Utamjuaje mtu mwenye ugonjwa wa akili au tatizo la kisaikolojia, sio lazima kuchanganyikiwa

Joined
Nov 3, 2014
Posts
38
Reaction score
10
AFYA YA AKILI

Ni mjumuiko wa hali ya mtu kuwa vizuri kihisia, kisaikolojia na kijamii. Hii inahusisha jinsi ambavyo mtu anafikiria, anavyohisi,na jisi anavyotenda/kufanya mambo yake. Inamaanisha kua, Kunapokua na tatizo kwenye afya ya akili ndipo mtu anakua na tatizo katika hisia, mawazo, mtazamo, na/ au matendo.

UTAMJUAJE MTU MWENYE TATIZO LA AFYA YA AKILI (UGONJWA WA AKILI, TATIZO LA KISAIKOLOJIA? (VIASHIRIA)

Anaweza kua na dalili mojawapo au zaidi kati ya hizi zifuatazo na zinamfanya ashindwe kufanya mambo yake vizuri.

1. Anakua na hali ya kua na huzuni iliyopitiliza, analia mwenyewe, hana raha n.k Anakuwa na mawazo hasi kama vile ya kukata tama, kujiona mwenye hatia, kuwaza vitu negative muda wote, na hata kuwaza kutaka kujiua


2. Anakua na kuogopa au mtu anakua na hofu kupita kiasi. Anaweza kuwa na wasiwasi wa kila kitu..ye anaogopa tu, simu ikiita tu hofu tayari..ukigonga meza ..ye presha juu…mwingine , anaweza kuogopa kuongea mbele ya watu, kusafiri na ndege au majini, n.k mapigo ya moyo huweza kwenda mbio, misuli kukakamaa, kushindwa kuhema vizuri, kupanic n.k

3. Kuwa na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, maumivu yasiyoelezeka, yanaweza kua yanahama toka sehemu moja hadi nyingine, na akienda hospitali vipimo vinaonyesha hana tatizo lolote. Wengine huweza pia kupoteza uwezo wa kuona au kutembea ghafla tu.

4. Anakua na hali ya hofu na kukumbuka matukio ya zamani yaliyomuumiza bila kutaka kuyafikiria kama vile (ajali, kubakwa, kufiwa, kutendwa , vitani, kuvamia na wezi, n.k) , anaota ndoto za kutisha, anaumwa kichwa, anaweza kua anazimia, mapigo ya moyo kwenda mbio, kukosa utulivu n.k

5. Kuzimia, kusahau kusikoelezeka mfano mtu anaweza kununua vitu halafu akasahau kama ni yeye amenunua, au akaenda mahali akapasahau kabisa wakati anapajua kila siku, kujikuta sehemu halafu hajui amefikaje, na kuongea sauti tofauti tofauti (mfano mwanamke anaweza kuongea sauti ya kiume n.k (wengine tunasema wanapandisha mashetani..Shhhhhhhhh…yawezekana ni tatizo la kisaikolojia au ugonjwa wa akili..mpeleke hospital)

6. Kuona vitu ambavyo watu wengine hawavioni au kusikia sauti ambazo watu wengine hawazisikii, kuamini vitu ambavyo sio vya kawaida mfano kuamini kuwa yeye ni mungu, yesu, mtume, mtu maarufu n.k kuhisi ana kipaji maalumu na kua na nguvu za ajabu

7. pia mtu anaweza kuonyesha dalili nyingine zisizoendana na jamii kama vile ukatili ulopitiliza (mfano unyanyasaji wa watoto), hasira zisizozuilika, matumizi ya madawa ya kulevya au ulevi kupita kiasi

8. Kujikata (hasa mkononi) kula kucha, kuwa na mood sana, dakika mbili kashakasirika, sekunde tatu anacheka …punde kanuna…ilimradi shida, kutishia kujiua …..auuchhhhh

9. Hupata shida ya kukosa usingizi, kusahau kulikopitiliza na kushindwa kutulia, kukosa hamu ya kula au kula sana n.k
Lastly,,,,,but not least kujiacha mchafu, kutojitunza na kufanya mambo yasiyoeleweka

Kwa hiyo basi, afya ya akili kwa ujumla ni hali ya kuwa vizuri kihisia, kisaikolojia na kijamii inayomuwezesha mtu kuujua uwezo wake, kukabiliana na msongo wa mawazo au stress za maisha na kuweza kutoa mchango chanya kwenye jamii yake.

Ushauri: kama ndugu yako au wewe una dalili mojawapo kati ya hizo, kabla hujawaza kulogwa, kabla hujafikiria laana na mambo mengine, hebu mtafute mtaalamu wa afya na magonjwa ya akili…

Kwa habari zaidi kuhusu saikolojia, afya, mahusiano, matatizo ya afya ya akili nay a kisaikolojia , matatizo ya tabia kwa watoto , Kwa maoni, msaada au ushauri

USISAHAU KUTUFOLLOW INSTAGRAM: @ psychological_support_tz
LIKE PAGE YETU FACEBOOK : https://www.facebook.com/pages/Psychological-Support-and-Mental-health-Awareness/159663587434912
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…