Utajiri wa rafiki yangu ulivyofanya nikamuamini Shetani

Zote nilizoma za kina Monica kule Tabora, na ile ya fedha bandia/mitutu ya bunduki.
Anajua kusimulia huchoki kusoma. Mimi simulizi zake zote, nikisoma nakuwa kama naangalia movie, nishawapa sura na maeneo yote anayotaja kama nayaona.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Daaah yaani historia YAKO inatosha kabisa kutengeneza series ambayo haichoshi. Hongera kaka una talent kubwa sana kuachilia mbali historia inayofundisha na inayosisimua. Lini unaendelea mkuu?
 
Way back nikiwa mdogo nilikuwa naishi na jirani yangu mpemba, alikuwa na mke na watoto pamoja na ndugu wengine wengi tu, nyumba yake ilikuwa na vyumba vinavyoangaliana mfano wa vyumba vya bweni ya shule, alikuwa ni mfanya biashara wa duka pia na hiace.
Alikuwa na watoto kadhaa mmoja wapo alikuwa kama taahira mda mwingi alikuwa anazubaa zubaa tu, basi kila mwanzo wa mwezi siku ya ijumaa alikuwa anachinja kuku kwenye kibaraza cha kuingilia ndani halafu anapika wali na ile nyama ya kuku na kuwaita watoto kula ila yeye na familia yake walikuwa hawali.
Nyumbani walinipiga marufuku kula kile chakula ingawa nilikuwa natamani sana kula lakini watoto wengine walikuwa wanakula na kufurahia, mpaka kuna wakati wakawa wanataimu siku yule mzee akichinja kuku na huku home wanapika wali maharage ili nisitamani kile chakula na kweli sikuwahi kula.
Ikapita miaka kadhaa, siku moja asubuhi nikasikia shehe khalifa amefariki nikashangaa kwani siku moja jioni kabla ya kifo chake alipita nyumbani wala sikuona kama ana dalili ya kuumwa, ila baadae maneno yakaanza kuzagaa kwamba jini/ majini yake yalianza kudai kafara la damu ya mtu hivyo ilibidi atoe kafara la damu la mtoto wake akachelewa kutii maagizo ndipo akafa yeye.
Sasa nilipokuwa mkubwa ndipo nikajua kwanini alikuwa anachinja kuku mlangoni kila mwezi.
 
Unajifariji tu. Sio wote . Usitake kupata uhalali wa wewe wa kutoitafuta range mkuu. Komaa mpaka kieleweke,. Mie Sina hizo Imani. Ingekuwa ivyo AFRICANS tungekuwa matajiri kuliko wazungu
Alokwambia wazungu hawana ulozi ni nani??
Ni kwamba tu jamaa wameendelea ila ila ulozi wanao sana tu na wachawi wapo kama huku, sema huku tatizo umasikini.

Kwa maana hiyo masharti ya huku na huko ni tofauti, na huku tunadakwa sana na nguvu za giza kwasababu ya umaskini wetu na kutojitambua.
Ila wenzetu wanamuasi Mungu kwa mambo tofauti na ulozi ukiwemo.
 
Ungekula.tu wala haina madhara. Chakula cha dua kafara wahusika hawali ila wengine wanakula tu.mnaogopaga hadi naz we ukizikuta beba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…