SoC04 Utalii kukua kidijitali

SoC04 Utalii kukua kidijitali

Tanzania Tuitakayo competition threads

usshindi

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
5
Reaction score
10
Utalii ni Neno Pana na lenye manufaa makubwa kwenye uchumi wa taifa letu la Tanzania.
Uchumi wa nchi yetu ya Tanzania unategemea rasilimali mbalimbali ikiwemo rasilimali inayohusisha vivutio vya utalii na utalii wenyewe.

Kutokana na umhimu wake kwenye pato la taifa utalii hutakiwa kutangazwa na Kila mtu kwani nchi zenye vivutio zipo nyingi na Zina vivutio tofauti tofauti vingine vikifanana na vilivyopo Tanzania na vingine vikiwa havipatikani Tanzania yetu.Kila mtanzania ana wajibu na haki ya kuutangaza utalii na kufanya utalii katika vivutio vya utalii nchini.Mabalozi wa nchi yetu na nchi zenye mahusiano na sisi kidiplomasia ndio hutumika kwa kiasi kikubwa matangazo ya runinga machapisho ya majarida na mabalozi binafsi kama timu za mpira na wasanii hufanya kazi kubwa kutangaza utalii na vivutio vyetu.Pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dr Samia Suluhu Hassan kwa kufanya mkanda wa video THE ROYAL TOUR unaotangaza vivutio vya utalii na kua miongoni mwa sababu zilizopandisha idadi ya watalii nchini kwetu ni jambo kubwa na jambo la busara.

Katika kutambua mchango wa Kila mtanzania akiwemo mama yetu mheshimiwa nilitafakari njia kadhaa ambazo zinaweza kutumika kumuunga mkono rais wetu na wananchi wote kwa ujumla katika kuutangaza utalii kwa njia za mtandao kama maoni yangu yakiwekwa katika vitendo Kuna matarajio ya kuongezeka kwa pato la taifa kupitia utalii wa ndani na WA nje na kuchangia shughuli nyingi za kiuchumi na kimaendeleo nchini kwetu

Njia ya kwanza ni kupitia michezo ya mtandaoni(online games) nchini kwetu michezo ya mitandaoni inaruhusiwa na mara nyingi huchezwa na wale watu wanaomiliki simu janja na kompyuta kwa aina zake.michezo hii humuruhusu mtu kucheza mchezo huo na mtu mwingine yeyote aliyepo nchi yoyote Ile duniani mwenye mchezo kama huo na aliyepo mtandaoni.Kwa kasi kubwa michezo ya mitandaoni imezidi kuongezeka na idadi kubwa ya vijana hupenda michezo hii ushauri wangu ni vijana kuitumia hii fursa kuutangaza utalii wa nchi yetu.

TUFANYE VIPI VIJANA?
Ni rahisi tu Kuna michezo inayoruhusu watu wawili kuwasiliana kwa maneno wakati wa michezo na Kuna michezo inaruhusu kuwasiliana kwa emojis wakati wa michezo na michezo mingi inaruhusu mtu kutumia majina yake atakayopenda mda wote wa mchezo.Hii nifursa kwetu vijana kuunga mkono zoezi la kuutangaza utalii kwanza kwenye jina unaeza tumia jina la kivutio chochote Cha utalii kilichopo Tanzania ukianza na Neno visit kwa mfano visit mt Kilimanjaro visit Serengeti .mtu utakaecheza nae kama akiwa wa nchi za wenzetu atatamani Kujua hii Serengeti ni Nini au hii Kilimanjaro ni wapi atatafuta kwa mtandao na ataangalia na anaeza panga kuitembelea ili ajue Nini kizuri mpaka wacheza michezo wanaisifia kwa mfano mimi hua nacheza mchezo wa Dream league 2024 nimeiita timu yangu visit Tanzania(picha kwenye viambatanisho)na kocha wangu nimemuita Mt Kilimanjaro na wakati nikicheza hua natumia emojis za ukarimu kama kusalimia kufurahi hata nikifungwa hii inatangaza ukarimu tulionao kumbuka ukarimu ni silaha kubwa ya kukuza utalii.Kama simu au mchezo wako utaruhusu kutumia maneno yaani kuchat baada au wakati wa michezo tumia nafasi hiyo kumkaribisha mgeni wako nchini kwa ajil ya utalii.wakati mwingine ikiruhusu picha tumia picha ya vivutio inapendeza na watalii wataongezeka

Njia nyingine ni kupitia ads(advertisement) mtumiaji wa mtandao na mchezaji wa games mbalimbali hua anakutana na hizi ads mara kwa mara nyingine zikiwa mbaya na nyingine nzuri kwa mfano kampuni la Alibaba katika mchezo wa dls wanatoa advertisement ya bidhaa zao Ili mchezaji aweze kupata gold coins kwa matumizi yake.Nchi yetu inayo wizara inayohusika na utalii ni vyema kuingia mikataba na kampuni za michezo inayochezwa sana na kutengeneza ads zenye vivutio vyetu Ili ziwe zinakuja kama ilivyo za makampuni mengine hii itasaidia kuutangaza utalii katika maeneo mengi duniani kwa kua siku hizi vijana wengi ni wapenzi wa michezo nchi kupitia wataalam wake wanaweza kutengeneza michezo ya kuwinda na kukimbia katika mazingira ya vivutio vyetu kwa mfano mchezo wenye jina la hunting in ngorongoro na kuweka mandhari za ngorongoro na baada ya kutengeneza wakapakia mchezo huo kwenye googlestore vijana wengi wataicheza michezo hiyo na utalii wetu utakua kwa Kasi kubwa na uchumi wa nchi yetu utakua sana jambo linguine ni kwa content creators(watengeneza maudhui) maudhui yamekua ni biashara kubwa sana duniani kwa miaka ya karibuni wao hua na wafuasi wengi na tofauti tofauti nchini Tanzania kwangu naiona ni fursa Tanzania kupitia wizara kusaini mikataba na watengeneza maudhui wakubwa hasa nchini kwetu kutumia mandhari za vivutio vyetu Ili kukuza soko la utalii hapa nchini kwetu na nchi zote yangu ni hayo na yakizingatiwa yajayo yanafurahisha.Visit Tanzania witness beauty of the world
 

Attachments

  • Screenshot_20240623-055319.jpg
    Screenshot_20240623-055319.jpg
    439 KB · Views: 3
  • Screenshot_20240623-054010.jpg
    Screenshot_20240623-054010.jpg
    573.7 KB · Views: 4
  • Screenshot_20240623-054000.jpg
    Screenshot_20240623-054000.jpg
    814.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20240623-053915.jpg
    Screenshot_20240623-053915.jpg
    622.5 KB · Views: 2
Upvote 6
Back
Top Bottom