21/3 haya bashiri, but kama ni mambo mabaya just tell kwenye pm usiyaweke hapa
Mimi nitakubashiria lakini mimi sio Sheikh wala sio Mganga wa kienyeji wala sio Nabii wala sio Mchungaji.Kwa tarehe uliyotowa yaani 21/3March inakwenda hiyo Tarehe mpaka tarehe 20/4April kutoka Marach21,22,23,24, na kuendelea mpaka April 20.
NYOTA YA PUNDA AU KONDOO (ARIES)
Hii ni nyota ya kwanza katika mlolongo wa nyota 12.
Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21st March na tarehe 20 April ya mwaka wowote.
Sayari yao ni Mars (Mariikh)
Siku yao ya bahati ni Jumanne
Namba yao ya bahati ni 9
Rangi yao ya Bahati ni Nyekundu.
Asili yao ni Moto.
NYOTA YA PUNDA KATIKA MAPENZI NA MAHABA
Kwa vile wao ni wenye nyota ya kwanza mara nyingi wenye nyota hii wanapenda kuwa mbele. Wanakuwa wakarimu na wenye pendo kwa wapenzi wao.
Ni watu wenye kupenda kushirikiana na watu wengine, wanapenda mikusanyiko ya jamii na wacheshi. Ni watu wazuri kuwa nao karibu na mara nyingi wao wanakuwa ndio maisha na roho ya kundi wanalojihusisha nalo. Hivyo inatokana na
tabia zao za asili za uchangamfu. Hata hivyo wakiudhiwa huwa ni viumbe wenye hasira kali.
Wenye nyota hii ni wepesi sana kuvunjika moyo na hii inatokea wakati wapenzi wao wanapowaangusha au
kuwadharau katika mapenzi ambayo wao wanayachukulia kwa uzito mkubwa.
Pamoja na uchangamfu walio nao wenye nyota ya Punda wana moyo dhaifu usiovumilia matatizo na wanaweza kudhuriwa kirahisi katika mapenzi.
Wanaingia katika mapenzi na kupenda kirahisi. Mara nyingi wanawafanya wapenzi wao ndio nguzo au kiegemezo na hapo ndipo matatizo yanapoanza.
Wasipopata njia ya kutatua matatizo ya kimapenzi huwa wanachanganyikiwa na wanafadhaika sana hasa wanapogundua kwamba wapenzi wao ni binadamu kinyume na walivyofikira wao.
Kwao wazo la kuwa waaminifu kwa mpenzi mmoja milele linapewa kipaumbele katika mambo ya mahaba, lakini wakiona mambo yanaenda kombo basi ni mwepesi sana kuondoka kwenda kutatufa mpenzi mpya sehemu nyingineyo.
Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kuwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali
kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu.
Hayo ninakupa kwanza machache yapo mengi ila ninakupa kidogo kwanza upate kusoma.