Kwa sababu yoyote ile, iwe ni kwa kuteleza au kwa uchakaramu wako,
lakini mwenzako amegundua au ana wasiwasi nawe kuwa si mwaminifu
katika mahusiano na akaamua kukuuliza kutaka ukweli. Jee:
Utakiri na kutubu? Utaongopa lakini utatubu? Utaongopa na utaendelea?
Ni mazingira gani yatakufanya uchukue uamuzi mmoja au mwengine?
Nimekupata Mkuu, bila ubabe au kutaka yaishe, ikiwa ni kweli hauko mwaminifu,,bora ni lipi, kukiri au kuuchuna?[/QUOTE
kuuchuna na kurekebisha tabia yangu
It wasnt me....
Nimekupata Mkuu, bila ubabe au kutaka yaishe, ikiwa ni kweli hauko mwaminifu,,bora ni lipi, kukiri au kuuchuna?
Ni kumuacha anayekutuhumu athibitishe........... kwa mfano, LINI, WAPI,SAA NGAPI, NA NANI.......................
Hongera zake, akomae hivyo hivyo!Dah mimi mwenzeni kila nikitaka kuakupiga kazi za nje wife ananishtukia dah, mpaka najionaga **** .... nimeamua kutulia NGURUWE PITA SINA MKUKI MIYE!!!!!
Ninakubaliana nawe lakini si wanawake wote wanaokubali kusamehe. Ile akisikia tu harufu ya usaliti anakunja virago na hakuna kumrejesha nyuma. Pia si wanaume wote wasiosamehe wake zao; kuna wengine sijui kama ni kupenda kupindukia, ufahamu kuwa binadamu tunakosea au vipi, lakini wapo wanaosamehe.Kwa mwanamke itakuwa ngumu kukiri kwa sababu hatua inayofuata hapo kila mtu anaijua ni ngumu sna kwa mwanume kumsamehe mwanamke msaliti. Ila kwa mwanaume atasema tu anajua atasamehewa,
Hapo red! Inaonesha kama mtu hakukamatwa kwenye mlo, anaweza kuzua lolote ili asikubali kosa lake. Tatizo kwa kutumia hoja ya nguvu wanaume ni rahisi kukwepa na wanawake kuingia mtegoni. Mwanamke akikiri anatafuta kipigo na talaka, asipokiri kisago mpka atajuta. Wanaume wengine kama polisi wa mahabusu.kukiri kunategemea na mazingira lakini mara nyingi wanaume wanaweza kukiri kutoka nje kama kufupisha kelele au ugomvi ilihali hajafanya hivyo , hasa akikutana na mwanamke muongeaji na yeye si muongeaji.. wanawake wanatengenezewa mazingira ya kipigo na inamlazimu kukiri kwamba katoka au alikaribia kutoka katikka kujinusuru kipigo
Boss mbona umeruka?It wasnt me....
Hii ndio hiyo kutafuta hoja ya nguvu - hakuna ushahidi, hakuna kosa, hata kama umekosa.Ni kumuacha anayekutuhumu athibitishe........... kwa mfano, LINI, WAPI,SAA NGAPI, NA NANI.......................
Bora kuuchuna na kujirekebisha na kuacha kabisa, haya mambo ya kukiri kiri hovyo yanaweza leta balaa bure ikala kwangu.[/QUOTE]. Hapo red: Bora nusu ya shari kuliko shari kamili, ingawaje kiustaarabu bora kukiri, hatari zake ni kupunguza mapenzi usiaminike tena.