Tangu tupate uhuru yapo mambo mengi ambayo yamefanywa na viongozi wa taifa letu, mambo hayo yalifanywa ili kuliwezesha taifa letu kuimarika kiuchumi na hatimaye kuweza kuendesha shughuli mbalimbali ndani ya taifa letu bila kuteteleka. Kwa kuwa na malengo kama hayo viongozi wa taifa letu waliyaweka malengo mbalimbali ikiwa ni yale ya muda mfupi na yale ya muda mrefu kwa lengo tu la kuimarisha uchumi wa Taifa letu.
Mpaka sasa tumepiga hatua kubwa sana lakini bado tunahitaji kufanya zaidi. Kila nchi duniani inahitaji kuwa bora zaidi ya mwenzake, hata sisi nasi kama Taifa tunahitaji kufanya vizuri zaidi ya nchi nyingine ili kuweza kuwa kinara na kutegemewa na mataifa mengine. Kwa pamoja tumelifanya taifa hili kuwa na amani na utulivu, hata hivyo amani tuliyonayo inatosha kabisa kuweka mikakati mingine zaidi ya kuimarisha uchumi wa taifa letu na hatimaye kuwa kinara barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Taifa letu limekuwa ni muhanga wa matatizo ya nchi nyingine, matatizo yao yamelitesa bara la Afrika na Taifa letu, kwa mfano majanga ya asili kama vile mlipuko wa magonjwa, vita vya Urusi na Ukraine, Izraeli na Parestina, vimelitesa taifa letu katika suala la mafuta nakupelekea kupanda kwa bei ya mafuta nchini kwetu na hatimaye kupanda gharama za bidhaa nyingine zilizopelekea kutokea kwa ugumu wa maisha kwa watanzania wote.
Nchi nyingi zilioendelea duniani zina utambulisho wa pekee unaoitambulisha nchi hizo na kuzitofautisha na mataifa mengine, kwa mfano nchi ya Libya iltambulika vizuri kutokana nakufanya vizuri kwenye sekta ya uchimbaji wa mafuta, nchi ya Iraq nayo ilitambulika vizuri kutokana na uchimbaji wa mafuta, ufaransa inatambulika kwa kufanya vizuri katika utalii, Ethiopia inatambulika kwa kufanya vizuri katika usafiri wa anga, unaweza usiitaje marekani lakini dollar inaitambulisha vizuri nchi ya marekani lakini je! umeshawahi kujiuliza taifa letu linatambulishwa na nini kiuchumi?
Hivyo pamoja na kufanya vizuri kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi ni lazima tuchague sekta moja wapo ya kuifanya kuwa kinara ili kupitia sekta hiyo tuweze kuimarisha uchumi wa taifa letu kwa kutuongezea mapato na hatimaye kuimarisha sekta zinginezo na kuifanya Tanzania kuwa kinara kiuchumi. Tanzania tuna eneo kubwa lenye raslimali nyingi sana ambazo tukiamua kuchangua mojawapo ya kuifanyia kazi vizuri zaidi ndani ya miaka mitano au kumi ijayo, hakika tutaipata Tanzania tuitakayo.
Katika taifa letu zipo sekta nyingi zinazoweza kuimarishwa na hatimaye kuwa utambulisho wa taifa letu lakini msingi mkubwa ni kuanza na moja na kutoruhusu sekta hiyo kuanguka kiuchumi, na baadhi ya sekta hizo ni kama sekta za kilimo na ufugaji, uvuvi, sekta ya utalii, sekta ya madini na sekta ya usafirishaji.
Sekta tajwa hapo juu ni mfano tu kwani tukiamua kutumia sekta mojawapo kati ya hizo ni dhahiri kwamba inaweza kuwa mkombozi wa kuimarisha uchumi wetu na hatimaye kuitambulisha nchi yetu ndani ya bara la Afrika na nje ya Afrika yetu. Zaidi sana ili kuhakikisha hilo linafanikiwa ni mhimu sekta tajwa inatengwa na kuwezeshwa ili kuweza kujitangaza sokoni.
Lazima tuanze kwa kuifanya sekta moja kuwa kinara na ili kuweza kuifanya ifanye vizuri zaidi kuna umhimu wa sekta hiyo kuendelezwa na serikali badala ya kusubiri wawekezaji ambao nao wakitokea huja na masharti yao ambayo kiuhalisia hayawezi kuifanya sekta hiyo kufanya vizuri zaidi, jaribu kuwaza mfano mzuri sisi tunazalisha gesi asilia lakini kwa uhalisia gesi hiyo haijakata kiu ya watanzania kwani bei yake ipo juu sana ukilinganisha na kipato cha watanzania. Ni mhimu kufahamu kwamba kiu ya watanzania ni kuona tunamaliza matatizo yetu ndani ya taifa letu lakini huwezi kumaliza matatizo yote ndani ya siku moja au kuyamaliza matatizo yote kwa pamoja ni lazima tuwe na mahala pa kuanzia ili kukomboa maeneo mengine na mahala penyewe ni kuchagua sekta mojawapo na kuifanya kinara ili iweze kutoa huduma bora kwa watanzania huku ikiendelea kuipatia mapato nchi yetu.
Kuna wakati itatubidi tuzitenge sekta zetu ili ziwepo sekta zitakazotoa kipaumbele katika kuhudumia wananchi na kuzitoa katika mfumo wa kikodi ili kumnufaisha mwananchi wa chini mfano mzuri ni kama sekta ya nishati, ukihitaji wananchi watumie gesi asilia badala ya kutumia kuni na mkaa ni lazima uhakikishe gesi inayozalishwa nchini kwetu inaondolewa kodi kwa watumiaji ambao ndio watanzania wenyewe ili waweze kuinunua kwa bei nafuu na kodi zinaweza kuendelea kwenye sekta nyinginezo na kwa kuufanya hivyo kupitia sekta hiyo inaweza kuwasaidia wananchi kupata nishati safi ya kupikia huku wakiyalinda mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hivyo kuna umhimu mkubwa sana wa kuhakikisha tunakuwa na sekta inayokuwa kinara ndani ya nchi kwa kutoa huduma bora lakini pia kuwa sekta kinara inayoweza kuitambulisha taifa kutoka mataifa mengine ili kuwa ya mfano na kupitia sekta hiyo kuweza kuinua sekta nyingine na kutumika katika kuleta maendeleo ya taifa letu na kupitia sekta hiyo inaweza kusaidia kutuletea Tanzania tuitakayo ndani ya miaka kumi ijayo.

Upvote
4