Utajuaje ukubwa wa timu kubwa?

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
  • Baada ya mechi ya juzi viongozi wa Tp Mazembe kusema, Yanga ni timu kubwa Tanzania [emoji1241] kuliko timu yoyote kumeibuka mijadala mikubwa kuhusu nini hasa kinafanya timu iitwe kubwa ?!
  • Binafsi nachojua ili uwe timu kubwa ni lazima uwe na makombe mengi yaliyo rasmi yanayotambuliwa na (CAF) au (FIFA)
  • Pamoja na hayo ili uwe mkubwa lazima uwe kwenye top (3) kila msimu kwenye ligi yako pasi na kutoka hapo ipi ni timu kubwa hapa Tanzania?
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
  • Simba SC na Young Africans SC ni vilabu vikubwa nchini Tanzania [emoji1241] na Africa Mashariki, hilo halihitaji degree kujua
  • Ukweli unauma siku zote, na ndio tabia yake ya asili. Naelewa wapo watakao tukana kwenye andiko hili lakini ieleweke, ukweli hauwezi kuachwa kusemwa eti kwa sababu ya kuhofia matusi[emoji117]
  • Turejee kwenye hoja ya msingi,, Dhana ya kwamba Simba SC ni klabu kubwa kuliko Yanga SC mizizi yake haijishikizi kwenye udongo ili kuifanya istawi. Ukubwa upi unazungumzwa hapa?
  • Ukubwa wa klabu ni mataji[emoji471]na sio mataji tu bali mataji yenye hadhi yanayotambuliwa na (CAF) au (FIFA) ndiyo yanayoipa klabu UKUBWA
  • Baada ya mataji ndipo vinafuata vitu kama MIUNDOMBINU, UWEKEZAJI E.t.c .. Vitu ambavyo Simba na Yanga hawajazidiana sana.

Pyramids ya misri ni klabu ya pili Africa kwa klabu zenye thamani kubwa lakini si klabu kubwa kuizidi Zamalek kwa sababu haina mataji yenye hadhi ya kuipa ukubwa.

Tukiangalia hapa nyumbani mataji yenye hadhi ya juu kwetu ni (2)tu, ambayo unaweza pita kokote na kutamba nayo
[emoji471] 27 = Ligi kuu Young Africans sc[emoji471] 22 = Ligi kuu Simba sc

[emoji471] 03 = (FA) cup Simba SC
[emoji471] 01 = (FA) cup Young Africans

- Kuna mambo (3) ambayo klabu ya Simba SC wakiyafanya yatawapa uhalali (LEGITIMACY) ya kuitwa timu kubwa kuliko Yanga SC
1. Simba SC Kuwapiku Yanga SC idadi ya makombe ya ligi kuu
Tanzania bara
au

2. Kutwaa ubingwa wa Africa, klabu bingwa Africa au Shirikisho (CAF)
3. Yanga SC kupotea katika ramani ya soka, kwa maana gani? Ishuke daraja au isiwe title contender kwa kushika nafasi nje ya top (3) kila msimu ligi kuu Tanzania bara
- Bila hivyo bado Simba SC haina uhalali wa kuitwa timu kubwa kuliko Yanga SC.
 
Una hoja kimtindo

Unanikumbusha mashabiki wa chelsea wenyewe hua wanataka mjadilia makombe kuanzia miaka 10 nyuma
 
Yaani kishabiki kimoja cha mazembe kuwafariji kwamba wao ni timu kubwa wanadhani mashabiki wa mazembe wote ni wapuuzi kama wengine,wacheze mpira wasipende cheap popularity
Unatumia msuli Sana aisee [emoji1787][emoji1787]
 
Huo ni upunguani kusema mataji makubwa ni mawili kwa ajili ya interests zako kuonyesha Yanga ina makombe mengi ,hayo makombe mengine umeyaficha kwapani ili ujifariji ,mbona hayo makombe mengine kama hayana umuhimu ulikuwa unaingia uwanjani kukata mauno? Mgesusia hayo makombe mengine ,hutaki usitake hayo makombe yote hayafutiki yako pale pale ni historia haifutiki.

Je Kombe la club bingwa na shirikisho Africa siyo makombe? Kwahiyo Simba angeshinda ungeyaweka pembeni kisa Yanga hajashinda .

Lucy hakukosea
 
Huo ni upunguani kusema mataji makubwa ni mawili kwa ajili ya interests zako kuonyesha Yanga ina makombe mengi ,hayo makombe mengine umeyaficha kwapani ili ujifariji...
Hongera Sana Mbumbumbu kwakuwa bingwa wa kihistoria wa mtani jembe
 
  • Baada ya mechi ya juzi viongozi wa Tp Mazembe kusema, Yanga ni timu kubwa Tanzania [emoji1241] kuliko timu yoyote kumeibuka mijadala mikubwa kuhusu nini hasa kinafanya timu iitwe kubwa...
Ungeweka ushabiki pembeni ungekuja na mada nzur...al ahly ndio club yenye makombe mengi duniani je makombe yote yanayowafanya watambulike na makombe mengi duniani yanatambulika na FIFA na CAF.
 
Lenu nyie ambalo sio la 'historia' Yaani current ni Mapinduzi Cup.

Bwana Yule angekuja na slogan hii 'Return of Mapinduzi Cup Champion'.

Mbona angeeleweka...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…