Pre GE2025 Utamchagua mgombea mwenye sifa zipi aje kuwa kiongozi wako?

Pre GE2025 Utamchagua mgombea mwenye sifa zipi aje kuwa kiongozi wako?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu, hiki ndio kipindi cha kufanya tafakari za sifa za mgombea anayefaa na asiyefaa kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Wakati wa kampeni ukianza ukiwasikiliza wagombea wote itakuwa rahisi kwako kumjua unayemtaka kwa kuwa tayari ulishaainisha sifa zake mapema hivyo itakurahisishia kufanya maamuzi sahihi.

Kwa upande wangu mimi nitamchagua mgombea mwenye sera zinazotekelezeka, mwenye kutoa ahadi na njia atakayotumia kuzitekeleza.

Mgombea yoyote ambaye hataonesha chembe chembe za kutaka kuchaguliwa kwa kutoa rushwa ya aina yoyote.

Mgombea yoyote asiyenishawishi kwa vifurushi vya zawadi na asiyeeneza sera za kugawa makundi ya watu, iwe kidini, ukabilank

Kama anarudia kugombea asiye na rekodi ya kutotimiza wajibu wake wakati alichaguliwa awali.

Je, kwa upande wako mgombea mwenye sifa zipi anafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi wako?
 
Back
Top Bottom