SoC04 Utamaduni wa nchi yoyote duniani ni kiini kikuu cha maendeleo vinginevyo watu wengi watakuwa mateka wa kiutamaduni

SoC04 Utamaduni wa nchi yoyote duniani ni kiini kikuu cha maendeleo vinginevyo watu wengi watakuwa mateka wa kiutamaduni

Tanzania Tuitakayo competition threads

PAN AFRICANIST JR

New Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Serikali kwa kushirikiana na sisi wananchi, kudumisha na kurejesha hadhi ya tamaduni za kitanzania na Afrika kwa ujumla, ili kuwaoko watu kutoka mateka wa kiutamaduni.

Tanzania tuitakayo baada ya miaka 20.

SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA SISI WANANCHI KUDUMISHA,NA KUREJESHA HADHI YA TAMADUNI ZA KITANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA.

Maendeleo bila utamaduni ni sawa na kukausha nguo kwa kutumia maji ya moto, Tanzania yangu ya leo wananchi wake wameacha kabisa tamaduni zao, ambazo ni muhimu sana katika maendeleo ya jamii, itakuwa ngumu sana kuipata Tanzania ya kesho, kama tamaduni zetu tutaziacha zipukutike kesho. Mtanzania atambululika kwa lipi,kama wananchi wenyewe hawaelewi walikotoka, Tanzania inapoteza utamaduni wake, wakati wananchi wapo bize na tamaduni za watu.

MADHARA YAKE

Kutozingatiwa kwa tamaduni za kitanzania kumepelekea kuongezeka kwa mateka wa kiutamaduni, mmomonyoko wa maadili Kila Kona ya nchi malezi, watoto hawalelewi katika maadili ya kitanzania, mtoto anakulia maziwa waziwa ya kisasa na mama yake yupo!, Nguo wanazovaa wazazi na watoto ni robo sketi , lugha chafu nk na watoto wamefuata humo humo kwa sababu wamelelewa maisha ya kisasa.

Kuna kizazi kinakuja miaka ijayo, kizazi hiki naweza kukiita kizazi cha (DAY CARE) hiki kitakuwa kizazi hatari sana katika maadili ya nchi yetu kwa sabau siku hizi wazazi wanapeleka watoto day care wakiwa wadogo bado wanahitaji uangalizi wa wazazi, kwa kisingizio cha majukumu, najiuliza mbona wazazi wetu sisi walitulea vyema na majukumu walifanya. Vilevile ni majukumu gani yameongezeka kiasi cha mtu kushindwa kukaa na watoto wake? Mtu anatoka asubuhi ana mpeleka mtoto day care anamchukua jioni na tunategemea Tanzania yenye maendeleo kesho hii itakuwa ndoto.

Kutozingatia tamaduni na mila zetu kumeathiri hadi familia, siku hizi ndoa zimekuwa kama status za wahatsapp zinadumu ndani ya masaa 24 na kuyeyuka, ni kwa sababu watu hawajui tamaduni na taratibu zao, watu wanakutana kwenye bajaji, safari ya dakika kumi wameshakubaliana hadi siku ya ndoa hii si utamaduni wetu sisi watanzania kuna taratibu za kufuata kulingana na kabila husika, mahari yenyewe inalipwa kwa mpesa,tigo pesa,airtel money au halopesa wazazi hawamjui hata anaeishi na mtoto wao. Hivyo kutokana na msingi mibovu ya familia, pia tutegemee jamii yenye misingi mibovu.

MAPENDEKEZO YANGU

Kwanza, ili kutengeneza Tanzania tuitakayo yatupasa kushinda vita vya kiutamaduni, katika karne hii kuna vita vinapiganwa, ni vile tu vita hii haihusishi silaha za moto wengi hawajui, kuna vita ya kiutamaduni kila taifa linaeneza tamaduni zake na uwanja wa vita hii ni utandawazi, ni kweli hatuwezi kujitenga na utandawazi bali yatupasa kuchukua mazuri na kuacha mambo ambayo yanaangamiza tamaduni zetu maana kufurahia utandawazi na kusahau tamaduni zetu ni sawa na golikipa kwenda kushambulia na kusahau goli, ndugu zangu kabla hatujapigiwa (counter attack) turudieni tamaduni zetu. kama tunaitaka Tanzania tuitakayo, tuanze kwa kupenda tamaduni zetu ili tushinde vita hii.

Serikali iweke utaratibu wa kufundisha mila na tamaduni kwa vitendo kama ilivyo kwa masomo ya sayansi, kwa kuzingatia tamaduni za eneo husika. Ni kweli serikali imeanzisha hili somo la historia na maadili ya Tanzania, niipongeze serikali kwa hatua hii, lakini nashauri nadhalia pekee haitoshi, kuwe na vipindi vya vitendo(practical) kama ilivyo kwa masomo ya sayansi na walimu wa hivi vitendo watafutwe wazee wa tamaduni husika (wabobezi) wapewe nafasi na wapewe posho na serikali hii itasaidia kuandaa vijana wenye maadili na misingi ya taifa letu ili kuiendeleza Tanzania.

Pia mfumo wa elimu ya Tanzania uendane na mahitaji ya tamaduni za kitanzania ili wasomi wa nchi hii waitumikie Tanzania tofauti na tunavyoenda Sasa hivi mfumo unatengeza vijana tegemezi kuliko jamii kutegemea wasomi ni kwa sababu vijana hawamjui kuwa hata utamaduni wako waweza kuwa fursa ya ajira na si lazma ajira itoke serikalini hivyo serikali iwafanye vijana wajitegemee.

Serikali kwa kushirikiana na wazazi/walezi na jamii kwa ujumla kuwa na ushirikiano wa karibu katika malezi ya mtoto kwa hali ilivyo sasa katika Tanzania yetu, ushirikiano wa malezi ya watoto kati ya wazazi,serikali na jamii upo kwa kiasi ukilinganiasha na miaka 20 iliyopita sikuhizi jirani hatakiwi kutoa adhabu kwa mtoto ambaye anaende kinyume na maadili , kuna ile kauli ya mtoto wa jirani ni wako haipo tena, ni kwa sababu ya usasa, mtoto akionekana analia tu tayari mtu anaitwa kuhojiwa na mamlaka kwa tuhuma za unyanyasaji wa watoto. Hivyo serikali iangalie suala hili kama Sheria zirekebishwe mtoto awe wa jamii nzima, kuwe na mabaraza ya wazazi yaliyo hai katika kila kijiji kwa maana kuna wazazi wapo bize na uzalishaji na wamesahau kulea, vuta picha mtu anaamka asubuhi sa kumi na moja watoto wamelala anarudi saa nne watoto wamelala na ni baba au mama wa familia, watoto wake atawafunza saa ngapi ndo maana sishangai mtoto kumwita baba yake mjomba, kwa kufanya hivyo kizazi cha Tanzania tuitakayo kitakuwa vyema sana.

Mwisho

Utamaduni imara unatengeneza familia yenye nguvu, familia nyingi zenye nguvu kimaadili , zinaunda jamii yenye nguvu kimaadili, jamii zenye utamaduni wenye nguvu zinatengeneza taifa lenye nguvu kimaadili na hatimaye watu wenye maadili watajenga uchumi imara na maendeleo ya taifa. Ombi langu serikari ifanyie kazi mapendekezo inayoona yanafaa. Pia shukrani kwa jamii forums kwa kuwa sehemu nzuri ya sisi tusio na sehemu ya kutolea maoni ya kujenga taifa tulitakalo.

by PAN AFRICANIST JR

Email.paulluteng20@gmail.com
 
Upvote 5
Back
Top Bottom