UTANGULIZI WA BIBLIA

UTANGULIZI WA BIBLIA

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
.

Karibu binti na mwana wa mama Afrika.

Ili kumuelewa Mungu wa Biblia ni lazima kwanza kuielewa Biblia, chanzo na asili yake.

Wengi wananiuliza binafsi naamini nini kuhusu Biblia na mahusiano yake na Mungu.

Kwa wanaofuatilia post zangu, sijawahi sema Biblia na Quran si vitabu vya Mungu, Mnielewe hapo.
Kawaida post zangu huwa zina hoja mbili kuu kuhusu Biblia na Quran.

Hoja ya kwanza ni kuwa Biblia na Quran si vitabu vya Wazungu na waarabu bali ni maandiko ya waafrika weusi.

Kwa nini waliamua kutumia maandiko yetu ili kututawala.
Sababu kuu toka zama mtu mweusi ndiye anamjua Mungu na alikuwa na mahusiano naye kwa usahihi, hivyo hata akipoteza mahusiano naye huwa anamtafuta kwa bidii.
Huo ni udhaifu wa asili wa mtu mweusi, ndiyo maana, sehemu ambayo unaweza kumdhuru mtu mweusi na asilalamike ni katika jambo linalohusishwa Mungu.
Na kwa kujua hilo mkoloni Kawekeza sana katika dini ili kutugawa na kututawala kirahisi.
Kwa namna ileile ya kuigawa Afrika vipande vipande ili aitawale kirahisi, ndiyo anatumia dini kutugawa ili atutawale kirahisi.
Uliza wenye kujua, hati za mkataba wa Berlin wa kuigawa Afrika vipandevipande upo wapi kama si Vartican.
Kwa nini zimehifadhiwa huko, kaulize Polisi.
Ndiyo maana nikakwambia Quran na Biblia ni kitabu kimoja ila walikigawa na kukipanga vibaya, Ili unabii utimie.

Nyuma ya pazia upangaji mbovu ndiyo maana ya kubadili siku na nyakati.
Nyakati ni zama, Zenye umri wa kati ya miaka 2000 hadi 4000.
Siku ni hizi za kutoka na kuzama jua.
Uliza utofauti kati ya siku za kalenda ya kiislamu na kalenda hii tunayotumia ya kikatoliki.

Kubadili nyakati kuna athari za mzunguko wa zama na historia ya kimungu sababu Maandiko ni ramani ya matukio ya kidunia.
Katika hili wanaofuata kisahihi ili kujua matukio ni wanajimu, usiulize wanajuaje, baada ya matukio fulani yatafuata matukio fulani.
Hivyo wanajimu hawatumii uchawi kama tunavyodhani bali wanafuata mzunguko asili wa kalenda ya kimungu.

Biblia na Qurani ni kati ya kitabu cha kiutabiri( kinabii), kinachowezesha mtu kujua mzunguko wa matukio yake binafsi na matukio ya kidunia na dunia.

Kama Biblia ingepangwa vizuri tungejua hiki ni kizazi Cha ngapi na kinaisha lini kisha kitafuata kizazi gani na kitaisha lini.
Na kila kizazi kina tabia yake, na matukio yake.
Sambamba na kujua wewe ni nani katika hii dunia, utakubwa na matukio gani na kwa nini, mbali na kujua kila kitakachofuata toka kilichopo, itajua poa mwisho wako ni upi katika hii dunia.
Njia hiyo ndiyo walitumia manabii wa maandiko kujua vizazi, matukio, yaliyopita na yajayo, kutia ndani mwisho wa kila kitu, kutia ndani wao.

Ukiona kalenda ya kinajimu ina nyota 12 sawa na biblia ina nyota 12 sawa na makabila(vizazi) 12, sawa na kalenda hii ya kikatoliki ina miezi 12. Kwa wanaojua kuhesabu au kutamka namba kwa kilatini utaona hesabu za miezi zipo kinyume mfano Dechem (desemba ) sio 12 ni 9.

Kubadili siku kuna athari za kimaumbile, miili kushindwa kupokea, taarifa sahihi za kimungu, ikiwa ni pamoja na kufanya ibada fulani, Kutoa sadaka, kufanya mambo, nje ya siku za kimungu.

Ukumbuke siku zinatokana na mzunguko wa mwezi.
Kila hatua moja ya mwezi inaathari katika mwili wa viumbe hai wa dunia.
Kila mwezi unapokuwa na siku fulani kuna jambo inatakiwa ufanye ili kufanikiwa kimwili na kimaisha.
Fuatilia kwa nini mwezi fulani kuna hali fulani ambayo huleta magonjwa fulani.

Na hata hali ya afya ya Dunia huwa ina badirika, upepo, baridi nk.
Ukienda kinyume kuna madhara ya kiafya kutia ndani saikolojia, kwa maana utapoteza hata uwezo wa kufikilia.
Ukitaka uamini hili.
Jenga utaratibu wa kulala vizuri mchana alafu afya yako na mawazo yako, uoanishe na mtu anayelala usiku na kuamka mapema kama agizo la maandiko yanavyosema.
Mfano hai fuatilia afya na saikolojia ya wakristo, waislamu na wafanya kazi wenye utaratibu wa kulala mapema na kuamka kuanzia saa 11 mpaka saa 12 asubuhi.
Wanaofuata siku kisahihi ni Freemason, baadhi ya waislamu, baadhi ya wakristo bila kujua na wanajimu.
Baadhi ya Wakristo na waislamu wengi hawajui nguvu ya saa inapotakiwa kulia hadhana au kengere.
Mida ya hadhana na kengere imetegwa kwa sababu za kiroho na kisaikolojia.
Ndiyo maana adhana au kengere visiposikika ndani ya Muda aviruhusiwi kufanywa kabla au baadaye.

Hoja ya pili Ni kuwa, kile kinachomaanishwa katika Maandiko si maana ile tunayofundishwa.
Tunafundishwa mambo yanayosukuma akili zetu kuwa chini ya wengine, ili kuona mambo kwa namna anayoitaka mkoloni, ndiyo maana, Wakristo wa mapema hawakuruhusiwa kumiliki Biblia Wala kujaribu kutafakari.
Lengo wasitafakari nje ya mawazo ya wakoloni, na hata ukifanya hivyo peke yako, utafungwa na dhambi ya kukufuru.
Yaani kumtafakari Mungu vibaya, Hata ukiwa sahihi.

Siku za hivi karibuni kanisa Katoliki limeanza kuruhusu watu kutafakari lakini bado wamewekewa mipaka kwa kuweka kitabu cha namna ya kutafakari ambayo nayo haitoi haki ya kutafakari mwenyewe bali utafakari kwa kuoanisha na tafakari iliyowekwa.

Tuwe pamoja.
 
Roman Catholic ndio walizuia maarifa mengine yasijulikane kwa watu wengine level ya chini kwa kuyazuia mafundisho mengine au kuhoji maarifa mengine nje ya mafundisho ya Biblia.
Kumbuka Ukristo kwa miaka mingi ulikuwa ni dini ya lazima kwa ulaya ndio umeleta ustaarabu na maendeleo yote uyaonayo Ulaya.
Zama hizi tunapata maarifa mengine nje ya Biblia mfano elimu za kale za Wakermit waMisri wa kale,na elimu zingine kongwe kabla ya Biblia.
Ushauri elimu ni nyingi zama hizi za mwisho ukisema uzifate zote utachanganyikiwa utatoka nje ya mstari we tafuta maarifa Yale tu yanayokufaa kwa wakati wako.
 
Siyo tu roman catholic hata dhehebu lako ukija na tafakuri lako na likaonekana ndani yake lina nguvu basi hutoboi.

Ni figisu au kukuondoa kwenye hilo dhehebu, iwe ni KKKT, SDA, Uislam nk.
 
Roman Catholic ndio walioamua Biblia hii ndo itumike duniani kwa kupiga ban Biblia zingine zenye machapisho vitabu vingine vya ujuzi na maarifa kwa ajili ya mind control mfano kuna ya Ethiopian Bible ina vitabu 88 nk.
Na elimu zingine za siri huwezi zipata kama wewe sio members wa secret society nk.
Pana vitabu vimebeba siri za ufunguo wa mfalme sulemani alifanya nini ili kuwa na nguvu,mapiramidi nani waliyajenga,miaka 18 ya Yesu iliyopotea nk.
Biblia ni coded books imebeba siri za dunia na funguo mbalimbali za maisha.
Ukiona Mkristo ni masikini shida sio maandiko bali ni yeye amekosa maarifa ya kuzifungua hizo codes.
Kila andiko ni coded vipo vitabu vingine vinaivunjavunja hio code unapata maana ukiifanya kwa vitendo unapata matokeo
 
Vitabu vyote vingewekwa kwenye Biblia ingefikia uzito wa tani moja so isingebeba,thus waliacha tu vile muhimu tu kwa watu wa level ya kwanza ya ufahamu.
Huwa nashangaa sana wasabato kutwa wanawachallenge wakatoliki ambao wameitunza Biblia kwa zaidi ya miaka 2025 duniani bila wakatoliki Biblia isingekuwepo duniani
 
Hii ni Ethiopian Bible inatumiwa na madhehebu ya Coptic wa Ethiopia.
Roman Catholic iligawanyika matawi matatu Pana Roman Catholic makao makuu ni Vatican,Pana Orthodox makao makuu ni urusi na Pana Coptic church hawa ni Ethiopia
 

Attachments

  • FB_IMG_1741620495625.jpg
    FB_IMG_1741620495625.jpg
    65.6 KB · Views: 1
Roman Catholic ndio walioamua Biblia hii ndo itumike duniani kwa kupiga ban Biblia zingine zenye machapisho vitabu vingine vya ujuzi na maarifa kwa ajili ya mind control mfano kuna ya Ethiopian Bible ina vitabu 88 nk.
Na elimu zingine za siri huwezi zipata kama wewe sio members wa secret society nk.
Pana vitabu vimebeba siri za ufunguo wa mfalme sulemani alifanya nini ili kuwa na nguvu,mapiramidi nani waliyajenga,miaka 18 ya Yesu iliyopotea nk.
Biblia ni coded books imebeba siri za dunia na funguo mbalimbali za maisha.
Ukiona Mkristo ni masikini shida sio maandiko bali ni yeye amekosa maarifa ya kuzifungua hizo codes.
Kila andiko ni coded vipo vitabu vingine vinaivunjavunja hio code unapata maana ukiifanya kwa vitendo unapata matokeo
Upo sahihi ila nadhani hata hivi vilivyopo 66 vina full code na ndiyo maana ukionekana unachimba sana humo ndani ya dhehebu lako unafukuzwa au kuambiwa 'unaleta mafunuo mageni' au 'unaanza kupotea sasa'.

Wakiona unazidisha unaitiwa polisi daaa 😂!

Vinginevyo hakuna muanzilisho wa hizi imani ataruhusu uliye ndani ya imani yake ulete kitu kipya ukiwa humo ndani, ndiyo maana unaona watu wanafukuzwa makanisani au misikitini.

Hao waethiopia wapo Afrika na wana imani yako tofauti na hizi tulizo nazo Tanzania lakini wana survive nayo na hakuna mbanga yoyote!.
 
Chanzo cha madhehebu ni watu kufungua hizi codes za kwenye Biblia so unaonekana unakwenda kinyume na waasisi wa imani au unafukuzwa unaenda anzisha la kwako
 
Back
Top Bottom