Utamaduni na tasnia ya filamu Tanzania

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Habari wakuu, naomba mnisamehe kwa kuwa kimya sana, majukumu ya hapa na pale. Kama kawaida naomba kuleta uzi kuhusu jamii zetu. Leo nimeona ni vyema nikazungumzia tasnia yetu ya filamu hapa Tanzania (Bongo Movie).

Kiukweli tupo nyuma kabsa katika kuwapatia watoto wetu utamaduni na mila ikiwemo kuelewa historia ya jamii mbalimbali haswa jamii ambazo wamezaliwa nao kupitia luninga.

Amini usiamini kuna watu hata majina matatu ya babu zao ama bibi zao hawayajui, inasikitisha sana ila mtu huyo huyo anafahamu majina ya familia nzima ya kardashian.




Janga kubwa hili.

Nilifurahi na kuumia kwa wakati mmoja nilipotazama tasnia ya filamu ya Hollywood ambao wanatumia filamu na tamthilia pamoja na nyimbo kuendeleza utamaduni na kuyafanya majina ya watu mashuhuri yaendelee kuishi.

Majina kama Joseph Brant, Lone Horn, Bill Bowlegs, Geronimo, Lozen, Osceola, pamoja na Red Cloud ni majina ambayo ni maarufu kwani hata katika filamu mbalimbali basi husika zao zimeonekana! Wakionesha ushujaa na morali ya kupambana.

Upande wa muziki ndo wamewaenzi kila kona;
1. “Indian Outlaw” kutoka kwa Tim McGraw



2. “America the Beautiful” kutoka kwa Jody Brown Indian Family.



Kwetu huku Tanzania, nimepata kutazama filamu ya Mkwawa pekee ambapo mwanadada Seko Shamte alipambana akiwa na waigizaji kama vile, Mutaju Issac Marobhe, Paul Clithero pamoja na Doug Bramsen.

Seko Shamte


Mkwawa: Shujaa wa Mashujaa



Kwa Hollywood na dunia huko kuna filamu chungu mbovu kuhusu mashujaa wa makabila ya wahindi wekundu;

Dance with Wolves (1990)




Shalako (1968)


Against a Crooked Sky (1975)


Two Rode Together (1961)


Grayeagle (1977)




Na zingine nyingi tu.
Kweli tumeshindwa hata kutengeneza filamu kuhusu mashujaa wetu ili vizazi na vizazi viendelee kusoma kuhusu utamaduni wetu.
1. Kimweri Mputa Magogo
2. Mganila Nonga Bukoli
3. Ludomya Ng’hwele
4. Thomas Marealle Mbegha
5. Mangi Meli
6. Chief Mirambo
Tatizo lipo wapi mpaka tunakosa filamu zinazoelezea utamaduni wetu na makabila zaidi ya 128 bado hatujaruhusu filamu zituoneshe wahusika wa zamani waliobeba utamaduni wa makabila yetu.

Hawa wahindi wametuacha mbali;

1. Lagaan (2001)



2. Manjhi: The Mountain Man (2015)


3. Lakshya (2004)



Tumebakia kuoneshwa mambo ambayo ya tofauti tu tena yasiyo na umuhimu kwetu. Leo dada na mama zetu wanafurahia tamthilia ya La Sultana: The story of Kosem, lakini ni 5% tu au chini ya hapo wanajua kuwa hiyo sio tamthilia ya kutugwa tu bali ni maisha halisi ya Kösem Sultan moja kati ya mwanamama aliyekuwa na nguvu sana kwenye utawala wa Ottoman.

Kösem Sultan



La Sultana: The story of Kosem




Nina imani kuwa jamii forums kuna watu wenye ushawishi ebu kidogo tujitahidi kuwasawishi hawa waongozaji na wadau wa filamu na hata Wizara husika maana tumekosa kabsa ladha na hamu ya kufuatilia filamu na tamthilia za Kitanzania.
Mtu yupo radhi anunue bando aende Net Naija kuchukua
Operation Fortune: Ruse de Guerre au Chokehold ila sio filamu ya Kitanzania.

Leteni filamu zenye utamu kama filamu hizi; Misukosuko, Nsyuka na Odama.








Naomba kuwasilisha…..
[mention]Mshana Jr [/mention] [mention]Tit 4 Tat [/mention] [mention]MalcolM XII [/mention]
 

Attachments

  • IMG_0143.jpg
    7.1 KB · Views: 9
Damaso ni furaha kubwa kukuona tena hapa jukwaani ukiwa bukheri wa afya.. Niko hapa nimefika kwa wakati.. Nitarejea...[emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Aisee sijawahi kupenda filamu za Kituruki ila Kosema ni Game of thrones ya Kituruki. Nilianza kuichungulia kiutani utani ila story yake ni bomba. THe game of politics and power. Waturuki kumbe wako vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…