SoC02 Utandawazi una neema jamii ineemeke lakini pia una adha jamii ijihadhari

SoC02 Utandawazi una neema jamii ineemeke lakini pia una adha jamii ijihadhari

Stories of Change - 2022 Competition

Mbaga Lazaro

Senior Member
Joined
Aug 9, 2020
Posts
132
Reaction score
108
Utandawazi unaweza kufafanuliwa kuwa ni kuongezeka kwa uhusiano na kutegemeana kwa watu na nchi. Kwa ujumla hujumuisha vipengele viwili vinavyohusiana kufunguliwa kwa mipaka ya kimataifa na mtiririko wa haraka wa bidhaa, fedha, huduma, watu mawazo nK.

utandawazi umekuwa mfumo wa dunia nzima kwa sababu unaunganisha watu kuvuka mipaka yao ya kitaifa, na kuifanya dunia kufanya kazi kama kijiji na hivyo kufanya watu, bidhaa, mitaji na taarifa kusafiri huru. .mchakato wa utandawazi unachangiwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya haraka katika biashara ya ukuaji wa teknolojia na ushindani.

Asili ya kihistoria ya utandawazi
.muunganiko wa dunia na kutegemeana kati ya vipengele vyake tofauti vya kijamii, kisiasa na kiuchumi ulianza zamani sana wakati wa kipindi cha biashara cha Ulaya (15000-1750) na umeendelea hadi leo.

.katika kipindi cha biashara, wafanyabiashara wa Ulaya walivuka mipaka yao na kufanya biashara katika sehemu nyingine za dunia kama vile Afrika, Asia na Amerika Kusini.

.tukio la biashara ya utumwa na usafirishaji wa Waafrika kutoka bara lao hadi mabara mengine, haswa Amerika, iliyounganishwa na Afrika zaidi na zaidi na nje ya Ulimwengu. Shughuli zote hizi zilikuwa maonyesho ya utandawazi wakati huo.

Kwa ujumla utandawazi umeweza kuwa na mchango chanya katika jamii hasa kwa upande wa maendekeo ya sayansi na teknolojia ambayo yanachagiza maendekeo katika nyanja za kiuchumi, kisasa, kiutamaduni nk. Pia zipo athari hasi ambazo zimesababishwa na maendekeo haya. Lengo la makala hii ni kuangazia upande chanya wa utandawazi ili jamii iweze kutumia Kama fursa pia kuuona upande hasi ili jamii ijihadhari.

Kwa kuanza na upande (+)Faida za utandawazi zipo nyingi na baadhi yake ni Kama zifuatazo.
Teknolojia ya hali ya juu.Teknolojia ya Hali ya juu ni matokeo ya utandawazi. Wavumbuzi wengi wamejaribu kuhudumia mahitaji ya jamii ya kisasa kwa kuboresha teknolojia. Maendeleo haya yamefungua njia kwa athari chanya hasa katika harakati za kujikwamua kiuchumi na kuimarisha ulinzi.

Kutokomeza umaskini. Kabla ya utandawazi nchi zinazoendelea zilikuwa na rasilimali nyingi ambazo hazikujua namna ya kuzitumia.Watu katika nchi hizi hawakuwa na elimu na vilevile hapakuwa na barabara zenye viwango na vyombo bora,imara na vyakutosha vya usafiri. Siku hizi watu wameelewa umuhimu wa elimu na hata kuweza kusafiri nje ya nchi kuisaka elimu mwisho wa siku wameweza kutumia elimu hiyo kujinasua katika lindi la umaskini.

Vile vile kutokana na utandawazi makampuni yameweza kuanzishwa na wenyeji na mengine pia yameweza kuanzishwa na wageni yameweza kushindana kibiashara jambo ambalo kwa namna moja au nyingine limeweza kuinua maisha ya mtu mmoja mmoja (kupitia ajira zitolewazo) na pia kuinua pato la taifa (kupitia Kodi)

Vile vile upanuzi wa taasisi kuu za kidini za ulimwengu hasa katika Afrika na Asia umebadilisha tunu zao za kijamii na kitamaduni kuwa za kisasa na zinazokubalika. .nchini Tanzania kwa mfano kuenea kwa Ukristo na Uislamu karibu kila sehemu ya nchi kumekuwa na mchango mkubwa katika kutokomeza mila na desturi zisizokubalika kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni,unyanyasaji wa wanawake n.kutandawazi umeboresha utoaji wa huduma za kijamii.

Huduma za kijamii kama vile elimu, afya, mawasiliano zimeboreshwa. Kwa mfano elimu imeboreshwa kutokana na uwepo wa vitu kama vile kujifunza umbali kutokana na matumizi ya mtandao, video n.k

Utandawazi umefichua baadhi ya tamaduni mbaya ambazo zimefanywa na baadhi ya jamii. .kwa mfano, suala la ukeketaji ambalo sasa linalaaniwa kimataifa kwa msisitizo mkubwa na mashirika mbalimbali ya kimataifa.Tumekuwa tukishuhudia tamaduni Kama hizi zisizofaa zikiibuliwa kupitia vyombo vya habari na hata mitandao ya kijamii mwisho wa siku jamii huweza kuona na kuweza kufanya jitihada za kudhibiti na kutokomeza tamaduni hizo.

Upatikanaji wa masoko mapya.
Biashara hupata faida kutokana na utandawazi .Ikiwa ni pamoja na wateja wapya na njia mbalimbali za kuongeza mapato.Makampuni yanayovutiwa na manufaa haya huongeza ubunifu namna ya kukuza biashara zao.

Kuenea kwa teknolojia ya ubunifu.Nchi nyingi duniani hushikamana kila mara hivyo ujuzi na maendekeo ya kiteknolojia husafiri haraka kwa sababu maarifa pia husafirishwa haraka Sana.

Hii ina maana kwamba maendekeo ya sayansi na teknolojia yanayoweza kufanya kazi ulaya yanawezakufanya kazi barani Afrika baada ya Siku chache vile vile maendekeo ya sayansi na teknolojia yanayofanya kazi Afrika huweza kufanya kazi ulaya baada ya Siku chache.

Upatikanaji wa tamaduni mpya. Utandawazi hurahisisha kupata utamaduni wa kigeni ikiwa ni pamoja na vyakula ,Sanaa, sinema na muziki. Licha ya athari chanya ambazo zimetokana na utandawazi pia zipo athari hasi(-) ambazo zimekuwa zikishuhudiwa kila uchao.

Miongoni mwa (athari) changamoto hizo ni pamoja na;
Kuongezeka kwa magonjwa hasa yatokanayo mtindo wa maisha. Utandawazi umepelekea magonjwa kuongezea katika jamii hasa magonjwa yatokanayo na mtindo wa maisha. Kwa mfano utandawazi umeleta matumizi ya vyakula vilivyosindikwa, kupanda mazao kwa kutumia kemilali ili kupunguza muda wa ukuaji na kuongeza faida.

Pia ili kufaidika na biashara wanyama mfano Ng’ombe hulishwa kwa kemilali zinazowafanya watoe maziwa mengi na kuongezea uzito kwa wale wanaouzwa hivyo kupelekea uwezekano wa kuongezeka kwa idadi ya vifo . Pia matumizi ya kemilali hizi hupelekea hata kupungua kwa muda wa maisha kwa nchi hasa kwa nchi zinazoendelea.

Nikitumia uzoefu kutoka mazingira ninayoishi jamii hii inajitahidi sana kwa upande wa kilimo lakini matumizi ya kemilali yamekithiri fikiria zao Kama kabichi ,nyanya nk hupigwa dawa mpaka dakika za mwisho kuelekea sokoni jambo linalonipa wasiwasi kuhusu usalama wake licha ya kupata mavuno mazuri yatokanayo na matumizi ya kemilali hizi.

Kuacha tamaduni hasa zile zilizo nzuri.

Kila jamii au taifa lina maadili na imani zake.Tamaduni hasa zilizo nzuri ni muhimu kwani hufinyanga tabia inayokubalika ya watu katika jamii fulani. Wazee na viongozi wanahakikisha kwamba watu wanaishi katika hali ya uadilifu.Kutokana na utandawazi tunaona namna ambavyo tamaduni hasa za kimagharibi zimeathiri tamaduni za wazawa hasa katika nchi zinazoendelea. Leo hii si ajabu kumuona kijana wa kiume amesuka nywele,ametoga masikio na hata kuvaa hereni.

Wapo pia mabinti(wasichana) ambao unakuta uvaaji wao hauakisi tamaduni za kiafrika. Unakuta mtu amevaa nguo fupi kiasi kwamba ni aibu hata kupita mbele za watu ila yeye anajiona sawa kabisa. Mtu anatembea viongo vya mwili wake vipo nje kiasi kwamba jamii hasa watoto wanashindwa kujifunza maadili yaliyo mema kutoka kwao. Hii yote inatokana na athari za utandawazi hasa kutokana na maendeleo ya vyombo hivi vya kupashana habari.

Tunajua kwamba wasanii ni kioo cha jamii lakini mambo yamekuwa tofauti hao ambao wanatakiwa kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kutunza tamaduni zetu lakini baadhi Yao wamekuwa wakifanya tofauti na mategemeo ya jamii. Unakuta msanii kavaa nusu utupu, na hata maudhui ya nyimbo wanazoimba(baadhi Yao) yanakuwa kinyume na maadili. Sio hao tu wapo pia wadau wanaojihusisha na masuala ya habari kusema ukweli hili nalo linawahusu.

Unakuta mtangazaji wa kipindi fulani cha runinga yupo hewani lakini mavazi aliyovaa Kulingana na maadili yetu hayangepaswa kuvaliwa akiwa hewani ukizingatia wapo wanaotazama kipindi husika na miongoni mwao ni watoto na hata wazazi(huenda ikawa hata wazazi wa mhusika wanaangalia pia) Je wazazi na hata uongozi wa chombo husika wameshindwa kukemea au hata upande wa utawala unaohusika kusimamia wizara husika? Sio hayo tu pia Lugha ya asili ya Kiafrika kikiwemo Kiswahili, zimedhoofishwa na lugha za kigeni kama Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani n.k Kiingereza kwa mfano, kimekuwa lugha ya utandawazi kiasi kwamba inatazamwa na Watanzania wengi wanaoweza kuizungumza kuwa ni ishara ya ustaarabu. .kwa kufanya hivyo lugha zetu za kienyeji kikiwemo Kiswahili zinaachwa au kuachwa zitumike na watu wenye elimu ndogo ambao nao wanatamani wangejua Kiingereza.

Ukosefu wa ajira.

Karibu katika nchi zote zinazoendelea zaidi ya nusu ya watu wanaofanya kaki wanategemea kazi za kawaida mfano kwenye viwanda nk lakini kutokana na utandawazi kuota mizizi maendeleo ya teknolojia yamepunguza ajira na kuongezea hitaji la kimataifa la wataalamu wenye ujuzi.

Tumeshuhudia matumizi ya teknolojia mfano matumizi ya roboti katika viwanda, matumizi ya kompyuta maofisini, matumizi ya(mashine) trekta kwenye kilimo katika ulimaji , palizi na hata uvunaji(japo maendeleo kama haya yameongeza uzalishaji ukilinganisha na kilimo cha mkono ) Kutokana na utandawazi wapo ambao wameachwa kwanye ajira(japo ukiangalia upande shilingiwa pili wa shilingi utandawazi huibua pia ajira) na kushindwa kukidhi mahitaji Yao ya msingi na kusababisha kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu Kama vile wizi uporaji, mauwaji na matumiza ya sawa za kulevya.

Kushamiri kwa matukio ya kigaidi. Hili ni tatizo kubwa kwa nchi zinazoendelea. Kutokana na ushirikiano wa dunia unaowezesha watu wa mataifa tofauti kutembeleana(ukizingatia maendekeo ya njia za usafiri kwa Sasa ni ya kiwango cha juu) imekuwa jambo la kawaida kwa baadhi ya watu kuhamia nje nchi za kwa ajili ya masomo, biashara, kutembelea ndugu, kazi na kupata huduma za hospitali.

Hata hivyo si wote waaminifu wapo wasio waaminifu wanaotumia mianya hii kuingia katika nchi husika wakiwa na lengo lililofichika ikiwa Ni pamoja na kufanya mashambulio ya kigaidi jambo ambalo limepelekea changamoto ya kutoaminiana baina ya mataifa na hivyo kuwekwa masharti magumu kuingia katika nchi mbalimbali.

Utandawazi umesababisha ongezeko la joto duniani kutokana na ongezeko la joto polepole linalosababishwa na utoaji wa gesi kutoka viwandani na magari. Gesi hizi huzuia joto kutoka kwa uso wa dunia hadi angahewa.Ongezeko hili la joto wakati mwingine limekuwa likisababisha vifo,na pia kupunguza kwa theluji ya Milima maarufu Kama Kilimanjaro nk

utandawazi pia kwa namna moja au nyingine umedhoofisha juhudi zinazofanywa na nchi zinazoendelea kama Tanzania kuunda mashirika yenye nguvu ya kisiasa kama vile Umoja wa Afrika au Jumuiya ya Mashariki kwa sababu ya kuenea kwa nyanja za masilahi kwa kanda na mataifa makubwa kama Amerika na Ulaya Magharibi. Matokeo yake baadhi ya nchi zinazoendelea zimependa zaidi kushirikiana na nchi za kibepari badala ya nchi jirani .

Kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania biashara huria husababisha kuzorota na chini ya maendeleo ya sekta ya viwanda na teknolojia ya ndani. .kushuka kwa sekta ya viwanda na teknolojia ya ndani kunasababishwa na utitiri wa bidhaa kutoka nje ambazo bei yake ni ya chini, ilhali zikiwa na ubora wa juu kuliko bidhaa za ndani.

Uwepo wa makampuni ya kimataifa katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania usipodhibitiwa vyema unaweza kupata faida kubwa kwa kuwanyonya wananchi na kuwaacha maskini. Baadhi ya makampuni yanaelekea kuwanyonya wananchi kwa kulipa mishahara midogo kwa wafanyakazi wa ndani ikilinganishwa na wageni. .pia baadhi ya makampuni yanakwepa kulipa kodi kwa serikali hivyo kuinyima mapato.

Kuyumba kwa bei. Kuyumba kwa bei ni athari mojawapo ya utandawazi kwenye biashara.Baadhi ya watu wamekuwa wakianzisha viwanda ndani na hata nje ya nchi ambapo wanapata malighafi ya bei nafuu na hata vibarua. Wanaweza pia kupunguza gharama za uzalishaji na kuuza bidhaa zao kwa bei nafuu. Kwa sababu ya ushindani baadhi ya bidhaa za ubora wa juu hutofautiana bei licha ya asasi mbalimbali ikiwemo shirika la biashara ulimwenguni kujaribu kudhibiti kushika kwa bei mara nyingi juhudi hizi hazifaulu.

Makampuni hayayanawezafikia watumiaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa, Biashara zinazofanikiwa ni za wale wanaoweza kupata faida ya ushindani na hasa kwa kutengeneza bidhaa za ubora kwa bei ya Chini. Kwa kuhitimisha Ni vizuri itambulike kuwa dunia kila uchao inabadilika, maendekeo hasa ya sayansi na teknolojia yanaongezeka. Lakini maendekeo haya yanaleta matokeo chanya na matokeo hasi jamii haina budi kuyapokea matokeo chanya kwa mikono miwili na kujihadhari na matokeo hasi.

Aksanteni na ni Imani yangu kwamba kwa haya machache jamii itaweza kuyazingatia na mwisho wa siku jamii itaweza kutoka hatua moja hadi nyingine.

Karibuni kwa mjadala na naomba kura yako kupitia kimshale ^ hapa Chini👇
 
Upvote 0
Back
Top Bottom