Utajuaje kama utafiti au research unayotaka kuifanya ni Qualitative au Quantitative au Mixed?

Festo Andrews

Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
23
Reaction score
25
Kama wewe ni mwanafunzi au mtu unayetaka kujifunza kuandaa research na kuzioffer kwenye majukwaa ya freelancing kama upwork, Fiverr na Linkedin lakini huelewi baadhi ya concepts zinazotumika huko gather here.

Kabla hujaanza kufanya research yako, ni muhimu kufahamu kuwa kuna aina mbalimbali za research ambazo huwa zinafanywa na watu mfano wa hizo research ni;

1.Investment research

2.Remmitace research

3. Market research

4.Medical research

5.Academic research


Ila kwa leo nitajikita zaidi kuielezea Academic Research kiundani na kwa namna ninavyoifahamu kwanza. Katika Academic Research mth anaweza kufanya research tofauti tofauti kutokana na format na category anayoihitaji yeye kama vile;

1️⃣ Quantitative Research
2️⃣ Qualitative Research
3️⃣ Mixed Methods Research
4️⃣ Experimental Research
Naa nyingine nyingi inategemeana na utafiti unavyokuhutaj wewe.

Sasa tuzichambue moja baada ya nyingine kwa undani zaidi tukianza na quantitative research.

1️⃣ Quantitative Research
Kwenye quantitative research hapa researcher mara nyingi huwa anatumia data za namba kwenye graphs na takwimu.

Ambapo data unaweza ukakusanya kupitia; surveys, experiments, questionnaires n.k, Hebu twende kwa huu mfano ili uweze kunielewa zaidi.

Hebu tuseme unataka kujua athari za muda wa kusoma kwa wanafunzi ukilinganisha na ufaulu wa wanafunzi wenyewe.

Tuseme labda unachagua wanafunzi 200 kati ya 400 ambao wapo kisha unaamua kuwahoji muda wao wa kusoma kila siku.

Unakusanya matokeo yao ya mitihani na kuchambua uhusiano wake na muda wao wa kusoma ulioupata kwa hao wanafunzi.

Ukiona kuwa wanafunzi wanaosoma zaidi ya masaa 3 au mawili wana ufaulu wa juu kwa 20% kuliko wale wanaosoma chini au ndani ya lisaa limoja, basi unakuwa umeshapata data inayothibitisha uhusiano huo.

Hivyo basi...

✅ Quantitative Research = Namba + Takwimu

Tuje aina ya pili ya research inayoitwa qualitative research.
2️⃣ Qualitative research
Aina hii ya research huwa hatutumii takwimu sana, badala yake unazingatia maoni ya watu, uzoefu wao, na hisia za watu kwenye jambo husika. Hivyo utatumia mahojiano, uchunguzi, na tafsiri za maandishi ili kupata uelewa wa kina.

Tukienda na mfano pia hebu tuseme unataka kujua kwa nini wanafunzi fulani wanapendelea kusoma usiku kuliko mchana.

Unawahoji wanafunzi 20 wanaosoma usiku na 20 wanaosoma mchana.

Unawauliza maswali kama;

1.Kwa nini unapendelea kusoma muda huu?

2.Unapata faida gani ukisoma mda huo?

Unakusanya majibu yao na kutafuta patterns katika maelezo yao.
Matokeo yanaweza kuwa:

Wanafunzi wengi wanasema "Usiku kuna ukimya hivyo concentration huwa inakuwa kubwa.

Wengine wanasema "Mimi ni mtu wa usiku, ubongo wangu unafanya kazi vizuri zaidi wakati huo kuliko mchana.

3️⃣ Mixed Methods Research
Hii aina ya research inahusianisha mchanganyiko wa quantitative na qualitative research Hivyo huwa inakupa picha kamili kwa kutumia namba na maelezo ya kina.

Aina nyingine ni Experimental research hii huwa inafanywa sana sana kwenye maabara na ipo kipractical zaidi so hebu tuiangalie nayo ipoje

4️⃣ Experimental Research

Tuseme unataka kujua kama kusoma usiku kunaboresha ufaulu wa wanafunzi.

Unachagua wanafunzi 50 na kuwagawanya katika makundi mawili:
✅ Kundi la kwanza – Wanasoma usiku pekee kwa mwezi mmoja.
✅ Kundi la pili – Wanasoma mchana pekee kwa mwezi mmoja.

Baada ya mwezi, unawapa mtihani sawa na kulinganisha matokeo yao.

Kama wanafunzi wa usiku wana ufaulu wa juu kwa 15%, basi unaweza kusema kusoma usiku kunaweza kuwa na faida kwa wanafunzi

Hivyo kwa kifupi sasa 📌

✅ Quantitative – Unatumia namba na takwimu.
✅️ Qualitative – Unatumia maoni na maelezo ya kina.
✅ Mixed Methods – Unachanganya takwimu na maelezo.
✅ Experimental – Unafanya majaribio ili kuthibitisha kitu.

Hizi ndizo aina za research zinazotumika kwenye academic research kama kuna niliyoisahau nisaidie kwa comments kupitia namba 0765772976

1.Unataka kujifunza zaidi jinsi ya kufanya research yako kwa usahihi?

2.Una shida na jinsi ya kuandika research proposal au data analysis?

Nicheki WhatsApp kwa msaada zaidi: wa.me/255765772976

#Research #AcademicWriting #Science
 

Ahsante sana mkuu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…