Utajuaje kuwa ukaribu wenu ni zaidi ya 'urafiki'?

Bishanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2008
Posts
15,321
Reaction score
10,075
Mmekuwa watu wa karibu kitambo sasa,labda mko ofisi moja,darasa moja,mtaa mmoja etc. Mnaelezana mambo mengi hata yanayohusu mahusiano yenu ya kimapenzi na watu wengine. Mkiudhiwa na wapenzi wenu mnaambizana na kufarijiana,mkifurahishwa hali kadhalika.Ghafla mnaanza kuhisi mazungulukee na mahusiano yetu yanaanza kubadilika,kawivuuu kwa mbaaaaali kanaanza. Tuulizane wadau,ishawahi kukutokea hii,ulii handle vipi situation, kwa waliopitia hali hii nini dalili za kwanza kwamba 'ukaribu' unaanza kutoka ngazi ya 'urafiki' na kuwa 'romantic',je mwenzako aliipokeaje hii hali je naye alikudondokea au ndo yalikuwa mambo ya kuumizana roho? na je hao ma ex wenu waliichukuliaje ukizingatia wao walikuwa wanajua ninyi ni marafiki tu hivyo hata outing mlikuwa mnatoka wote?
.....Jumapili njema,Tanzania 5 Morocco 0......
 
mbali wapi Husninyo?

bishanga unaweza kuwa na rafiki wa jinsia tofauti ukahisi amefall in love kwako kumbe walaa.
Niliwahi kuwa na rafiki wa kiume, tulikuwa tunapatana sana halafu tulikuwa neighbours. Kadri siku zilivyoenda nikashangaa kwao wananichangamkia kupita kawaida. Ikafikia kipindi wengine wananiita wifi, wengine shemeji, mamdogo etc. Kumuuliza mshkaji. Dah,..... (Sikumalizii bwana).
 


hahahahaha akakutoa baruti... e bana eeh,pole,yote maisha bana,na maisha ni popote. lakini from your postings nahisi alipoteza lulu.
 
hahahahaha akakutoa baruti... e bana eeh,pole,yote maisha bana,na maisha ni popote. lakini from your postings nahisi alipoteza lulu.

khaaa! Sasa yeye ndio kapenda atanitoaje baruti?
 
khaaa! Sasa yeye ndio kapenda atanitoaje baruti?

alaaaaaaaaaaaa kumb tungo niliiangalia kiutata,haya hadisi njoo,twendelee,ikawaje? ulimtoa nduki?
 
hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa husninyooooooooooooooo me love u mwaaaaaaaaaaaaaaaaaah!
we mkali dah!
 
hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa husninyooooooooooooooo me love u mwaaaaaaaaaaaaaaaaaah!
 

Malizia basi na wengine tufaidi.
Wengine hijawahi kututokea.
 
Malizia basi na wengine tufaidi.
Wengine hijawahi kututokea.

hahaha! Kwa heshima ya peri kuquote post yangu ngoja niendelee.
Jamaa nikamuuliza amewaambia nini ndugu zake mbona naona kuna tofauti awali na sasa. Akawa anasita kusema, baada ya kumbana sana akaniambia amenitambulisha kwao (kumbuka hakunishirikisha na wala hatukuwahi kuongelea mapenzi ). Mdada pozi likaniisha, nilivyomuuliza kwanini alifanya hivyo wakati sisi sio wapenzi akasema "umekuwa mzuri sana kwangu na namna ulivyokuwa unanitreat nilijua hata nikikwambia tuwe wapenzi hautokataa". Dah, pozi liliniisha ikabidi nianze kupunguza kuwasiliana na kuonana.
Mnataka party 3 yake iendelee?
 
Kuna imani kuwa mapenzi hufanyika kukiwa na "Chemistry of Love". Hali hii kama itatokea kwa nyote, ndio hapo mapenzi huanza, lakini ikiwa ni kwa upande mmoja tu, muathirika anaweza akaangukia katika kupoteza rafiki na kutoaminiwa tena.

Ili kuhakikisha kuwa kweli mahusiano yenu ni mapenzi, lazima mpitie hatua tatu: 1. Matamanio 2. Mvuto. 3. Mapenzi/Upendo. Katika hatua ya 1&2 inaweza kuwa kwa upande mmoja au pande zote mbili, mkatamaniana, kuvutiana na hata kujaribiana, lakini hii huwa kwa muda tu. Msipofika hatua ya 3 itakuwa mmo katika kutafuta, na ikiwa mtafikia hatua ya mapenzi mnakuwa vipofu na viziwi (hapa inakuja ile Love is blind) kiasi hamtoona wala kusikia weengine wanasema nini.
 
Unaweza kuniita old fashioned lakini ndio maana mimi huwa nasisitiza hakuna kitu kama urafiki wa karibu baina ya jinsia mbili tofauti (I mean best friend thing). Hiyo kitu lazima mwisho wa siku mmoja wapo imzidi, imenitokea sana tu.
 
Usitubanie, Malizia kabisa mapaka part ya mwisho. Haujui mwisho ndio kankonoga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…