Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeweka nondo za kutosha mkuu, Heko.Soma zaidi hapa Isimila - Wikipedia, kamusi elezo huru
Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Njia ya kuingia si rahisi kuikuta iko kabla ya kufika kwenye kijiji cha Tanagozi ukitoka Iringa na kuingia upande wa kushoto.
Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa wa Iringa.
Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hili ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa hapo tangu mwaka 1951.
Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana kati yao ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina tofauti ya viboko.
Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila, ambalo lina mikondo miwili, ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zana nyingine na shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.
Marejeo
Viungo vya nje
- Zama za mawe za kale za Isimila
- Isimila
- The Isimila Stone Age Project, tovuti ya University of Brighton, iliangaliwa Machi 2018
- Isimila Stone Age Site, tovuti ya Lonely Planet