Utajuaje Brake Pads za gari yako zimeisha?

Samatime Magari

Senior Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
119
Reaction score
457

Kuna madereva huwa wao wakishaweka D ndo nitolee mwendo mdundo, unakuta Brake pads zinaisha hajui zinakula disc mpaka inakua nyembamba utafikiri CD.
.
Sasa Basi nimekuandalia Tips rahisi kwa ufupi kabisa zitakazokusaidia kujua Brake Pads zimeisha na utazijua ndani ya sekunde 60 tu, Kwanza Taa ya brake kwenye dashboard itawaka...
.

.
Hii itatokana na Low level ya brake fluid, pindi unapoona hiyo taa imewaka chunguza gari lako kwenye kile ki container cha brake fluid sasa ukiikuta level ya mafuta iko chini usiongeze...
.
Sababu ya kupungua mafuta ni yameenda kwenye brake pistons kucover kiasi cha brake pads kilicholika, ukiforce kuongeza kutaifanya gari ishindwe kupata taarifa sahihi pindi brake pads zitakapoisha tena...
.
Pia ukiweka Pads mpya kama uliongeza mafuta yatamwagika na utaikosa ile level stahiki, Pili Pads zikiisha Zitatoa kamlio flani hivi kama mluzi ukishika brake [wadau wa madafu huwa hawaupendi]...
.
Jinsi walivyozitengeneza hizi Pad [sio zote] zikiisha zikafika chini kabisa kuna kibati kitaanza kusugua ile disk ambapo brake pads zinabana, zikisugua tu zitakupa kelele za kutosha.
.

.
Kwa gari zenye brake shoe nyuma Hand brake itakua haishiki kabisa. Yani ukikanyaga hand brake then ukatia D mzigo unaondoka..
.

.
Tatu Ukikanyaga brake zinaenda chini sana sasa hapa ni kwamba Pads zikiisha zinasababisha mafuta kwenda kwenye cylinder za brake na hii inasababisha brake kuwa chini...
.
Ukiona brake unakanyaga mpaka inafika chini kabisa ndo inashika jua kwamba brake pad zimeisha na ni muda muafaka wa kubadilisha, Naamini/kama una indicator za ziada naomba u share hapa kwa faida ya wengine..
.
Asante
Samatime
0714547598
 
Wajerumani, wanaangalia tu hii taa wanabadili brake pads.

Oooops nimeshindwa kuupload.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…