SoC04 Utalii ni tiba

SoC04 Utalii ni tiba

Tanzania Tuitakayo competition threads

kabwiga

New Member
Joined
May 29, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Mpaka 2022 nilienda kutalii nikiwa na rafiki yangu katika hifadhi za tarangire national park, like manyara national park, mikumi national kisha saadan national park tukamalizia pugu kazimzumbwe (ushoroba)

Sababu ya kufanya utalii huo wa muda Mlefu na maeneo tofauti ilikua ni kuangaria namna ya kunisaidia kuondokana na tatizo la hasira hizo gharama zote zililipiwa na mtu baki tu ambaye tukikutana kanisa moja akatokea kunielewa nami nikamuelewa tukawa marafiki. Changamoto yangu ikawa hasira za alaka pamoja na kususa,

Alipo nipeleka kwa msaikorojia akatwambia Nina tatizo la afya ya akiri hivyo Ili kupona ni mawili

1: Nitalii
2: nisome Sana vitabu pamoja na makala uku nikipata uangalizi wa karibu na kunijari sana.


Rafiki yangu huyo akachagua vyote kwa pamoja.

Kabura mtaaramu huyo wa sekrojia ajashauri aliniuliza sababu ya jina langu sababu ni Jina la kushangaza.
Jina langu ni Damu N Kabwiga

Alikazana sana kutaka kujua kwanini wazazi wangu waliamua kunipa jina la Damu

Ikabidi nimueleze ukweli.

Mimi ni mzaliwa wa kisiwa bumbile kilichopo wilaya muleba mkoa Kagera kisiwa bumbile kina visiwa vingi vidogo kama kisiwa Iroba, Kerebe, Kinagi, Maiga na Ishenyi.

Katika visiwa vyote hivyo ni Ishenyi pekee yenye huduma ya Zahanati hivyo Ili mgonjwa kupata matibabu inabidi upatikane mtumbwi wa kumvusha kumtoa kisiwa alichopo kwenda Ishenyi.

Nyumbani kwetu ni Iroba.

Ziwa Victoria linalo zunguka visiwa hivyo ni ziwa lenye upepo mkali sana unaweza kupiga hata wiki mzima bira kupungua.

Hivyo uwa ni hatari sana pale inapo tokea mama mjamzito anakaribia kujifungua na upepo ukapiga kwa kipindi hicho.

Ndicho kilicho tokea kwa mama yangu Mimi, akiwa amebakiwa siku chache Mimi kuzaliwa.

Naomba niweke kumbukumbu sawa stori ya namna nilivyo mzaliwa niliadithiwa na baba yangu mzazi.

Ulipiga upepo mkali sana kwa wiki nzima wakati upepo unakata wakamuweka mama kwenye mtumbwi namanisha mtumbwi wa kasia ule mgogo sio bolt inayo tumia mashine.

Wakati wako katikati ya maji mama alisikia uchungu na kujifungua mtoto ambaye ni Mimi.

Kwakua hakukua na mtaramu wa afya mama yangu alitokwa na damu nyingi, mpaka wanamfikisha Zahanati mama yangu anafariki Dunia kwa kutokwa na damu nyingi.

Hivyo baba yangu akaona jina litakalo muenzi mama ni kuniita Damu.

Nilipo Anza kua mkubwa kidogo wa kwenda shule nilikua nikitengwa sana na watoto wa ndugu zangu pamoja na majirani,

Wakiniita Damu ya rahana uku wakisema Mimi Nina nuksi kwa sababu kuzaliwa kwangu kulisababisha kifo cha mama yangu shuleni nako watoto walikua awakai na Mimi dawati moja.

Watoto walimezeshwa sumu nikachukiwa kweli kweli awakucheza na Mimi wala kukaa na Mimi njiani wakati wa kwenda au kutoka shule awakuongozana na Mimi.

Ikanitengenezea hasira Sana nikawa nawachukia watu, hata kwa kosa langu mwenyewe.

Nikiwa darasa la Tano nikamkwaza baba yangu naye akanifukuza nyumbani.

nikaishi kama mtoto wa mtaani, shuleni nikawa mkorofi wakanifuta kwenye orodha ya wanafunzi lakini awakuniambia. Nilipo maliza darasa la Saba.
na ninajinunulia Kila kitu madafutari na huduma zote Ili nisome kwa kufanya kazi za uvuvi usiku.

Matokeo ya darasa la Saba yanakuja jina langu alipo kwenye ubao wa majina

Nikaenda wilayani kwa afisa elimu akaniambia niliacha shule toka darasa la Tano. Iliniuma sana baada ya kujua kua miaka miwili yote napambana silali kumbe sihesabiki kama mwanafunzi.

Nikapachukia nyumbani nikatoka mkoa Kagera nikaja kupambana dar es salaam bira kujua nitafikia kwa nani nitafanya Nini nakumbuka siku tatu za mwanzo nililala ubungo stendi ya mabasi.

Asira za mara kwa mara zikanifanya niwe mtu wa magomvi Kila mara nikawa wa kukamatwa na kuwekwa polis.

Kama vituo vya polis chanika, ostabey na stakishari.

Baada ya kumuelezea Ali hiyo msaikorojia ndio akashauri ushauli wa kutalii au kusoma vitabu.

Rafiki yangu akasema tutafanya vyote, alipo pata likizo kazini kwake akaniambia twende akalipia gharama zote kwa sababu kwa kipindi hicho hata uwezo wa kujilisha Milo miwili sikua nao.

Tukaanza kutalii uku usiku tukisoma vitabu.

Taratibu nikaaza kupunguza asira, nikaacha kususa na kuanza kufikiria kumiliki vitu vikubwa na vizuri.

Nikapenda sana utalii ikabidi niulizie taratibu za kusajiri kampuni kwa sababu elimu yangu hainiruhusu kuajiriliwa kama muongoza watalii,

Nikakosa vigezo vya kua na kampuni ya Utalii kwa sababu sikua na hea ya usajiri pamoja na magari ya Utalii

Nikaomba kua balozi wa ihari

Kuutangaza utallii na kuwawezesha watalii kutalii kirahisi.

Nikapata nafasi Leo hii.

Kwa mwezi napata kati ya watalii 30_50

Uku nikiendelea kujikusanya Ili kua na kampuni nimeambatanisha na picha za baadhi ya watalii wangu.

Tayari tusha maliza tofauti zetu na baba na sasa ni marafiki sana.

Hila mpaka sasa nyumbani hakuna huduma zozote za kiafya kitendo kilicho sababisha miezi mtatu ilivyo pita kumpoteza ndogo wangu aliye chomwa kisu saa tatu usiku akafariki saa mbili asubuhi akipelekwa hospital.

Kimsingi nyumbani ni eneo hatari halina kituo cha polis, halina hospital wala umeme na ni eneo lenye wakazi wengi kwa sababu ya shughuri za uvuvi.

Watu wanaishi kwa neema ya Mungu.

Lakini Niko hapa kuwambia kua asiri ni tiba.

Kukaa kwenye maeneo asiri ya Utalii yalinitibu na sasa Niko vizuri na ninayo furaha sana.

Nashauri Wana jamii form kutunza mazingira na kuhishi maisha arisi kusamehe, kuto kuwanyanyapaa watu kwa sababu yoyote ile.

Asante kwa kusoma andiko langu.
 

Attachments

  • TRIPART_0001_BURST20240525125111911_COVER.JPG
    TRIPART_0001_BURST20240525125111911_COVER.JPG
    2.5 MB · Views: 8
Upvote 3
Sababu ya kufanya utalii huo wa muda Mlefu na maeneo tofauti ilikua ni kuangaria namna ya kunisaidia kuondokana na tatizo la hasira hizo gharama zote zililipiwa na mtu baki tu ambaye tukikutana kanisa moja akatokea kunielewa nami nikamuelewa tukawa marafiki. Changamoto yangu ikawa hasira za alaka pamoja na kususa,

Alipo nipeleka kwa msaikorojia akatwambia Nina tatizo la afya ya akiri hivyo Ili kupona ni mawili
Ahsante umetushirikisha kumbe ni dawa!!!?
Ndo maana wasomi waliosafirisafiri wengine wakafika hadi nje wakaishi huko.... wanakuwaga waelewa sana.

Nashauri Wana jamii form kutunza mazingira na kuhishi maisha arisi kusamehe, kuto kuwanyanyapaa watu kwa sababu yoyote ile
Na ndugu yangu Damu nikuombe kitu kimoja. Hata kama watu hawakuelewa ujio wako na kifo cha mama ako. Tambua kwamba hujamuua wewe. Alifariki kwa changamoto za uzazi ambazo wewe hukuhiyari kwa lolote wala maamuzi. Mtu anapaswa kulaumiwa kwa mambo aliyoyaamua na si bahati mbaya kama hizo hata haujitambui. Pole sana
 
Back
Top Bottom