Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwa Mjini kama Dar es Salaam na kwingineko si jambo la ajabu kukuta makundi ya watu mabarabarani wakitembea kuelekea huku na kule , wengine masokoni , wengine kwenye viwanja vya soka , wengine wakitafuta Bar nzuri za kunywea pombe zao baada ya uchovu wa hapa na pale , wako pia wengjne wanaokwenda Mahakamani kusikiliza kesi za ndugu zao , na wengine wakiwa na barua za utambulisho wa serikali za mitaa na hati za mali zao ili kuwawekea dhamana wapendwa wao.
Sasa watu wa namna hii nao huwa wako kwenye maandamano au wanatafsiriwa wako kwenye mwendo upi ? Maandamano ni nini hasa ? Je wakivaa sare za namna fulani ndio huitwa wanaandamana? Tandika Mwembe Yanga haipiti siku bila kuona akina mama wakiwa kwa umati wametinga Sare za Vijola kwenda kumsuta mtu ama kwenda kwenye ndoa ya mkeka au ya halali , huku kigoma cha Uruguay kikiongoza njia , Je watu kama hawa tutaita wanaandamana?
Ni nini hasa maana halisi ya Maandamano?