Soma zaidi hapa
Isimila - Wikipedia, kamusi elezo huru
Isimila ni eneo la
kihistoria lililopo
mkoani Iringa nchini
Tanzania, katika
kijiji cha
Ugwachanya kwenye
kata ya
Mseke kilichopo
kilomita 20 kutoka
Iringa mjini karibu na
barabara kuu ya A 104 kuelekea
Mbeya. Njia ya kuingia si rahisi kuikuta iko kabla ya kufika kwenye kijiji cha Tanagozi ukitoka Iringa na kuingia upande wa kushoto.
Eneo hili ni
kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa wa Iringa.
Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu
Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hili ndipo
zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa hapo tangu mwaka
1951.
Pia ndani ya eneo hili
mafuvu na
mifupa mingi ilionekana kati yao ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na
twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na
shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina tofauti ya
viboko.
Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka
laki tatu hadi
nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika
korongo la Isimila, ambalo lina mikondo miwili, ni pamoja na
mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya
kombeo kwa ajili ya
uwindaji.
Pia vifaa kama
nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zana nyingine na
shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa,
nyembe na
visu.
Marejeo
Viungo vya nje