DMmasi
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 561
- 900
Salam wanajamii hasa jukwaa hili la michezo, niende kwenye mada moja kwa moja.
Timu zetu pendwa watoto wa kariakoo wako kimataifa wameshacheza mechi tatu kila mmoja na matokeo tunayo yote. Tukiwa kama mashabiki wa hizi timu utani wetu unaenda hadi huko kimataifa hakuna wakumshangilia mwenzake uko kimataifa hata mimi sina huo mpango.😀
Siku za karibuni kumekuwa na mfumo wakuambiana umecheza na kibonde ndiyo maana umeshinda mbona alipigwa hivi mara vile.
Nadhani kuna muda tukae tusifie zaidi timu zetu kuliko kuja na hizi sababu za kusema mmecheza na mserereko, mara uchawi, mara mlitembeza bahasha. Simba ikishinda ninafurahi na nikikutana na shabiki wa Yanga nacheka kwa nguvu maana najua amekerekwa na upande wao iko ivyo pia.
Ushauri wangu kwa mashabiki, tuzitetee sana timu zetu kuliko kutania zaidii upande wapili.
Kishabikii tukiongea sasa hivi nitasema kwa kujiamini na kwanguvu zote kwamba Simba tumeshaenda makundi
ila kimpira najua bado kazi yakufanya ipo pale taifa.
Hivyo hata mtani simameni mkisema kwa kujiamini mnaenda pindua meza licha sisi tutawajibu hakuna kitu ila jijengeeni imani. Mfano video zile zinazosambaa baadhi ya mashabiki wakijieleza tayari wamekata tamaa hata zinafika mbali na wachezaji pia wanaziona wanaeza jijengea picha kuwa tayari shabiki wameshakubali
Tusiwe wepesi sana wa lawama tuvumilie tukipata tusichotamani.
Matamanio yangu ni hata mtani aende makundi kama siyo klabu bingwa basi hata shirikisho ili na wao wawe na mechi nyingi za kufikiria.
Mpira unamatokeo matatu yakija yoyote tuyapokee, naondoka kwa mwendo wa kiwendawazimu.