Hapo kwenye nyekundu umepotoka Chupaku....unaposema madaktari wengi hawana maadili kwa kigezo gani? Una statistics zozote? Au kwa sababu hospitalini kukitendeka mazuri 1000 hayataandikwa ila likitokea baya 1 inakuwa breaking news basi nawe unahukumu wahudumu wa afya kwa kufuata mkumbo tuu! Sio vizuri bana..
Ultrasound haiwezi kuwa mbadala wa physical examination...gynaecologist anapompima mwanamke si vidole tuu, vidole ni final..na sometimes kuotkana na tatizo lenyewe vidole vinaweza visitumike kabisaa. Lakini hata hivyo...hata huko ambako ultrasound machines zipo mpaka corridoni bado PV examination ni essential pale inapokuwa indicated.
Mwanamke anapofanyiwa PV examination kwanza anaombwa na anaridhia, kama hataki hakuna atakayemlazimisha. Pili kama amefuatana na mwenza wake (mumewe, mchumba), huyo mwenza ana haki ya kuwepo wakati mwanamke huyo anachunguzwa, na kama hayuko na mwenza wake..basi mwanamke huyo ana haki ya kuomba nesi awepo wakati anachunguzwa. Madaktari makini wengi huwa wanaita nurse aje awepo wakati wa kuwafanyia wanawake uchunguzi. Tatizo unakuta hospitali manesi habaa, utampata wapi huyo wa kuja kusimamia zoezi hilo wakati huyo huyo anahitajika wodini, clinic, etc?!
Usiwe na haraka ya kujudge kabla hujaangalia mfumo wenyewe ukoje...critically!