Utambulisho wa Jezi kwa timu za VPL.

Utambulisho wa Jezi kwa timu za VPL.

0909Hekima

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2013
Posts
226
Reaction score
65
Habari wana jamvi.

Baada ya kufuatilia kwa undani na kugundua hili, nimeona nilete kwenu tuliongee kwa pamoja.

Bila shaka wengi wetu tumeona jinsi mdhamini mkuu wa ligi ( Vodacom ) alivyo tambulisha jezi za timu tofauti zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom.

Ila ukakasi wangu ni pale unapotambulisha jezi zote kwa siku moja, tena anayetambulisha jezi si timu husika bali ni mdhamini. Achilia mbali hilo na bado aliyetambulisha jezi hizo na kuzivaa tumekosa kuwaona wachezaji, wakatafutwa watu wakavalishwa na kutembea mbele ya vyombo vya habari kuzitambulisha jezi hizo.

Wapi tunaenda??? Naomba wakuu em tuliangalie hili jambo kwa kina, kama wahusika wapo tuwape njia sahihi za masuala ya utambulisho wa jezi za timu na nini kifanyike kuongeza ubora wa ligi pamoja na ushindani hasa katika ubunifu wa jezi, maana jezi zimetofautiana rangi tu, ila muuondo kwa asilimia 80% zinafanana.

Karibuni.​
 
Hivi inakuaje BARCLAYS BANK ( mdhamini wa EPL ) siku akaamua kukusanya jezi ya Man U, Arsenal, Man C, Chelsea, Spurs, Liverpool, Swansea na nyinginezo na kuamua kuzitambulisha! Huu mpira wa Tanzania tunauangaliaje ktk masuala kama haya???
 
Back
Top Bottom