njundelekajo
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 310
- 227
1.UTANIKUMBUKA
1, Nikazibeba dhihaka, kukusitiri na chuki.
Nikaitwa jina paka ,na mengi sana matusi.
Lawama nikajivika, nikazidisha juhudi.
Umenisahau Leo, kesho utanikumbuka .
2. Kwa ahadi kemkem,wewe ndiwe mkombozi.
Utaleta chemchem, na maji ya tangawizi.
Hosipitali makumi, sipate shida wazazi.
Umenisahau Leo, kesho utanikumbuka.
3. Maneno yenye bashasha, yakakita moyo wangu.
Imani namshawasha, kukupigania wangu.
Mimi na bwana Kalasha, dua ushinde kwa mungu.
Umenisahau leo, kesho utanikumbuka.
4. Mitaani kama wehu, pita kukupigania.
Shindia mazambarau, njaa hatukusikia.
Bure bila hata dau, ushinde wewe ndo nia.
Umenishau leo, kesho utanikumbuka .
5. Mungu sio Athumani, ushindi ukaupata.
Mbio mpaka bungeni, kiapo ukaapishwa.
Katu bado siamini, kama ni wewe kabisa.
Umenisahau leo, kesho utanikumbuka.
6. Gari kioo hushushi, wala mwendo kupunguza.
Wavimba kama furushi, na wazidi kupendeza.
Zako za gharama suti, ulaya wazishonesha.
Umenishau leo, Kesho utanikumbuka.
7. Nyuma umepasahau, mbele wapakazania.
Umezidisha dharau, wengi tunakuchukia.
Unatunga manahau, ukiombwa tembelewa.
Umenisahau leo ,kesho utanikumbuka .
8. Umenifanya mbachao, chaguzi ilipokwisha.
Bado napiga mihayo, mwenzangu unabashasha.
Nangoja kura ijayo, unifate na mapesa.
Umenisahau leo, kesho utanikumbuka.
9. Miaka tano si mingi ,miwili mebakia.
Jatimiza mambo mengi, kura nikakugaia.
Pale shule ya msingi,bado chini wakalia
Umenisahau leo, kesho utani kumbuka.
10. Kawatumie wengine, Mimi nishakua janja.
Unazidi kua nene, Mimi nazidi kukonda.
Nashindia masenene, mihogo, ugali chunga.
Umenishau leo, kesho utanikumbuka.
11. Hali ngumu vilevile, maji nachota mtoni.
Walimu hakuna shule, wala dawa sipitalini.
Likizo ughaibuni, china na ujerumani.
Umenisahaul eo, kesho utanikumbuka.
12. Jimboni huonekani, bungeni kutwa kulala.
Washinda mitandaoni ,eti ni mbunge bora.
Najicheka tu moyoni, jinsi nlivyokua fala.
Umenisahau leo, kesho utanikumbuka.
13. Siasa zigo la mavi, kulibeba mi sitaki.
Kutwa kufuatwa na Inzi, wewe wala misikaki.
Bora nitafute kazi, nilipwe iliyohaki.
Umenisahau leo, kesho utanikumbuka
Nguzo Noel.R.