitia primary dealers ambao kwa urahisi ni mabrokers na commercial banks zilizoainishwa na banki kuu ya Tanzania.
Primary dealers ambao wamethibitishwa na BOT ni hawa wafuatao (ambao wale wenye mitaji chini ya milioni tano watapitia kwao) Akiba Commercial Bank Ltd, Citibank (T) Ltd, CRDB Bank Ltd, Diamond Trust Bank (T) Ltd, Eurafrican Bank (T) Ltd.Exim Bank (T) Ltd. Habib African Bank Ltd. International Commercial Bank (T) Ltd. Kenya Commercial Bank (T) Ltd, NBC Limited, NMB Ltd, Stanbic Bank (T) Limited, Standard Chartered Bank Ltd, Orbit Securities Co. Ltd, Rasilimali Limited, Solomoni Securities Ltd, Core securities Ltd, Tanzania securities Ltd, Vertex International Securities.
Unapata vipi pesa na faida kupitia dhamana za muda mrefu?Mfano huu nimeuchukua kwenye zabuni iliyofanywa tarehe 22-Jul-2015 na banki kuu ya Tanzania.
Taarifa muhimu katika majibu ya mnada huo ni ifuatavyo.
Rate ya coupon: 9.18%
Coupon payment frequency &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; semi annual : 23-Jul and 21-Jan
Ukomo (maturity date) 23-Jul-2020
Face value ya coupon moja TZS 100,000
Bond zilitolewa kwa discount ya TZS 75.8133/100 kwa maana coupon moja yenye face value ya TZS 100,000 iliuzwa kwa TZS 75,813.3
mfano sasa:
Kama ulinunua koponi 1000 zenye face value ya TZS 100,000 ambazo umezipata kwa diskaunti hiyo ya 75,813.3 kwa kila coupon. ina maana utakuwa na uwekezaji wa 1000*TZS 100,000= TZS 100,000,000
Lakini kumbuka umepata discount kwa hiyo ulichokitoa mfukoni ni 1000*TZS 75,813.3= TZS 75,813,300
Hivo unaweza kuona umetoa TZS 75,813,300 ukapata mali yenye thamani ya = TZS 100,000,000
Kwa mahesabu ya haraka kuna faida kama ya TZS 24,186,700 ambayo itakuwa imejificha kwenye uwekezaji wako. (kwa hiyo elewa mpaka sasa umeshatengeneza kama 24 million)
Pato la ribaKwa kutumia taarifa za kwenye mfano wetu unaweza kuona ni kiasi gani utakuwa unapata kama pato la riba kwa kipindi chote cha uwekezaji. Ambacho ni kipindi cha miaka mitano utokanao na uwekezaji wako.
Rate 9.18%
Semi annual-2
Face value TZS 100,000
Idadi ya koponi ulizowekeza 1000
Formula ya kukokotoa pato la riba
Riba= (idadi ya koponi×face value)×(rate/2)
=(1000×100000)×(0.098/2)
= 4,590,000 (hiki utakuwa unalipwa mara mbili kila mwaka kwa miaka mitano ambao mkataba wako ndio utafika kikomo)
Kiasi hiki utakipokea mara mbili kwa mwaka mpaka mkataba wako utapoisha 23-Jul-2020
Kwa hiyo pato la riba ndani ya miaka 5 litakuwa (5×2×4,590,000)=TZS 45,900,000
Mwaka wa tano ambao ndio maturity date utarudishiwa na kianzio ulichowekeza (principal) ambacho ni (1000*100,000)= TZS 100,000,000 na sio ile milioni 75 kwa sababu kumbuka ulipewa diskaunti na uwekezaji wako ulihesabika ni TZS 100,000,000
Jumla ya mapato yote ya uwekezaji= pato la riba + principal
=45,900,000 + 100,000,000
=145,900,000
Kiasi halisi ulichotoa mfukoni =75,813,300
FAIDA KUU YA UWEKEZAJI = 145,900,000 -75,813,300 = TZS 70,086,700
Kwahiyo kwa miaka mitano umepata faida jumla ya TZS 70,086,700
Faida hiyo ni sawa na kusema
.TZS 14,000,000 kwa mwaka
.TZS 1,166,666 kwa mwezi
. 92.5% ROA
Uwekezaji huu wa bonds ni murua sana kwa wazee wetu ambao ama wamepokea pension zao na wanakosa maarifa ya namna ya kuziwekeza. Watu pia wenye pesa zao nyingi hii pia ni fursa.
Kama kuna mtu atahitaji kueleweshwa zaidi anaweza akaacha comment halafu ntamjibu endapo kuna sehemu sijaeleweka.
Chapisho lijalo nitajaribu kuzungumzia fursa zilizopo kwenye hisa na biashara ya fedha za kigeni na pia timing ya kuuza na kununua. Pia ntafikiria kuwa na mada maalumu juu ya riba katika taasisi zetu za kifedha hapa nchini na ni rafiki kiasi gani kwa ujasiriamali mdogo mdogo. Ningependa pia kupata uzoefu wenu katika hili.
Asanteni.
Asante kwa somo zuriDHAMANA ZA MUDA MREFU (TREASURY BOND)

Coupon payment frequency – semi annual : 23-Jul and 21-Jan