"....utakuta kuna Wazanzibari na Wazanzibara!..., utakuta hivyo!"

"....utakuta kuna Wazanzibari na Wazanzibara!..., utakuta hivyo!"

Mzanaki

Member
Joined
Feb 25, 2011
Posts
20
Reaction score
11
.......na pia wamo "Watanganyika na Watanganzibar!.

Mimi shida yangu ni utitiri wa maraisi kwenye hii rasimu ya katiba!...Tunahitaji raisi wa shirikisho halafu hao wengine wawe mawaziri wakuu!..Waziri mkuu wa Tanzania bara na Waziri mkuu wa Zanzibar. Hawa ndio wawe watendaji wakuu katika hizi inji mbili. Maraisi watatu hawa kwanza watusababishia foleni bure!.
 
Na pia wamo "Watanganyika na Watanganzibar!; Hii rasimu ya katiba itawaanika wote hawa waliotabiriwa na babu yangu Nyerere.

Mimi shida yangu ni utitiri wa hawa maraisi!...Tunahitaji raisi wa shirikisho halafu hao wengine wawe mawaziri wakuu!..Waziri mkuu wa Tanzania bara na Waziri mkuu wa Zanzibar. Hawa ndio wawe watendaji wakuu katika hizi inji mbili. Maraisi watatu hawa kwanza watusababishia foleni bure!.
 
Hayo ni maoni yako,ya kwangu mm ni mamlaka kamili ya z'br ikifuatiwa na muungano wa mkataba wa nchi yoyote kati ya kenya,uganda,nigeria au tanganyika wakipenda.
 
Kwani huyo Waziri Mkuu au Chief Minister hawatuwekei foleni?

Sema jinsi ya kuwahudumia walau gharama zipungue tu.
 
Mi sipo watakapoanza kubaguana upemba, uunguja sijui umjimkongwe.. nk.
Nafurahia rasimu. Tuwe serikali tatu. Maana tumechoka kunyonywa ndani ya mwavuli wa serikali mbili.
Eti tulikuwa tunagawa keki kati kati, afu ile yetu wao wanahaki nayo tena kama wanaJMT. LoL
 
Regionalism imeshaingia tanzania tusipokuwa makini huu ndio mwanzo wa matabaka , ukabila na udini
 
Hakuna nchi itwayo tanzania bara
Na pia wamo "Watanganyika na Watanganzibar!; Hii rasimu ya katiba itawaanika wote hawa waliotabiriwa na babu yangu Nyerere.

Mimi shida yangu ni utitiri wa hawa maraisi!...Tunahitaji raisi wa shirikisho halafu hao wengine wawe mawaziri wakuu!..Waziri mkuu wa Tanzania bara na Waziri mkuu wa Zanzibar. Hawa ndio wawe watendaji wakuu katika hizi inji mbili. Maraisi watatu hawa kwanza watusababishia foleni bure!.
 
Hakuna nchi itwayo tanzania bara
Umeona eeeeh!!!, hii ni sawasawa na mkuu wa nchi kuogopa kutamka kuwa serikali haina dini,
Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara, mimi ni MTANGANYIKA, tuheshimiane tafadhali!!!!!!!!.
 
Umeona eeeeh!!!, hii ni sawasawa na mkuu wa nchi kuogopa kutamka kuwa serikali haina dini,
Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara, mimi ni MTANGANYIKA, tuheshimiane tafadhali!!!!!!!!.

Mkuu punguza munkari kidogo!
 
Mkuu punguza munkari kidogo!

Inakera mkuu, tunawabembeleza sana wazanzibari, tunakubali sana kufuata masharti yao, kwenye kuunganisha TANU na ASP wazanzibari walishinikiza izaliwe february 5, kama chama chao cha ASP tukakubali, wakashinikiza chama kipya kiitwe Chama Cha Mapinduzi ili kuenzi mapinduzi ya zanzibari tukakubali, Kwenye Muungano wakashinikiza hadhi ya zanzibar ibaki pamoja na serikali kamili tukakubali kuua Tanganyika, sasa nafasi ya kurudisha Tanganyika yetu katika mfumo wa serikali tatu unataka kupatikana halafu wanataka kuleta ujanjaujanja tu wa kuita Tanzania bara badala ya Tanganyika,

We want Tanganyika, to hell what they call Tanzania bara.
 
Napata kichefuchefu nikisikia watu wanazungumzia serikali ya Tanzania bara. Hawajui kwamba humo ndani ya jina Tanzania tayari kuna Zanzibar?? Kwa mantiki hiyo Zanzibar itakuwa na serikali yake na nusu ya serikali ya Tanzania bara!
 
Back
Top Bottom