Utamaduni viongozi kuwajibika umeishia wapi? Mbona Mwinyi mauaji Mwanza aliwajibika? Tusiruhusu madoa haya ya damu kuichafua nchi yetu -Wajibikeni!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo.

Viongozi wetu wawajibike kwa makosa yao.

Jumatano, Septemba 11, 2024

By Wakili Paschal Mayalla

Kitu chenye thamani kubwa duniani kuliko vyote ni uhai. Uhai wa binadamu unapokatishwa kwa umwagaji damu, hiyo ni hatia. Damu hiyo itaendelea kuwaumiza na kuwatafuna wahusika wa tukio hilo kwa kupitia kitu kinachoitwa karma.

Damu ya kiongozi huyu wa Chadema, aliyeuawa kikatili na mwili wake kutupwa Ununio, siyo tu itawagharimu waliokatisha maisha yake, bali na wengine wote wenye wajibu wa kuzuia kilichotokea, lakini hawakuzuia kwa uzembe.

Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni waumini wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, hivyo sio wengi wanajua kitu kinachoitwa karma ni nini, kwa sababu karma ni neno la lugha ya kihindi (Hindu) na linafundishwa kwenye dini ya Hinduism na Buddhism, mimi nilijifunza kuhusu karma wakati nikiishi jiji la New Delhi nchini India.

Huu ni wito kwa viongozi wetu, unapokosea hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge tabia ya kuwajibika kwa makosa yetu, au kwa uzembe wetu kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti, kabla ya kutokea majanga au maafa.

Karma ni kanuni ya binadamu kulipwa kwa kadiri ya mawazo yake, maneno yake na matendo yake, ukiwaza mema, ukasema mema, ukatenda mema, unalipwa mema. Ukiwaza uovu, ukasema uovu, ukatenda uovu, unalipwa uovu. Kwa kawaida malipo ya karma ni hapa hapa duniani na adhabu kubwa kuliko zote ya karma ni kifo cha mateso makubwa kufidia uovu wako.

Ukimtendea mtu jambo baya, hilo jambo likimuumiza, akiumia moyo, kama hukumtendea haki, wewe uliyetenda, litakufika jambo baya ambalo litakuumiza kufidia maumivu uliyomsababishia mwenzio.

Karma kwenye uongozi
Kwenye uongozi wa umma, jambo zuri na la furaha ni mtu kuteuliwa kwenye nafasi ya wadhifa wa uongozi, iwe ni kwa kuchaguliwa au kuteuliwa na kinacholeta raha ya kweli, siyo malipo ya mshahara mnono na marupurupu, bali ni ule utumishi wa umma wa kuwatumikia watu.

Ukijiuzulu mwenyewe, hata ukiumia vipi, hakuna adhabu ya karma kwa aliyekuteua, lakini ukitumbuliwa, ukiumia, kama hukutumbuliwa kwa haki, unambebesha mzigo wa karma aliyekuteua bila wewe kujijua na bila yeye kujua.

Wito kwa viongozi wote wa umma, ukiharibu, usisubiri kutumbuliwa na kumbebesha mzigo wa karma mkuu wa nchi, wajibikeni kwa kujiuzulu ili kumuepushia mizigo ya karma za uzembe wenu zisizomhusu, maana hizi karma, zinadunduliza, zikifika za kutosha kustahili adhabu.

Kwa kadiri siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika kizazi cha sasa, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni kizazi kipya cha utawala wa Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu walipofanya makosa ya wazi, sio tu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika.

Soma Pia: TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Kwa viongozi wetu wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa au makosa ya kujikwaa kisiasa, tuwaache waombe msamaha na maisha yaendelee kama kawaida au tujenge utamaduni wa viongozi wetu wanapofanya makosa, hata kupishana tu kauli na mkuu wa nchi, kuwajibika kwa makosa yao?

Uwajibikaji wa Mwinyi
Mfano mzuri wa ombi la msamaha likiandamana na uwajibikaji ni kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi kufuatia vifo vya mahabusu wakiwa mikononi mwa polisi, vilivyotokea mwaka 1976 mkoani Mwanza na Shinyanga ambapo mwaka 1977, Waziri Mwinyi aliandika barua kwa Rais Nyerere ya kuomba msamaha na kuwajibika.

Kwenye kadhia hiyo, haikuishia kwa Mwinyi pekee kujiuzulu, bali Rashidi Kawawa aliondolewa kwenye nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais, aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa alijiuzulu.

Pia, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Emelio Mzena alistaafishwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Samuel Pundugu alistaafishwa, Kamisha Mkuu wa Magereza alistaafishwa. Kisha moto huo ukahamia Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter Kisumo alimwaga unga. RPC, RSO, OCD na DSO wa Mwanza, walistaafishwa kwa manufaa ya umma.

Wakati huo, sio tu unastaafishwa na kuamua kuishi popote, bali unastaafishwa na kufuatwa usiku usiku kusafirishwa kurudishwa kijijini kwenu kwa Landrover 109 za enzi hizo na kukabidhiwa kwa serikali ya kijiji, huruhusiwi kutoka nje ya kijiji bila ruhusa.

Huu uwajibikaji wa enzi za Mwalimu umepotelea wapi? Mahabusu wangapi siku hizi wanakufa mikononi mwa polisi na hakuna uchunguzi wowote wala hatua zozote zinazochukuliwa na hakuna mtu yeyote anayewajibika?

Hitimisho
Ni lini uwajibikaji kwa viongozi wa umma utarejeshwa kwa kiwango cha uwajibikaji wa enzi za Mwalimu? Yaani kiwango cha uadilifu wa mke wa Kaisari? Kiongozi wa umma ni hadi afanye kosa kubwa kiasi gani au uzembe wa kiasi gani chini yake ndipo awajibike?

Viongozi wetu watambue kwamba cheo ni dhamana, ikitokea ukatuhumiwa tu, tuhuma za wazi, hata bila uthibitisho, ama kanusha au wajibika, msiwatwishe wengine mzigo wa karma kama mlivyomponza yule mwingine na karma ikafanya mambo yake.

Tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan asilifumbie macho jambo hili, awe mkali kama viongozi waliomtangulia. Mwinyi aliwahi kuwajibika na maofisa wa serikali walishitakiwa kwa uzembe, nini kinachokwamisha uwajibikaji wa kiwango kile?

Rais Samia asikubali kabisa kutiwa madoa ya damu na watendaji wazembe walio chini yake, asibebeshwe mizigo yao. Awe mkali kwenye hili, kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo.
Viongozi wetu wawajibike kwa makosa yao

Tawala karibia zote kabisa zilizopo Afrika huwa haziwajibiki kwa Wananchi. Udikteta is a part and parcel of all Regimes in Africa.

Ndio maana Watawala waliopo kwenye nchi zetu hizi za Afrika wana msemo wao kwamba "wa-Afrika tuna demokrasia yetu."
 
Haya yatapita na raia watasahau tu ...
 
Cha kushangaza bado mnamuomba rais afanye 123
Mnauma na kupuliza
Ndio maana hawafanyi lolote.
Hili si swala la kubembelezana na watawala
Kama inasemekana ni amri kutoka kwa wakubwa why begging hao wakubwa?
Hatupo serious
Fungueni kesi kwenye mahakama za kimataifa wahusika wamulikwe waitwe waface law period.
Mahakama za Tanganyika zimechotwa na watawala..
 
📢📌✅️
 
Kipindi cha Mwinyi ushahidi ulikuwa wazi kabisa wa polisi kuhusika na utesaji tena wakiwa na uniform watu wote waliona wazi haikuwa siri

Ushahidi wa polisi kuhusika ulikuwa wazi

Sasa hivi watu wanaongea kwa hisia wanahisi hakuna ushahidi wa wazi

Rule of law inahitaji concrete evidence kama ya kipindi cha Mwinyi

Haiwezekani viongozi wajiuzulu kwa hisia zisizo na concrete evidence itakuwa kuwaonea

Tusubiri report za vyombo vya dola kama wanahusika au la

Ni premature kuchukua mfano wa Mwinyi kujiuzulu kama precedence ya kisheria
Mleta mada you are wrong
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo.
Viongozi wetu wawajibike kwa makosa yao

Jumatano, Septemba 11, 2024
By Wakili Paschal Mayalla

Kitu chenye thamani kubwa duniani kuliko vyote ni uhai. Uhai wa binadamu unapokatishwa kwa umwagaji damu, hiyo ni hatia. Damu hiyo itaendelea kuwaumiza na kuwatafuna wahusika wa tukio hilo kwa kupitia kitu kinachoitwa karma.

Damu ya kiongozi huyu wa Chadema, aliyeuawa kikatili na mwili wake kutupwa Ununio, siyo tu itawagharimu waliokatisha maisha yake, bali na wengine wote wenye wajibu wa kuzuia kilichotokea, lakini hawakuzuia kwa uzembe.

Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni waumini wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, hivyo sio wengi wanajua kitu kinachoitwa karma ni nini, kwa sababu karma ni neno la lugha ya kihindi (Hindu) na linafundishwa kwenye dini ya Hinduism na Buddhism, mimi nilijifunza kuhusu karma wakati nikiishi jiji la New Delhi nchini India.

Huu ni wito kwa viongozi wetu, unapokosea hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge tabia ya kuwajibika kwa makosa yetu, au kwa uzembe wetu kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti, kabla ya kutokea majanga au maafa.

Karma ni kanuni ya binadamu kulipwa kwa kadiri ya mawazo yake, maneno yake na matendo yake, ukiwaza mema, ukasema mema, ukatenda mema, unalipwa mema. Ukiwaza uovu, ukasema uovu, ukatenda uovu, unalipwa uovu. Kwa kawaida malipo ya karma ni hapa hapa duniani na adhabu kubwa kuliko zote ya karma ni kifo cha mateso makubwa kufidia uovu wako.

Ukimtendea mtu jambo baya, hilo jambo likimuumiza, akiumia moyo, kama hukumtendea haki, wewe uliyetenda, litakufika jambo baya ambalo litakuumiza kufidia maumivu uliyomsababishia mwenzio.

Karma kwenye uongozi
Kwenye uongozi wa umma, jambo zuri na la furaha ni mtu kuteuliwa kwenye nafasi ya wadhifa wa uongozi, iwe ni kwa kuchaguliwa au kuteuliwa na kinacholeta raha ya kweli, siyo malipo ya mshahara mnono na marupurupu, bali ni ule utumishi wa umma wa kuwatumikia watu.

Ukijiuzulu mwenyewe, hata ukiumia vipi, hakuna adhabu ya karma kwa aliyekuteua, lakini ukitumbuliwa, ukiumia, kama hukutumbuliwa kwa haki, unambebesha mzigo wa karma aliyekuteua bila wewe kujijua na bila yeye kujua.

Wito kwa viongozi wote wa umma, ukiharibu, usisubiri kutumbuliwa na kumbebesha mzigo wa karma mkuu wa nchi, wajibikeni kwa kujiuzulu ili kumuepushia mizigo ya karma za uzembe wenu zisizomhusu, maana hizi karma, zinadunduliza, zikifika za kutosha kustahili adhabu.

Kwa kadiri siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika kizazi cha sasa, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni kizazi kipya cha utawala wa Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu walipofanya makosa ya wazi, sio tu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika.

Kwa viongozi wetu wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa au makosa ya kujikwaa kisiasa, tuwaache waombe msamaha na maisha yaendelee kama kawaida au tujenge utamaduni wa viongozi wetu wanapofanya makosa, hata kupishana tu kauli na mkuu wa nchi, kuwajibika kwa makosa yao?

Uwajibikaji wa Mwinyi
Mfano mzuri wa ombi la msamaha likiandamana na uwajibikaji ni kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi kufuatia vifo vya mahabusu wakiwa mikononi mwa polisi, vilivyotokea mwaka 1976 mkoani Mwanza na Shinyanga ambapo mwaka 1977, Waziri Mwinyi aliandika barua kwa Rais Nyerere ya kuomba msamaha na kuwajibika.

Kwenye kadhia hiyo, haikuishia kwa Mwinyi pekee kujiuzulu, bali Rashidi Kawawa aliondolewa kwenye nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais, aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa alijiuzulu.

Pia, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Emelio Mzena alistaafishwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Samuel Pundugu alistaafishwa, Kamisha Mkuu wa Magereza alistaafishwa. Kisha moto huo ukahamia Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter Kisumo alimwaga unga. RPC, RSO, OCD na DSO wa Mwanza, walistaafishwa kwa manufaa ya umma.

Wakati huo, sio tu unastaafishwa na kuamua kuishi popote, bali unastaafishwa na kufuatwa usiku usiku kusafirishwa kurudishwa kijijini kwenu kwa Landrover 109 za enzi hizo na kukabidhiwa kwa serikali ya kijiji, huruhusiwi kutoka nje ya kijiji bila ruhusa.

Huu uwajibikaji wa enzi za Mwalimu umepotelea wapi? Mahabusu wangapi siku hizi wanakufa mikononi mwa polisi na hakuna uchunguzi wowote wala hatua zozote zinazochukuliwa na hakuna mtu yeyote anayewajibika?

Hitimisho
Ni lini uwajibikaji kwa viongozi wa umma utarejeshwa kwa kiwango cha uwajibikaji wa enzi za Mwalimu? Yaani kiwango cha uadilifu wa mke wa Kaisari? Kiongozi wa umma ni hadi afanye kosa kubwa kiasi gani au uzembe wa kiasi gani chini yake ndipo awajibike?

Viongozi wetu watambue kwamba cheo ni dhamana, ikitokea ukatuhumiwa tu, tuhuma za wazi, hata bila uthibitisho, ama kanusha au wajibika, msiwatwishe wengine mzigo wa karma kama mlivyomponza yule mwingine na karma ikafanya mambo yake.

Tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan asilifumbie macho jambo hili, awe mkali kama viongozi waliomtangulia. Mwinyi aliwahi kuwajibika na maofisa wa serikali walishitakiwa kwa uzembe, nini kinachokwamisha uwajibikaji wa kiwango kile?

Rais Samia asikubali kabisa kutiwa madoa ya damu na watendaji wazembe walio chini yake, asibebeshwe mizigo yao. Awe mkali kwenye hili, kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
naheshimu sana maoni yako mwalimu Paskali, na nafurahi umeeleza kwa kirefu na kwa mifano mujarabu sana...

lakini mimi nadhani, huko ni kuhalalisha dhana ya kukimbia matizo,
na naiona imepitwa na wakati kabsaa, na wala hakuna sababu ya kung'ang'ana na mila, tamaduni na maigizo yasiyo na maana yoyote ati kwasababu tu,

eti fulani na fulani ziku za nyuma, walikimbia matatizo ya wananchi kwa kujiuzulu, na huenda ni labda baada ya kushishindwa kua na mipango madhubuti ya kuyakabili ipasavyo matatizo hayo, lakini pia huenda ni kutokana labda na uwezo wao mdogo, maradhi, kuchoka kazi n.k na watu kama hao ndio yafaa wawaachie ngazi na wengine wachukue hatamu na si vinginevo...

yaani watu kwa tofauti zao binafsi huko mtaani, siasa, madeni au wafumaniae huko mtaani waparuane vibaya, waumizane au wasababishieane vifo, halafu ambae hakuwepo kabisa na wala hahusiki na visasi vya watu hao binafsi vya kuviziana ajiuzulu kweli?

kiongozi madhubuti mwenye mipngo na dhamira ya kusimamia taasiasi kwa niaba ya umma lazima awe mstahimilivu sana na mwenye kuonyesha njia, kujizatiti kupambana na mambo magumu na kuyatafutia majawabu ya uhakikia...

amepewa kazi na dhanama hiyo muhimu na nzito, sio kwenda kucheza ngonjera, kwaya au kunywa kahawa na maziwa, halafu kukitokea tatizo zito akimbilie kujiuzulu ati sijui ndiyo aonekane bora zaidi ama nini...
unamuachia nani tatozo hilo? na ikiwa hivyo sasa si kila mtu tu likitokea tatizo zito ana kimbia? hapana hiyo si sawa hata kidogo

no hayo ni mambo ya kizamani,
kiongozi mahiri anang'ang'ana kutafuta suluhu na majawabu ya mikwamo mbalimbali mizito inayojitokeza maeneo mabalimbali nchini :pulpTRAVOLTA:
 
Nyokq wameanza kutoka shimoni sasa.

Dada yetu ana hashtag yake inasema #Tutaelewana

Kada kindaki pascal umeanza kupata akili sasa kwamba makada wenzio wajiuzulu sio, vile vingora na mabodyguard itakuwaje sasa au dereva afanya kama yale ya Nape ya kumuacha mlimani city atafute uber kurudi nyumbani.
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye gazeti la Mwananchi la leo.
Viongozi wetu wawajibike kwa makosa yao

Jumatano, Septemba 11, 2024
By Wakili Paschal Mayalla

Kitu chenye thamani kubwa duniani kuliko vyote ni uhai. Uhai wa binadamu unapokatishwa kwa umwagaji damu, hiyo ni hatia. Damu hiyo itaendelea kuwaumiza na kuwatafuna wahusika wa tukio hilo kwa kupitia kitu kinachoitwa karma.

Damu ya kiongozi huyu wa Chadema, aliyeuawa kikatili na mwili wake kutupwa Ununio, siyo tu itawagharimu waliokatisha maisha yake, bali na wengine wote wenye wajibu wa kuzuia kilichotokea, lakini hawakuzuia kwa uzembe.

Kufuatia Watanzania wengi kuwa ni waumini wa dini kuu mbili, Ukristo na Uislamu, hivyo sio wengi wanajua kitu kinachoitwa karma ni nini, kwa sababu karma ni neno la lugha ya kihindi (Hindu) na linafundishwa kwenye dini ya Hinduism na Buddhism, mimi nilijifunza kuhusu karma wakati nikiishi jiji la New Delhi nchini India.

Huu ni wito kwa viongozi wetu, unapokosea hata kwa kujikwaa tu ulimi, tujenge tabia ya kuwajibika kwa makosa yetu, au kwa uzembe wetu kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti, kabla ya kutokea majanga au maafa.

Karma ni kanuni ya binadamu kulipwa kwa kadiri ya mawazo yake, maneno yake na matendo yake, ukiwaza mema, ukasema mema, ukatenda mema, unalipwa mema. Ukiwaza uovu, ukasema uovu, ukatenda uovu, unalipwa uovu. Kwa kawaida malipo ya karma ni hapa hapa duniani na adhabu kubwa kuliko zote ya karma ni kifo cha mateso makubwa kufidia uovu wako.

Ukimtendea mtu jambo baya, hilo jambo likimuumiza, akiumia moyo, kama hukumtendea haki, wewe uliyetenda, litakufika jambo baya ambalo litakuumiza kufidia maumivu uliyomsababishia mwenzio.

Karma kwenye uongozi
Kwenye uongozi wa umma, jambo zuri na la furaha ni mtu kuteuliwa kwenye nafasi ya wadhifa wa uongozi, iwe ni kwa kuchaguliwa au kuteuliwa na kinacholeta raha ya kweli, siyo malipo ya mshahara mnono na marupurupu, bali ni ule utumishi wa umma wa kuwatumikia watu.

Ukijiuzulu mwenyewe, hata ukiumia vipi, hakuna adhabu ya karma kwa aliyekuteua, lakini ukitumbuliwa, ukiumia, kama hukutumbuliwa kwa haki, unambebesha mzigo wa karma aliyekuteua bila wewe kujijua na bila yeye kujua.

Wito kwa viongozi wote wa umma, ukiharibu, usisubiri kutumbuliwa na kumbebesha mzigo wa karma mkuu wa nchi, wajibikeni kwa kujiuzulu ili kumuepushia mizigo ya karma za uzembe wenu zisizomhusu, maana hizi karma, zinadunduliza, zikifika za kutosha kustahili adhabu.

Kwa kadiri siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika kizazi cha sasa, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni kizazi kipya cha utawala wa Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu walipofanya makosa ya wazi, sio tu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika.

Soma Pia: TANZIA - Dar: Ally Mohamed Kibao, kiongozi wa chadema auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Kwa viongozi wetu wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa au makosa ya kujikwaa kisiasa, tuwaache waombe msamaha na maisha yaendelee kama kawaida au tujenge utamaduni wa viongozi wetu wanapofanya makosa, hata kupishana tu kauli na mkuu wa nchi, kuwajibika kwa makosa yao?

Uwajibikaji wa Mwinyi
Mfano mzuri wa ombi la msamaha likiandamana na uwajibikaji ni kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi kufuatia vifo vya mahabusu wakiwa mikononi mwa polisi, vilivyotokea mwaka 1976 mkoani Mwanza na Shinyanga ambapo mwaka 1977, Waziri Mwinyi aliandika barua kwa Rais Nyerere ya kuomba msamaha na kuwajibika.

Kwenye kadhia hiyo, haikuishia kwa Mwinyi pekee kujiuzulu, bali Rashidi Kawawa aliondolewa kwenye nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais, aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa alijiuzulu.

Pia, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Emelio Mzena alistaafishwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Samuel Pundugu alistaafishwa, Kamisha Mkuu wa Magereza alistaafishwa. Kisha moto huo ukahamia Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter Kisumo alimwaga unga. RPC, RSO, OCD na DSO wa Mwanza, walistaafishwa kwa manufaa ya umma.

Wakati huo, sio tu unastaafishwa na kuamua kuishi popote, bali unastaafishwa na kufuatwa usiku usiku kusafirishwa kurudishwa kijijini kwenu kwa Landrover 109 za enzi hizo na kukabidhiwa kwa serikali ya kijiji, huruhusiwi kutoka nje ya kijiji bila ruhusa.

Huu uwajibikaji wa enzi za Mwalimu umepotelea wapi? Mahabusu wangapi siku hizi wanakufa mikononi mwa polisi na hakuna uchunguzi wowote wala hatua zozote zinazochukuliwa na hakuna mtu yeyote anayewajibika?

Hitimisho
Ni lini uwajibikaji kwa viongozi wa umma utarejeshwa kwa kiwango cha uwajibikaji wa enzi za Mwalimu? Yaani kiwango cha uadilifu wa mke wa Kaisari? Kiongozi wa umma ni hadi afanye kosa kubwa kiasi gani au uzembe wa kiasi gani chini yake ndipo awajibike?

Viongozi wetu watambue kwamba cheo ni dhamana, ikitokea ukatuhumiwa tu, tuhuma za wazi, hata bila uthibitisho, ama kanusha au wajibika, msiwatwishe wengine mzigo wa karma kama mlivyomponza yule mwingine na karma ikafanya mambo yake.

Tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan asilifumbie macho jambo hili, awe mkali kama viongozi waliomtangulia. Mwinyi aliwahi kuwajibika na maofisa wa serikali walishitakiwa kwa uzembe, nini kinachokwamisha uwajibikaji wa kiwango kile?

Rais Samia asikubali kabisa kutiwa madoa ya damu na watendaji wazembe walio chini yake, asibebeshwe mizigo yao. Awe mkali kwenye hili, kila mtu aubebe mzigo wake mwenyewe.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Navuta picha ya maana halisi ya washika tonge vs washikatonge wanaopewa dhamana Afrika, (Tanzania), walivyo na ujuzi wa kujizima data, yaani kuahirisha kufikiri kizalendo
 
CCM ya Leo sionile ya zamani.
Ccm ya Leo wizi na ufisadi vimehalalishwa.
CCM ya Leo kuuawa, kuteka na kutesa ni sera wanazozinadi hadharani.
CCM ni chama dhalimu.
Chama cha mashetani hiki.
Chanzo Cha Matatizo yote nchini nibhiki chama na mifumo dhalimu kinayoijenga
 
Back
Top Bottom