SoC02 Utaoji wa mikopo kwa Wahitimu wa elimu ya juu nchini

SoC02 Utaoji wa mikopo kwa Wahitimu wa elimu ya juu nchini

Stories of Change - 2022 Competition

Shajumu

New Member
Joined
Aug 24, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Utangulizi
Chagamoto ya ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu nchini imekuwa ni tatizo sugu ambapo kama lisipotafutiwa ufumbuzi basi linaweza kulitumbukiza taifa katika dimbwi la unyang’anyi na waporaji na kuwa nchi ya wahalifu maana tunaona wasimamizi na watunga sera ambao si tu wamepewa mamlama ya kutunga na kusimamia sera hizo bali wamekosa ubunifu wa kuhakikisha wanaandaa mazingira wewezeshi kwa wahitimu wa vyuo vikuu kuwaweza kujiajiri badala ya kusubiri nafasi za ajira kutoka serikalini ambazo nazo zimekuwa zikitolewa kwa upendeleo au kwa kufahamiana na kama huna Ndugu anayefanya kazi au kujuana na mamlaka zilizotangaza nafasi za kazi basi utaishia kufanya tu mahojiano na kurudi nyumbani kwenu maana tumeona nafasi za utendaji zilizotangazwa juzi zilikumbwa na mizengwe ya ajabu ajabu lengo tu kuwalenga na kupitishwa wale tu wanaowataka na kuwakusudia wao.

Tunayo wizara ya kazi, vijana na ajira lakini hatuoni kwenye bajeti yake akizungumzia mikakati ya kutoa ajira kwa vijana wanaohitimu elimu mbalimbali kutoka vyuo vikuu bali tunaona maneno yasiyonastaha kutoka kwa wabunge wakati wakichangia michango yao bungeni ambao ndio wawakilishi wa wananchi wakiwemo vijana kwa kuwaambia hawataki kujiajiri bali wanasubiria kuajiriwa hali yakuwa wao kama watunga sera na wasimamizi wa utekelezaji wa sera hizo hawaoneshi juhudi zozote katika kuwatengenezea mazingira wezeshi kwa wahitimu kuweza kujiajiri.


Utaoji wa mikopo kwa Wahitimu wa elimu juu nchini,Mabadiliko chanya ambayo yanaweza kufanywa kuhusu kuhakikisha vijana wanaohitimu masoma ya elimu ya juu waweze kuthaminiwa na kutengenewa bajeti kila mwaka ili waweze kukopeshwa kwa ajili ya kwenda kuanzisha biashara na kutengeneza ajira kwa wengine .kwani vijana wengi wanahitimu vyuo vikuu hawana mahali pakuonesha thamani ya elimu yao katika kulisaidia Taifa matokeo yake wamekaa kwenye vijiwe vya kahawa pasipo hata kujua kesho na thamani yao katika maisha na familia zao hii imewafanya vijana na wasomi wengi kuishia kwenye kucheza michezo ya kubashiri jambo ambalo ni hatari na linaweza kulidumbukiza taifa kwenye janga la uhalifu


Mabadiliko chanya ambayo yanapaswa kufanywa ili kuweza kuwanusuru vijana wanaohitimiu ili elimu na maarifa waliyonayo yaweze kuleta tija na ustawi katika Jamii kwa yetu ni kuwezeshwa mikopo mara tu baada ya kuhitimu elimu zao kwa ajili ya kwenda kuanzisha biashara ili waweze kujiajiri na kujega kesho yao maana kama serikali imeweza kugharamia kwa kuwapatia mikopo ya elimu ya juu kwa muda wa miaka miatatu,minne na wengine mitano kupitia Bodi ya mikopo ya elimu ya juu inashindwa nini katika kuwakopesha wahitimu hao baada ya kuhitimu masomo yao ili waweze kwenda kujiajiri na kutengeneza ajira kwa watu wengine


Muda wa kutolewa kwa mkopo kwa wanufaika,Ili kuleta mabadiliko chanya kwa vijana na wahitimu wengi kama serikali inapaswa kuwakopesha tena pindi wanapohitimu aidha kupitia Bodi hiyo hiyo ya mikopo au kupitia wizara ya ajira na vijana ili wahitmu waweze kutumia mikopo hiyo kwa ajili ya kuanzisha biashara ambazo nazo zitakuwa na mchango katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo katika taifa letu na sio hivyo tu bali hata bodi ya mikopo itakuwa na uhakika kwa wateja yaani wahitimu waalionufaika na mikopo kuweza kurejesha/kulipa mikopo yao tofauti na sasa hivi kuwasubiri hadi wanufaika wa mkopo waweze kuajiriwa ndio walipe mikopo .hata hivyo mapato ya nchi yataongezeka kwani biashara ambazo zitaanzishwa na wahitimu hao zitalipa kodi na ushuru ambao utaiongezea serikali mapato ,mathalani kila mwaka wahitimu takribani 80,000 huhitimu elimu ya juu na kama wakipatiwa mikopo ya kuanzisha biashara tayari watakuwa wanaingiza mapato kwa mwaka zaidi ya bilioni 12 hivyo serikali itakuwa imetengeneza chanzo kipya cha mapato.


Wanufaika wa mkopo ,Mkopo wa wahitimu elimu ya juu sio lazima utolewe kwa wahitimu wote waliohitimu bali ni kwa wale wahitimu ambao watakuwa na wazo la biashara na ambalo limefanyiwa utafiti na mhitimu mwenyewe na kuandaa mpango biashara anayoenda kuifanya ambayo atayawasilisha kwenye idara ya biashara kwenye chuo husika ambayo yatapitiwa na kupitishwa na wasimamizi/seneta ya chuo na pindi wakijiridhisha nayo ndio apatiwe mkopo huo na kwenda kufanya kile alichokifanyia utafiti ili akafanye vizuri zaidi kwani tayari atakuwa anauelewa wa kile anachoenda kufanya.


Utafiti wa wazo la biashara utaofanya vipi Ni swali ambalo kila mtu atauliza hapa ni kwamba vyuo vingi vinautaratibu wa wanafunzi kwenda kwenye mafunzo kwa vitendo na uanagenzi kwenye ofisi mbalimbali ili kupata uzoefu .Hivyo basi kuliko wanafunzi kwenda kwenye mafunzo kwa vitendo na uanagenzi kwa ajili ya kupata uzoefu ni vyema sasa miatala ya vyuo iboreshwe kwa muhula wa mwisho wanafunzi waende kufanya tafiti kwenye wazo biashara.Kabla ya muda wa kwenda kufanya utafiti kufika mwanafunzi atapaswa kuwasilisha mhutasari wa wazo lake la biashara kwenye idara husika kwenye chuo husika ili liweze kukaguliwa na kuboreshwa kwenye mapungufu ndipo aruhusiwe kwenda kulifanyia utafiti wa wazo hilo na mwishoni atawasilisha matokeo ya utafiti na alichokipata na kutathiminiwa na seneta ya chuo na ndipo aweze kupatiwa huo mkopo wa biashara baada ya kuhitimu masomo yake.


Ufuatiliaji na Uthamini wa wanufaika wa mkopo,Mabadiliko chanya ili yaweze kufikiwa kwa ufasaha lazima utawekwa mfumo wa ufuatiliaji na uthamini wa mkopo huu kwa wahitimu utakuwa chini ya bodi ya mikopo,wizara ya kazi,ajira na vijana na mamlaka za serikali za mitaa hapa namaanisha wakuu wa Mikoa ,Wilaya,Watendaji kata /shehia/vijiji/mitaa na wenyeviti wa mitaa na vijiji kwa maana katika utafiti wa wazo la biashara mnufaika wa maombi ya mkopo ataonesha eneo ambalo biashara yake itafanyika hivyo bodi ya mikopo/Wizara kazi,ajira na vijana itazitaarifu mamlaka husika katika eneo hilo ili kuweze kuwafuatilia na kutoa taarifa na maendeleo yao.


Hitimisho ili mpango huu uweze kuleta tija na ustawi unahitaji serikali kuwajibika kwa dhamira ya dhati na kuhakikisha inaelekeza nguvu kwa kuwekeza zaidi kwa vijana ili tuwe na taifa lenye kujitegemea kwenye uchumi kwani vijana na wasomi hao wakitumia maarifa yao katika kuzalisha basi pato la taifa litaongezeka kwa maana watafanya biashara kwa weledi kutokana na kuwa na ujuzi wa kuweza kukabiliana na changamoto na vikwazo mbalilimbali .si hivyo tu serikali ikitoa mikopo kwa wahitimu hao ndio imemaliza kazi yake hapana itapaswa kuendelea kuwatengenezea mazingira wezeshi kwa ajili ya kufanya biashara kwa urahisi zaidi hii ni pamoja na kuboresha miundombinu na kupunguza utitiri wa kodi na kupunguza urasimu katika utoaji huduma kwenye mamlaka za serikali.​

By Shajumu
 
Upvote 1
Back
Top Bottom