Utani na Msichana ninaye fanya naye kazi unataka kunivunjia ndoa yangu

ukome!
Yaani nimepata hasira mpaka na-vibrate!
Utani gani huo, je ingekua ni mkeo anataniwa hvyo na kidume cha ofsn kwake ungejisikiaje?
Kila uhusiano una mipaka ww na huyo mate wako hamna mipaka? Hv ingekua wife hajaiona msg ungemjibu vp mate wako?
 
ingekuwa ni mm, kwanza kama kweli huyo rafiki wa ofisi hatuna mahusiano na ni rafiki kweli nitamuomba tuongozane nyumbani, aongee na mamsap wangu ili ukweli ujulikane....
si ana simu alyotumia kunitext? tutaona sent items au namba zake zitaprove. ila kama atakataa kwenda, nitajua hakuwa rafiki ila alkuwa na nia nyingine kwangu. Ila pole sana..
 
sasa meku...shimbonyi shafoo...sasa aisee kwanini aisee unaleta utani kwenye ndoa aisee mekuuu....halafu inaonekana wife ni mkali sana aisee mana unaogopa kabi kabisa kumsogelea na kumueleza ukweli....sasa aisee umeshalala gesti utamueleza vipi hukulala kwa huyo malaya wako aisee...rudi ho home mueleze banaaa kwa utaratibu atakuelewa.....acha kuwa lege lege mekuu. pole sana aisee
 
rudi nyumbani mkayazungumze...... utaishi hotel mpaka lini.....unavyozidi kuwa nje ya nyumbani unazidi kuharibu
 
Hata mimi nawaambiaga rafiki zangu hakuna utani kati ya mtoto wa kike na wa kiume wananiona mnoko. Mimi ukimtania mume wangu sikukopeshi. Wanaanzaga hivo hivo! Singles wameisha mpaka ukatanie mume/mke wa mtu. Eti umwite mume wangu honey! We! SItakuelewa kabisa nakuweka kwenye wanted list yangu!

Ni obvious hizo ni dalili za kunyemeleana. Utani my foot. Utakuta mijitu inaongea mambo ya chumbani kabisa tena wanaongelea wake na waume zao kwa hao the so called watani. Mimi uwa nawacheki, kimoyo moyo nasema ole wenu mumtanie mume wangu. NAWATOA NISHAI LIVE. Tunaona watu wa hivo makazini na in most cases ni wale maharage ya mbeya ndio wanapenda mambo ya utani. Ikitokea ukabug step tu unalo. UKIMWI UTATUMALIZA.

 
Kuna mdada mmoja ofisini ni dirvocee huwa namsikia anaongea na waume za watu kwenye phone, yaani napata hasira on behalf. Anaongelea mambo ya faragha kabisa so tempting. Afu akimaliza anasema huyu kijana tunatanianaga. Ni full matusi. Ni sawa na kuangalia movie za X na mume/mke wa mtu. Maanake asojua kuwa matani yanaamasisha nani?
 

damn!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!stpid husband
 
Heee! Pole, utani mwingne usivuke mipaka na minyau.
 
Wahi Loliondo tu mkuu
 
Tena kama wewe nyumba kubwa, mumeo ndiyo rahisi kwelikweli! basi tu hujui
 
mrs mkali hivyo.huyo dada wa ofisini ulimzoesha vibaya,matokeo yake umelikoroga.mpe muda mke wako,muelezee hali halisi,ingawa itachukuwa muda sana kukuamini.maana msg ni ushahidi tosha,haijalishi kama mnataniana au hamtaniani,maana kwa hayo maneno,hata mimi ningehisi huyo ni mpenzi wako tu.na huyo dada muambie kuanzia leo,wewe na yeye matani basi,hata ofisini msitaniane,sio kwa huyo tu,hata kwa wasichana wowote wale,wewe sasa umeoa, jaribu kujiwekea mipaka unapozungumza na wasichana wengine.maana wadada wengine ukimregezea kidogo,kosa kama hilo linaweza kutokea au zaidi ya hilo
 

Sio aishie ofisini tu! Yaani aache kabisa utani na huyo binti. Watu wengine hawataniwi ati! Kwa mtu anayejua kuwa huyu ni mmilikiwa wa mtu utani huishia mkitoka mjengoni mnakopiga mzigo. Kaa naye mbali ana dhamira ya kuwa mama mwenye nyumba babu!
 
Mimi nimeshtuka kusikia hivyo ila kwa sababu sina facts nimebaki kuguna tu!!!
Asavali umesema...one of my investments ni mmachame sasa nlishaanza kuogopa.

mmeambiwa mtalijua Lima kilimanjaro nyie sio Jiji tena....Huyo kaoa Bondia acha akome...umeoa Bondia unataka kuchakachua?
 

huyu jamaa anaye Chele...wewe umeoa unataniana na mtu kweli kihivyo? mie mfanyakazi mwenzangu tu kuniita kimahabahaba mwiko...sijui honey sijui switie helll NOOOOOOOO....halafu anajua kabisa niko home, mbele ya my wife wangu anatuma MSG kama hiyo? Walah ndoa yangu inatetemeka yeye sijui itakuwaje? Walah atakuja niombea msamaha...
 

Contact zake mie sitamtania...nitamwambia ukweli....
 
Sio aishie ofisini tu! Yaani aache kabisa utani na huyo binti. Watu wengine hawataniwi ati! Kwa mtu anayejua kuwa huyu ni mmilikiwa wa mtu utani huishia mkitoka mjengoni mnakopiga mzigo. Kaa naye mbali ana dhamira ya kuwa mama mwenye nyumba babu!

Utani ni live tu sio kwa msg tena....Niite majina yote lkn sio uniandikie maana written ni ushahidi tosha...mama kaisave text msg akibisha tu, linawekwa live...
 
Kwanza pole,pili mwache kwa muda hasira zikipungua umwambie,jaribu kuwashirikisha watu anaowaheshimu,akishindwa kukuelewa hayo yatakuwa nje ya uwezo wako!Huwezi kubadili hali halisi mzee!
 
Utani gani saa nne ucku? Au hajui kuwa una mke? Lakini mangi mkeo ndio angetumiwa hiyo msg akakwambia utani ungeelewa? Hukupaswa kuondoka home hata kama moto ungewaka vp,rudi home muombe radhi mkeo,siku ukiona hasira zake zimepungua mweleze hali halisi ilivyokuwa. Huyo bint mkumbushe jina lako la kwenye passport na formality ihusike from 2day on wards.
 
Situation kama hizi inabidi huwe mwepesi wa kufikiri....,
ungecheka saaana alafu ukasema kumbe kweli unanipenda.., yaani umeshinda mtego, tulipanga na rafiki yangu tukupime.., hivi kweli wife ningekuwa nategemea sms kama hiyo unadhani ningeacha simu chumbani.., dah kumbe mshikaji alisema kweli mi nilisema wife hawezi kukubali mtego mdogo hivi..., dah wife embu twende tukalale......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…