Utambulisho - Mnozya

Utambulisho - Mnozya

mnozya

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2009
Posts
213
Reaction score
56
Natumaini nyote ni wazima na mnaendelea vema na kazi za ujenzi wa Tanzania. Mimi naitwa S. H. Mnozya, nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu contributions, ideas, analysis and comments za JF. Kimsingi zimekuwa zikinipa changamoto na ninawapongeza kwa kazi nzuri.

Hata hivyo nia na lengo ni kujenga, ili kujenga hatuna budi kujitazama visogoni na kama mmoja wetu hajachana nywele vizuri basi tusisite kumwambie achane. Naamini kuwa ili JF izidi kujijengea heshma na kuthibitisha pasina shaka kuwa ni jamii ya watu mahiri katika kufikiri hatuna budi kuongeza ufanisi katika uchambuzi wa kisayansi.

Nahitimisha kwa kurudia kuwapongeza wanajamii forum wote kwa kazi nzuri.
 
Karibu sana kwenye JAMVI ndugu Monzya.......!

Selous......can you give more details re. kuwasiliana na Ngd Melo?
 
Karibu sana Mheshimiwa Mnozya, na ujisikie uko nyumbani. Tunasubiri kwa hamu kukuona ukijimwaya mwaya ndani ya JF, manake kweli hatujui kama kisogoni nywele zimechanwa ama la.
 
Karibu sana Mnozya!
Tupate michango yako kimawazo katika masuala mbali mbali.
 
Karibu sana kwenye JAMVI ndugu Monzya.......!

Selous......can you give more details re. kuwasiliana na Ngd Melo?

Nadhani katika kumhamasisha Mnozya aiwezeshe JF kwa mchango wa hiari ili JF iweze kuwa bora zaidi.....Karibu Mazeee!!
 
Karibu sana Mkuu Mnozya jamvini kwetu. Jisikie upo nyumbani na mawazo yako yanakaribishwa sana popote pale ambapo unaweza kuchangia.
 
Asante qwa qututembelea na jysyqye uqo nyumbany.

SAHYBA.
 
Karibu mzee..wengine tunaingiaga kimya kimya, na hapa huna haja ya kutaja jina lako halisi.

Humu tufanya party kimya kimya......
 
Mnozya wewe ulikuwa silent member ila leo umejiandikisha rasmi baada ya kugundua kuwa JF siyo jukwaa la wababaishaji.Uje basi ukiwa umechana nywele zako!!!
 
Karibu mpaka uani mkuu.

Lakini siku mbli tatu hizi hakuna issues za siasa kwa hiyo tumekalia kuongelea vitu visivyo na mwelekeo, unaweza kwenda kwenye thread ya Jaji Kiongozi ukaona jinsi JF inavyokuwa live hata kama hakuna hoja ya msingi kwenye thread hiyo.

Vilevile tupo sisi washabiki na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa, CHADEMA tumejaa sana kazi yetu kumchafua kila anayekatiza upande wa CCM
Na sisi wa CCM hatuko wengi sana lakini tumetulia tunakula vyetu kiulaini.
Sisi wa CUF bado hatujajua tutoke vipi, lakini nia yetu si siasa za bara sisi CUF tunataka Zanzibar na tukiikosa 2010 tunaingia baharini na kuichukua Pemba kutoka SMZ na JMT.

Kuna burudani inaendelea pale kwenye thread ya Kelly01 unaweza kwenda ukaburudika, kelly01 ni mbunifu wa kiaina inaelekea ni mtu wa jokes, lakini kuwa mwangalifu ana cupcake wake humu ndani.

Mwisho, usishangae kuona kuwa kuna watu wanapinga kila kitu hata majina yao yakitajwa humu ndani wanayapinga kuwa si yao.

Kwa mara nyingine tena karibu hadi uani
 
Ushauri wangu kwako ni kuwa hoja zako ziweke maslahi ya taifa mbele, itakadi yako ya siasa, dini, kabila, rangi yako viweke kapuni. Lakini ukumbuke kuwa JF ni reflection ya Tanzania halisi, kuna mafisadi hapa na wazalendo, wenye akili na mambumbumbu. Lakini uzuri ni kuwa sote tunaelimishana kuhusu namna ye kuifanya Tanzania yetu isonge mbele.
 
Asante qwa qututembelea na jysyqye uqo nyumbany.

SAHYBA.
Mmh! Mkuu SAHYBA, Kumbe Kiswahili kina namna nyingi ya kuandika, sikujua! Hiki ndo umekipeleka shule, ama?
Mh. Mnozya, karibu sana japo si mpaka uani - maana majukwaa mengine hadi upate kibali kutoka kwa Wakulu. All in all, huwezi kujuta kujiunga na JF. Siye mambumbumbu tunaelimikia humu humu. Raha tupu!
 
Last edited:


Mwisho, usishangae kuona kuwa kuna watu wanapinga kila kitu hata majina yao yakitajwa humu ndani wanayapinga kuwa si yao.



Hasa hasa Yo Yo na Nyani Ngabu, hawa jamaa wabishi sana sijui walizaliwa siku ya j.nne?
 
Hasa hasa Yo Yo na Nyani Ngabu, hawa jamaa wabishi sana sijui walizaliwa siku ya j.nne?
Sifa moja kuu ya JF ni kukubali kutokubaliana.......
...Mnozya karibu......unaweza ukataja jinsia but sio lazima saaana mkuu mbele kwa mbele....
 
Karibu ndugu, ninakuomba weka maslahi ya taifa mbele. Hata kama ni baba yako anapigwa makombora, radi au umeme hapa ndani ya forum ni vema ukawatetea watanzania wenye uzalendo. Kwa mantiki tuungane pamoja kumkoma nyani gilabu mafisadi na wala rushwa maana ndiyo wameifikisha Tanzania hapa ilipo "inayumba sasa". Karibu dada/kaka.
 
Makobota jamani.Naombeni mnipokee.Nina uchungu na nchi yangu.Kuna mwana jf ameniambia nipitie mlango huu,jina sijalikariri.Mimi nitachangia mada kwa umakini wa hali ya juu.Ninaona mbali kisiasa na mambo yajayo kwa jamii ya watanzania,n.k.HODI JAMANI!!
 
Back
Top Bottom