Rule L
JF-Expert Member
- May 31, 2020
- 1,846
- 2,754
Habari wanajamvi, natumai mmeamka salama salmini.
Kama mada inavyosema, utani hua ni mameno ya hapa na pale,
mara nyingine ni ya ukweli ila yanawasilishwa kwanjia ya utani.
Ila utani mara nyingine huota meno ya sumu na kusababisha ugomvi mkali, pengine mpaka kupigana.
Binafsi kuna kisa Cha rafiki yangu ambaye alifikia pabaya kisa utani.
Ilikua ni Arusha mjini pale maeneo ya mount meru hospital.
Sasa jamaa alikua anatembea tu kwa mguu akawa anakatiza pale maeneo ya mochwari, akawa anapishana na watu wamebeba jeneza .
Wale jamaa kutokana na msiba kuwavuruga wakamfokea jamaa yangu kwamba, we mpuuzi unaona tumebeba jeneza alafu nawewe unajipitisha tu, we mwehu nini??
Jamaa yangu akaangalia pale watu walivyo wengi mixer piss kali akaona usinitanie Mimi mwenyewe nipo vizuri kwenye maneno.
Akawaambia mnanitukana kwakosa gani? Kwani hii si njia?? Mtu wenu kajifia na ukimwi huko mje mnitukane Mimi? Sikumwambia akafanye umalaya. Nendeni mkafukie huko
Nyie mabwege nini.
Baada ya hapo palichimbika kwanza kabisa wale jamaa wakashuasha jeneza chini alafu wakamwambia huyu si amekufa kwa ukimwi wewe tunakuua sisi 😆😆😆😆😆 Mimi ilibidi nicheke sana wakati ananisimulia.
Wakaanza mbio walimkimbiza kutoka pale mochwari hadi maeneo ya clock tower pale nmb bahati nzuri akakuta kuna magari yamepark pale akajificha chini ya uvungu wa gari, pale kulikua na mdada ambaye wanasimamiaga ushuru wa parking.
Akamwambia kuna watu wananikimbiza wakija waambie ameenda.
Mara kidogo jamaa Hawa hapa wakamuuliza yule dada akawajibu ameelekea upande ule. Wakaangaza angaza hawakumuona ikabidi warudi. Akawa anasawasikia wanaosema tule mjinga ana MUNGU ilikua afe Leo yaani mama yetu kafa kwa ukimwi, pumbavu kabisa.
Baada ya hali kua shwari jamaa akatoka akaanza safari yake,
kila nikikumbuka huaga nacheka sana, maana jamaa alivyoniona tu alicheka vibaya mno alafu akanimbia jamaa yangu Leo ilikua nife usingiona nikiwa hai tena nikamuuliza kwanini ndo akanipa huo mkasa.
Mi naona hapo kila mtu alikua ana kosa, wenye msiba walizingua jamaa yangu naye akaja akazingua zaidi.
Muwe na siku njema